Umoja wa Ulaya wapunguza vikwazo Syria, Libya na Yemen

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
5,192
2,000
Uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kupunguza vikwazo dhidi ya Syria, Libya na Yemen

Kufuatia kuenea janga la corona kote duniani, na pamoja na kuwepo sisitizo la ushirikiano wa kimataifa katika kudhibiti na kupunguza kuenea corona, kuendelea vikwazo vya baadhi ya nchi, ikiwemo Marekani, ni chanzo cha kuvurugika vita dhidi ya corona. Vikwazo hivyo vimezuia nchi nyingi kupata bidhaa na vifaa vya kiafya vinavyohitajika kukabiliana na janga la corona.

Kuhusiana na nukta hiyo, Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa, utapunguza vikwazo dhidi ya Syria, Libya na Yemen ili kusaidia katika vita dhidi ya corona. Vita vingali vinaendelea Libya, Yemen, Syria na baadhi ya nchi zingine pamoja na kuwa kumetolewa miito ya kimataifa ya usitishwaji vita hivyo. Katika upande mwingine kuendelea vikwazo vya Umoja wa Ulaya na Marekani pia kumepelekea hali kuwa mbaya kutokana na kuwa ni vigumu kwa baadhi ya nchi kupata vifaa ya kitiba na kiafya.

Josep Borrel, Mkuu wa Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya amesema vikwazo havipaswi kuzuia oparesheni za kutuma vifaa vya kitiba vinavyohitajika katika kukabiliana na corona. Ameongeza kuwa: "Vikwazo vinaongeza hatari ya kuenea corona katika nchi nyingi hasa Syria, Libya na Yemen ambazo zingali zinashuhudia mapigano."

Kuenea ugonjwa wa corona duniani na kufariki makumi ya maelfu hadi sasa kutokana na ugonjwa huo kumepelekea nchi nyingi kuchukua hatua maalumu za kiafya, kitiba na kutekeleza sheria za kubana maingiliano ya kijamii. Hivi sasa maeneo mengi duniani yamefungwa na kunatekelezwa karantini au sheria za kutotoka nje . Aidha baadhi ya nchi, zikiwemo za Umoja wa Ulaya zimefunga mipaka yao. Kwa upande wake, Shirika la Afya Duniani limesisitiza kuwa, ili kufanikiwa katika kuangamiza ugonjwa wa COVID-19 au corona, kuna haja ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa sambamba na kuangaliwa upya baadhi ya sheria na vizingiti hasa vikwazo.

Michelle Bachelet Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa amesema vikwazo vina taathira haribifu katika sekta ya afya na haki za binadamu katika nchi ambazo zinakabiliana na janga la corona na kwa msingi huo, kwa mara nyingine ametaka vikwazo viondolewe mara moja. Ameongeza kuwa: "Katika hali hii nyeti na muhimu vikwazo vinapaswa kuondolewa au kupunguzwa kwa ajili ya mfumo wa afya duniani na pia kwa ajili ya kulinda maisha na haki za mamilioni ya watu katika nchi ambazo zimewekewa vikwazo."

Pamoja na kuwepo hali ya hatari na miito ya kimataifa, tungali tunashuhudia kuendelea vita na vikwazo. Vita vinaendelea nchini Libya na Yemen, hata baada ya kuibuka ugonjwa hatari wa corona na misaada ya kibinadamu haiwafikii wanaohitaji.

Abd al-Nasser Abu Bakr, Mkuu Idara ya Kuzuia Magonjwa ya Kumbukiza katika Shirika la Afya Duniani amebainisha wasi wasi wake kuhusu udhaifu katika sekta za afya nchini Syria na Yemen na kutahadharisha kuwa, katika mustakabali wa karibu, nchi hizo zitashuhudia kuenea kwa kasi corona.

Hali hii inaripotiwa huku vikwazo vya Marekani dhidi ya mataifa vikiwa ni kizingiti kikubwa katika vita dhidi ya corona. Katika miaka ya hivi karibuni, Mareknai imekuwa ikitumia vikwazo kama silaha ya kukabiliana na nchi ambazo zinapinga sera zake na vikwazo hivyo vingali vinaendelea hata wakati huu wa janga la corona. Iran na Venezuela ni nchi mbili ambazo zinakabiliwa na vikwazo vikali zaidi vya Marekani. Katika hali hii ngumu, utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani umesisitiza kuwa vikwazo vya Iran havitaondolewa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema nchi yake haitaruhusu Iran ipate fedha zake ambazo zinazuiliwa katika benki za kimataifa ili kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

Marekani imechukua msimamo huo katika hali ambayo sababu kuu ya kupoteza maisha watu wengi Iran katika janga la corona ni vikwazo vya Marekani ambavyo vimepelekea kukatika uhusiano wa Iran na mfumo wa kifedha wa kimataifa. Vikwazo hivyo si tu kuwa vimeizuia Iran kupata pesa zake bali pia ni kizingiti kwa nchi hii kununua dawa na vifaa vya kitiba. Kama alivyoandika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif katika ukurasa waka wa Twitter: "Vikwazo vilivyo kinyume cha sheria vya Marekani vimetoa pigo kwa jitihada za Iran za kukabiliana na COVID-19."

Hivi sasa Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa, kwa kuzingatia hali maalumu iliyoko duniani, vikwazo dhidi ya Libya, Yemen na Syria vitapunguzwa. Hatua hiyo ya Umoja wa Ulaya ni sahihi lakini kwa kuzingatia kuongezeka watu wanaofariki dunia kutokana na vurusi vya corona na kutokana na wasi wasi uliopo kuhusu hali ya kiuchumi baada ya corona, nukta inayopaswa kusisitizwa sasa ni kuchukuliwa maamuzi ya kuhusisha pande kadhaa kimataifa na kuondolewa vikwazo sambamba na kuwepo ushirikiano na mshikamano wa kimataifa kama njia pekee ya kuikomboa dunia kutokana na janga hilo la corona.

4bv8a3102a627e1mnhd_800C450.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom