Umoja wa Ulaya (EU) watoa msaada wa bilioni 84 kwa Tanzania kuisaidia kusambaza umeme Vijijini na kwenda Zambia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 30 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 84 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya Tanzania na Zambia.

Sehemu ya fedha hizo, kiasi cha Euro milioni 26 sawa na shilingi bilioni 72, Mkataba wake umeingiwa leo Jijini Dar es Salaam (15 Desemba, 2020) kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stephanie Mouen Essombe.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto james, alisema kuwa fedha hizo kiasi cha Euro milioni 26 kitatumika kujenga kituo cha kupooza umeme - Tunduma, kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kv 330 yenye urefu wa kilometa 4 kutoka Tunduma hadi mpakani mwa Tanzania na Zambia.

“Mradi huu pia unahusisha ujenzi wa njia mpya ya kusafirisha umeme katika maeneo ya vijijini, ambayo hayajafikiwa na Grid ya Taifa na kuongeza uwezo wa njia zilizopo za kusafirisha umeme kupitia Iringa – Kisada – Mbeya – Tunduma – Ushoroba wa Sumbawanga” alisema Bw. James

Alisema hatua hiyo itaongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea uzalishaji katika maeneo ya vijiji husika na pia kuongeza upatikanaji wa umeme katika maeneo yasiyofikiwa na yale ambayo umeme hautoshi hususan maeneo ya Kusini Magharibi mwa nchi yetu, ambayo yamekithiri umaskini.

Bw. James alisema kuwa msaada huo unaonesha kwamba Jamhuri ya Ufaransa na Umoja wa Ulaya ni marafiki wazuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinyume na dhana ya baadhi ya wapinzani wa nchi wanaodai kwamba uhusiano wa Tanzania na wadau wake wa maendeleo unadorora.

“Kupitia uhusiano wetu huu mzuri tunatambua kuwa kiwango cha uwekezaji cha AFD kwa Serikali ya Tanzania kimefikia takriban Euro milioni 454.5, sawa na shilingi trilioni 1.26 ambazo zinajumuisha mkataba uliosainiwa hivi karibuni wa mkopo wa masharti nafuu wa Euro milioni 100 kwa ajili ya mradi huu” Aliongeza Bw. James.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa Bi Stephanie Mouen Essombe alisema kuwa miezi michache iliyopita Shirika lake lilisaini mkataba wa mkopo nafuu wenye thamani ya Euro milioni 100 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo wa kusafirisha umeme wa Tanzania na Zambia.

“Leo tumekutana tena kwa ajili ya kusaini mkataba wa kiasi kingine cha nyongeza cha Euro milioni 26 sawa na shilingi bilioni 72 ambazo ni msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya kupitia Shirika letu” alisema Bi. Stephanie

Alisema Mradi wa kusafirisha umeme kati ya Tanzania na Zambia ni sehemu ya mwisho ya utekelezaji wa mradi wa ushoroba (corridor) kutoka Ethiopia, Kenya, Tanzania na Zambia unaolenga kupunguza gharama za matumizi ya nishati hiyo pamoja na kukuza uchumi wa nchi husika.

Alisema kuwa hivi karibuni, Shirika lake litatoa kiasi kingine cha Euro milioni 130 kwa ajili ya kutekeleza mradi mwingine mkubwa wa nishati jua (solar PV Power) wenye uwezo wa kuzalisha megawati 50, utakaojengwa mkoani Shinyanga.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier, alisema uhusiano wa Tanzania, Ufaransa na Umoja wa Ulaya uko imara na kwamba nchi hizo zitaendelea kuchangia maendeleo ya nchi kwa juhudi zote.

Alifafanua kuwa nchi yake kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) itaendelea kuwekeza katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ambapo katika kipindi cha miaka 10 Bodi ya wakurugenzi ya AFD imeidhinisha matumizi ya kiasi cha Euro milioni 430 kwa ajili ya sekta ya nishati.

Naye Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Mhe. Emilio Rossetti, alisema kuwa mbali na msaada wa kiasi hicho cha Euro milioni 26 zilizosainiwa, Umoja wake utatoa kiasi kingine cha msaada wa Euro milioni 4 kwa ajili ya kulijengea uwezo Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) na kufanya kiasi kilichotolewa na EU kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kufikia Euro milioni 30 sawa na shilingi bilioni 84.

Alisisitiza kuwa Umoja wa Ulaya unatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kwamba Umoja wa Ulaya utaendelea kuunga mkono juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
 
EU na WB zimetoa msaada kwa Tanzania kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo njia ya umeme wa KV 400 kwenda mpaka wa Tanzania na Zambia. Hili ni pigo kwa viongozi wa upinzani hasa Chadema wakiongozwa na TUNDU kwa upuuzi waliokuwa wakiufanya kuzurura kuisingizia nchi mambo mabaya ili tu kuona nchi inakwama kupiga hatua za kimaendeleo. Sasa wataaibika na ndio mwanzo wa mwisho wa siasa zao za matukio na kupiga madili.

Nakazia kwa video hii hapa chini

 
Hata wakitokea hiyo misaada, msimamo wetu uko pale pale. Haramu ni haramu tu.

Hakuna fedha ya msaada au mmkopo inayoweza kulingana na utu wa mwanadamu, hivyo misaada au mikopo haiwezi kutunyamazisha wala ku-justify uovu dhidi ya wanadamu.

Vile vile, wakiamua kutoa misaada na kwa vyama vya siasa, tusisikie mnawaita mabeberu huku fedha zao mnapokea.

Wazungu hawa wakisimama upande wa haki, tutwaunga mkono, na wakisimama upande wa dhuluma, tutawapinga.

Nitasimama upande wa haki hata kama shetani ndio atakuwa anatoa haki hiyo, na nitapinga dhuluma hata kama inatoka kwa au ina mkono wa malaika.

Mwisho, wazungu hawa angekuwa na roho za chuki na visasi kama wakoloni weusi, hiyo misaada na mikopo wasingeitoa kwa jinsi wanavyodhalilishwa kwa kuitwa mabeberu huku Kabudi akiwatolea maneno yasiyofaa.

Msisahau na za matundu ya choo kwa watoto wetu huko St. Kayumba.
 
Nachopenda ni kuona tunaomba wakati huohuo tunajipiga vifua kuwa tunatumia za ndani

Nachopenda ni kuona tunakopa wakati huohuo tunajigamba tunaweza kukopesha

Nachopenda ni kuona tunatangaza kupokea mikopo ya masherti nafuu lakini hatuyaweki hadharani masherti yenyewe ili wanyonge wayajue

Nachopenda ni kuona wananchi wanapandishiwa gharama za maisha kwa kigezo cha bei elekezi

Nachopenda ni kuona deni la taifa linapaa kama tiara huku tukijinasibu kuvunja rekodi ya makusanyo ya kodi

Nachopenda ni kuona CCM inaendelea kutuimbisha mbele kwa mbele na tunaimba sote
 
Wapinga maendeleo kwa sasa watakuwa wanapishana msalani mmoja anatoka mungine anaingia, maana lazima washikwe na tumbo la kuhara
Kitu kimoja tu tunapishana.

Kuamini kuwa chama pinzani ni kupinga maendeleo.

Lakini naamini, kati ya mambo elfu moja ya kisiasa uliyoyajua hadi sasa, zaidi ya nusu yake umeyajua kwa sababu ya vyama pinzani.
 
Yeeaaah kweli kabisa!! VIVA Magufuli
Wataajiriwa watu zaidi ya elf40 kuchimba mifereji, kutengeneza zege, kuuza chakula, kukunja nondo n.k
Then mradi ukikamilika wanarudi kitaa kuimba mbele kwa mbele

Nakupenda CCM
Piga keleleeeeeeeeeeeeeee
Wakati huo wamejipatia mtaji wa biashara ndogo ndogo na kilimo!
 
Back
Top Bottom