Umoja wa Ulaya waipa Ukraine msaada wa kijeshi wa Dola Milioni 508

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Umoja wa Ulaya (EU) umekubaliana kuipa Ukraine msaada zaidi wa kijeshi wa Dola Milioni 508 (Tsh Trilioni 1.17).

Rais wa Baraza la EU, Charles Michel amesema mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya wamekubaliana katika mkutano wao uliofanyika Brussels kujadili awamu nyingine ya vikwazo dhidi ya Urusi, ikiwemo marufuku ya dhahabu ya Urusi kuuzwa Ulaya.

Msaada huo unafanya kiasi kamili cha msaada wa kijeshi uliopelekwa Ukraine na Umoja wa Ulaya tangu kuanza kwavita Februari 24, 2022 kufikia Dola Bilioni 2.5.

Aidha, nchi wanachama wa EU pia zimeipa Ukraine msaada wa silaha kwa maelewano ya Nchi na Nchi.

Source: aa.com.tr

--------------------

EU foreign ministers agree on further $508M military aid for Ukraine

EU foreign ministers reached a political agreement Monday to send a further tranche of €500 million ($508 million) military aid for Ukraine.

Speaking at a news conference after their meeting, EU foreign policy chief Josep Borrell said that the EU top diplomats “unanimously agreed on the need to continue to stand firmly with Ukraine.”

Borrell said following his proposal the ministers reached a political agreement to provide another €500 million in military aid for Ukraine, bringing the bloc’s total contribution to €2.5 billion.

He confirmed that the ministers also discussed the European Commission’s latest proposal on banning Russian gold imports and amending the extension of sanctions, and said that EU ambassadors will negotiate the measures this week.

He also said Ukrainian Foreign Minister Dmytro Kuleba informed his EU counterparts about the “dramatic” situation on the ground as he joined the meeting via video link.

The EU is “terrified by Russian aggression against civilian people of Ukraine,” Borrell said, and there are “disturbing reports about the use of sexual violence as a weapon of war.”

The ministers also assessed regional issues, including the bloc’s relations with Latin America and Israel.

“The situation on the ground in Palestine territories is continuously deteriorating,” Borrell said, asserting that an upcoming EU-Israel Association Council meeting during the fall will be “a good opportunity” to rethink the Middle East peace process.

He, however, warned that EU countries have to first set up a common position on the matter.

The EU has slapped six sets of sanctions against Russia since it launched war on Ukraine on Feb. 24.

The packages target, among others, Russian President Vladimir Putin and Foreign Minister Sergey Lavrov, ban oil and coal imports, and the export of luxury goods, as well as exclude Russian and Belarusian banks from using the international money transfer system SWIFT.
 
Kwa hapa Tanzania team putin wanajua kabisa kwamba putin amekosea sana kuivamia Ukraine lakini wao wanafurahia putin kuivamia Ukraine kwa sababu hawawapendi wazungu lakini wanasahau kabisa hata putin nae ni mzungu.
 
Anachokifanya Russians ndio alichotaka kufanya USA Russians walivyotaka kuweka makombora yake Cuba lakini huo mgogoro ukaisha Kwa mazungumzo na moja ya mashart hakuna mmoja wapo kati ya USA na Russians kusogeza majeshi jirani na mwenzake Cha ajabu USA anataka kuweka base zake Kwa kuwatanguliza NATO.

Ajabu USA hataki ugomvi uishe Kwa mazungumzo anachochea tu mapigano wakati mgogoro wa Cuba alikaa chini na Russians ukaisha Russians wakaondoa missile zao.
 
Kwa hapa Tanzania team putin wanajua kabisa kwamba putin amekosea sana kuivamia Ukraine lakini wao wanafurahia putin kuivamia Ukraine kwa sababu hawawapendi wazungu lakini wanasahau kabisa hata putin nae ni mzungu.
Hatumpendi US na dada zake, acha kutulisha maneno wewe Nato
 
Wameongeza hela eeh , sawa tunahitaji iskander kreti moja tu ili kuiteketeza hio shehena itakayokuja kwa njia ya silaha 😂😂😂😂
 
Kwa hapa Tanzania team putin wanajua kabisa kwamba putin amekosea sana kuivamia Ukraine lakini wao wanafurahia putin kuivamia Ukraine kwa sababu hawawapendi wazungu lakini wanasahau kabisa hata putin nae ni mzungu.
hatuna shida na Wazungu, tuna tatizo na Marekani!
 
Kwa hapa Tanzania team putin wanajua kabisa kwamba putin amekosea sana kuivamia Ukraine lakini wao wanafurahia putin kuivamia Ukraine kwa sababu hawawapendi wazungu lakini wanasahau kabisa hata putin nae ni mzungu.
Hakuna mbwa au shoga anayeweza kupambana na mbabe Putin,
 
Kwa hapa Tanzania team putin wanajua kabisa kwamba putin amekosea sana kuivamia Ukraine lakini wao wanafurahia putin kuivamia Ukraine kwa sababu hawawapendi wazungu lakini wanasahau kabisa hata putin nae ni mzungu.
Tunacho angalia sisi ni circumstances zilizo isukuma Urusi kufanya kile watu wanacho kiita ni uvamizi - western nations hawataki ku-address valid concerns za Urusi kuhusu usalama wake as a NATION - lawama tu mwanzo mwisho, swali la kujiuliza hapa,ni: ni lini mataifa ya magharibi yatajifunza kuheshimu mataifa mengine equally bila ya kutumbukiza uzabazabina wa double standard - hapa kundi fulani linajifanya ku-shed crocodile tears wakiwalahumu warusi/Putin kuvamia Ukraine, lakini genge hilo hilo halisemi chochote kuhusu uvamizi wa NATO/US kwenye mataifa yafuatayo: Yugoslavia, Syria, Libya, Afghanistan, Iraq - katika uvamizi huo wanatumia mpaka depleted Uranium kuvunja madaraja na kulipua vifaru,lipua mashule,mahospitali,Ubalozi wa Uchina nk,wanatumia vile vile white phosphorus and cluster bomblets - yaani milipuko yote iliyo pigwa marufuku bado inatumiwa na NATO/US cha ajabu katika ukatiri wote huo sijawahi kusikia Dunia ikipendekeza kwamba Rais wa Merikani aburuzwe mahakamani the Hague kujibu war Crime,wako kimya kabisa,kazi kumkalia kooni Putin kwa kumtuhumu makosa ya jinai lukuki - huwezi kusikia wana wataja akina Bush Sr,Bush Jr,Clinton,Obama na Biden kuwa na wao ni wahusika wakuu kwenye kwenye masuala ya war crimes.

Sasa masuala kama haya ya baadhi ya Mataifa fulani kujiona ni bora zaidi Duniani kuliko mataifa mengine na wana haki za kuziwekea sheria nchi nyingine na kuzilazimisha zifuate sheria to the letter or else,slap punitive sanction wanapo jisikia - ujinga huu ndio umezifanya baadhi ya mataifa kusema enough is enough wakahamua kuanzisha a multipolar alliance (BRICS) ili waondokane na uwenda wazimu wa baadhi ya Mataifa ya magharibi - BRICS itafanikiwa sana kama washindani hawataifanyia hujuma - watu wote wapenda amani na ustawi wa mataifa yote tunaitakia kheri BRICS.
 
Back
Top Bottom