Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Umoja wa Ulaya unaandaa vikwazo dhidi ya maafisa wa Belarus ambao walihusika na ukandamizaji unaofanywa baada ya uchaguzi dhidi ya waandamanaji ambao umesababisha umwagikaji wa damu.
Idhini ya kutayarisha vikwazo ilitolewa na mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wakati wa mkutano wa video jana.
Watu watakaowekea vikwazo ni pamoja na waliohusika na vurugu za polisi na udanganyifu wa uchaguzi. Maelfu ya waandamanaji waliopinga uchaguzi huo wa wiki iliyopita katika nchi hiyo ya mashariki mwa Ulaya walikamatwa na kuzusha hasira kutoka jamii ya kimataifa.
Wakati wengi wao wameachiliwa huru, waandamanaji kadhaa walizungumzia mateso wakati wa kukamatwa na kuzuiliwa kwao. Jana jioni, maelfu ya watu kwa mara nyingine tena waliandamana kwa amani katika mji mkuu Minsk.