Umoja wa Ulaya wasisitiza kutomtambua Mugabe wa Zimbabwe

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
54,425
27,208
Umoja wa Ulaya wasisitiza kutomtambua Mugabe wa Zimbabwe

UMOJA wa Ulaya (EU) umesema hautambui serikali ya Rais Robert Mugabe nchini Zimbabwe, kutokana na mazingira yaliyotawala wakati wa marudio ya uchaguzi uliyomrejesha madarakani.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Ufaransa nchini, Jacques Champagne de Labriole alisema umoja huo unaamini kuwa hali ya Zimbabwe hivi sasa zi shwari.


Alisema kuwa katika kipindi cha miezi sita ya Urais wa Ufaransa kwenye EU, itahakikisha kuwa mazungumzo baina ya Chama cha Zanu-PF na Movement for Democratic Change (MDC) yanafanyika haraka, kulingana na mapendekezo yaliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU).


''Iwapo hatua zaidi hazitachukuliwa haraka, EU itaendelea kushawishi vikwazo zaidi, lakini hadi kufikia sasa hatuko tayari kufanya kazi yoyote na serikali ya Mugambe iliyoingia madarakani katika mazingira yenye utata, yaliyojaa udanganyifu na vitisho,'' alisema Lariolle.


Alisema yaliyotokea nchini Zimbabwe wakati wa maadalizi na baada ya uchaguzi wa marudio yanaonyesha wazi kwamba, haukuwa huru na wa haki, hivyo ili serikali ya nchi itambuliwe lazima Mungabe akutane na wapinzani wake haraka.


Aliongeza kwamba, hawaamini kuwa suala la Zimbabwe ni la ndani na kusisitiza kwamba, tatizo hilo linaathiri usalama wa kikanda na kimataifa.
 
Back
Top Bottom