Umoja wa Ulaya kuimarisha utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam in kuvutiwa sekta binafsi kuwekeza nchi


FikraPevu

FikraPevu

Verified Member
Joined
Jan 2, 2010
Messages
303
Likes
122
Points
60
FikraPevu

FikraPevu

Verified Member
Joined Jan 2, 2010
303 122 60
Umoja wa Ulaya (EU) umesema ili kuimarisha utendaji na ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, serikali ya Tanzania inatakiwa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara yatakayovutia sekta binafsi kuwekeza nchini.

Wito huo unakuja wakati kumekuwa na malalamiko kutoka sekta binafsi juu ya mazingira yasiyo rafiki ya kufanya biashara ambayo yanakwamishwa na ongezeko la kodi katika sekta ya usafiri na ughavi.

Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa EU, Neven Mimica amesema kutekeleza mkakati wa serikali wa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafiri na ughavi katika Kanda ya Afrika Mashariki ni muhimu kuiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuwa yenye ushindani kwa kuboresha miundombinu na ufanisi.

“Mazingira wezeshi ya kufanya biashara ambayo yatavutia uwekezaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kuimarisha ushindani wa bandari”, amesema Kamishna Mimica.

TanzaniaP035530-PC3.jpg


Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU), Neven Mimica akiwa na Balozi wa Poland nchini Tanzania, Van de Geer wakati alipokutana na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, hivi karibuni kuelezea ushirikiano uliopo katika ya Tanzania na EU.

Kamishna huyo ambaye ametembelea Bandari ya Dar es salaam na kupokelewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Lazaro Twange ambapo alikwenda kukagua mradi mkubwa wa upanuzi wa bandari hiyo unaojulikana kama ‘Dar es Salaam Marine Gateway Project (DMDP)’ ambao unalenga kuifanya bandari hiyo kuwa na hadhi ya kimataifa na kuwezesha kupokea meli kubwa na kuhifadhi mizigo mingi.

Mradi huo wa DMGP umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) ambayo ni mshirika wa karibu wa EU ambapo Tanzania imepokea Dola za Kimarekani milioni 345 kukamilisha mradi huo ambapo utaongeza uwezo wa kupokea mizigo kwa tani milioni 25 miaka saba ijayo. Pia utapunguza muda wa kusubiri kutoka saa 80 hadi 30.

Hata hivyo, Kamishna Mimica amesema mradi huo utaongeza wigo wa kufanya biashara za kimataifa katika ukanda wa Afrika Mashariki, kuchochea uanzishwaji wa viwanda na kutengeneza ajira nyingi kwa kuwa wananchi wataanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, imedhamiria kukuza viwanda vya ndani na kuiwezesha nchi kuzalisha bidhaa mbalimbali zitakazoshindana na bishaa zingine katika soko la kimataifa. Ili viwanda vifanye kazi vinahitaji nishati ya uhakika ikiwemo umeme wa maji, upepo na gesi.

Ili kuinua viwanda, UE imetoa msaada wa bilioni 130 kwa ajili ya miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kamishna huyo amesema nishati ya umeme ni muhimu hususani katika maeneo ya vijijini kwa kuwa inachangia uboreshaji wa huduma za jamii kama shule, vituo vya afya, hospitali, viwanda vidogo vidogo na kilimo.

Ujio wa wawakilishi wa EU unakuja kabla ya Mkutano wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya kufanyika siku ya 28 na 29 Novemba, 2017 ambapo utazikutanisha pande mbili kujadili maeneo muhimu ya ushirikiano ikiwemo nguvu kazi ya vijana kwa maendeleo endelevu.

Zaidi, soma hapa => http://www.fikrapevu.com/umoja-wa-ulaya-kuimarisha-utendaji-wa-bandari-ya-dar-es-salaam/
 
AirTanzania

AirTanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2011
Messages
1,139
Likes
705
Points
280
Age
33
AirTanzania

AirTanzania

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2011
1,139 705 280
Mshamba kapewa nchi hatokubali ushauri mzuri, msifieni katika mambo ya kipumbavu ndio atakubaliana na nyinyi
 
N

ngondaenyamisati

Member
Joined
Oct 19, 2017
Messages
6
Likes
3
Points
5
N

ngondaenyamisati

Member
Joined Oct 19, 2017
6 3 5
Mimi naona kama vile siku moja Tanzania itakuwa nchi yenye maendeleo makubwa
 
AirTanzania

AirTanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2011
Messages
1,139
Likes
705
Points
280
Age
33
AirTanzania

AirTanzania

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2011
1,139 705 280
Mimi naona kama vile siku moja Tanzania itakuwa nchi yenye maendeleo makubwa
Labda kile chama cha wahuni kitoke madarakani ndio maendeleo yatapatikana. Kwa sasa msahau na genge hili la wahuni
 
S

santali

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Messages
209
Likes
124
Points
60
S

santali

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2017
209 124 60
Kwanini Ndugu zangu watanzanzia wanachangia mawazo wanachangia kwa kutokana wakati mwingi kwa kiongozi mkuu wa nchi? Kunatatizo gani hasa kwenye fikra zetu kama watanzania, tuchangie maoni yetu kwa hekima, uongozi ni kazi ngumu Sana,Kabla hujatukane jiulize ww mwenyewe mchango wako kwa familia yako na kwa jamii nn? inawezekana sehemu ya mchango wa Watanzania waliowengi ni matusi, nivema tujiulize faida ya kuandika matusi na kejeli .
 

Forum statistics

Threads 1,237,905
Members 475,774
Posts 29,305,724