Umoja wa Ulaya wataka Serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK) Zanzibar

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
ambassadoreu.JPG


Umoja wa Ulaya(EU) umeishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupendekeza kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Van de Geer amesema kuwa anategemea mkwamo wa kisiasa kati Serikali ya Zanzibar na Chama Kikuu cha Upinzani Visiwani humo CUF kutatuliwa siku za karibuni.

Balozi de Geer amesema kuwa Umoja wa Ulaya uko kwenye mazungumzo na Serikali ya Rais John Magufuli na Umoja huo unategemea Rais Magufuli ataanzisha majadiliano kutatua mgogoro uliopo na hatimaye CUF kuingizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia tamati baada ya Uchaguzi wa Marudio, tarehe 20, Machi 2016 baada ya CUF kususia uchaguzi huo kwa madai kuwa wa Oktoba 25, 2015 uliofutwa walishinda na wa marudio ulikuwa hauko kisheria na usingekuwa huru na haki.

Umoja wa Ulaya umepunguza mahusiano yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein tangu Ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya uliokuwa ukiongozwa na Bi. Judith Sargentini kupinga Uchaguzi wa Marudio wa Machi 20, 2016.

Chama cha CUF ambacho kinaonekana kiko tayari kwa ajili ya mazungumzo, Serikali ya Zanzibar imewahi kukaririwa ikisema kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK) ilishazikwa, japokuwa inatambuliwa na Katiba ya Zanzibar.
 
Kuna watu watakuja kuwashutumu wakati hali ya uchumi ikiwa mbaya wapeleka huko bakuli

Uwa tu najiuliza hivi kama tunapenda kuwashutumu wazungu kwa kila kitu kwanini tusiwashutumu na wanapotoa misaada tuwaambie warudishe kwao?...

Kwanini UK walifikia kutoa 6 billion za tetemeko tukazitia mfukoni hata bk hazijafika? ..........
 
Hawa Wanataka Kum 'Drive'.?
Hawajui Hajaribiwi wala hana shida ya Misaada yao ..
 
wangeanza kwanza na DRC,Central Africa,Somali,Sudani kusini,Libya kwani huko ni tatzo zaid ya Tanzania kma kweli wana nia njema nasi.
Aisee! ..kwa hiyo unataka na sisi tufike huko alafu ndio waseme!? Kumbuka huu ni ushauri na sio amri.
 
Hao Umoja wa Ulaya wamepoteza Mwelekeo. Kama wameshindwa kuidhibiti Uingereza watawezaje mambo y Tanzania?
Mkuu,siasa bora sio kudhibitiana,siasa bora ni kuwanufaisha wananchi,hali ya Zanzibar ni mbaya sana wananchi wanateseka,lakini bado wanasiasa wanarushiana vijembe badala ya kutafuta suluhisho.

Samahani mkuu,tafiti zinaonyesha siasa za nchi za kiafika kusini ya jangwa na Sahara ni mbovu,maana yake wafrika hatuwezi kujitawala,na ndio maana mpaka leo nchi za Afrika chini ya jangwa la Sahara maskini wa kutupwa.

Kila mtu anajua,Dunia inajua nini tatizo la zanzibar,badala ya kulitatua wanasiasa wanapiga ngonjera kwa manufaa yao binafsi.
 
Back
Top Bottom