Umoja wa Ulaya (EU), waitikisa serikali mauaji ya Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umoja wa Ulaya (EU), waitikisa serikali mauaji ya Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 22, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  EU yalaani mauaji ya Mwangosi

  Umoja wa Ulaya (EU), jijini Dar es Salaam umelaani mauaji ya mwahabari Daudi Mwangosi, aliyedaiwa kuuawa na polisi na kuzitaka mamlaka zinazoshughulikia mauaji yake kuchunguza kifo hicho kwa uwazi mkubwa na kuwachukulia hatua stahiki watuhumiwa.

  EU ilisema imezifuatilia hatua za mwanzo za kisheria zilizochukuliwa kufuatia mauaji hayo ikiwemo kumfikisha kizimbani askari anayeshtakiwa kwa mauaji ya Mwangosi, lakini ikisisitiza juu ya kuwepo uwazi zaidi kwenye mamlaka zote zinazoshughulikia kifo chake.

  Mwangosi aliuawa Septemba 2, mwaka huu akiwa kazini kwenye tukio la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) la uzinduzi wa tawi la chama hicho kwenye mji mdogo wa Nyololo mkoani Iringa.

  Mshitakiwa wa mauaji hayo ni polisi Pacificus Simon (23) wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU), aliyefikishwa mahakamani Septemba 12, mwaka huu kujibu mashtaka ya kumuua kwa bomu la machozi mtumishi huyo wa zamani kituo cha televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa.

  Taarifa ya EU iliyotolewa jijini muda mfupi baada ya ujumbe wake ulioongozwa na Balozi Filberto Ceriani Sebrogondi kuzuru ofisi za vyombo vya habari vya IPP zinazohusisha The Guardian Limited, vituo vya televisheni vya ITV, East Africa , Capital , Radio One na East Africa Radio, kadhalika ilitoa salamu za pole kwa familia yake na tasnia ya habari nchini.

  EU ilisisitiza kuwa licha ya kwamba ni jukumu na haki ya serikali kuchukua hatua za kulinda amani na kudumisha utawala za sheria, ni jukumu la serikali pia kutekeleza majukumu hayo katika hali inayokubalika na kuzuia matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya raia huku ikilinda haki za wananchi.

  Taarifa hiyo ilikumbusha kuwa tasnia ya habari inatekeleza jukumu nyeti la kuwezesha uhuru wa haki ya kujua na kutoa maoni na kujieleza .

  “Kwa hiyo basi Umoja wa Ulaya, unaitaka Serikali ya Tanzania kufanya kila kinachowezekana kudumisha uhuru wa habari na hivyo kuhakikisha uwepo wa haki ya kutoa maoni,” ilisema taarifa hiyo.

  Mshitakiwa wa mauaji hayo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya mjini Iringa ambapo alisomewa mashtaka na kurudishwa rumande. Pamoja na kupandishwa kizimbani, pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, aliunda kamati ya kuchunguza mauaji hayo ikihusisha polisi, wanahabari na, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  Katika ziara hiyo, ujumbe huo wa EU, ukiwa kwenye vyombo vya habari vya IPP, ulieleza kufurahishwa na kazi zinazofanywa na vyombo hivyo vya habari.

  Balozi Sebrogondi, alivisifu vipindi vya televisheni na redio vinavyoelimisha jamii kuhusu mikakati ya kupunguza umaskini na uwezeshaji wa wananchi eneo ambalo umoja huo pia unalifanyia kazi ili kuziwezesha nchi maskini kuondokana na umaskini.

  Ujumbe huo ulikuwa wa viongozi na wafanyakazi wa umoja huo kutoka mataifa ya Kusini mwa Afrika Kusini mwa Sahara yakiwemo Ghana, Kenya, Zambia na Uganda.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  serikali yetu inauwa raia wake yenyewe!
  Ccm haiko tayari kung'ooka bila kuua!
   
 3. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu balozi atuambie wamechukua hatua gani maana watanzani tunampango wa kupata uhuru kwa damu ili mkoloni huyu Ccm atuache!Mimi nipo tayari kumwaga damu yangu au ya wanaccm,polisi na wote wanaokaa kimya katika dhuluma Ccm dhidi ya watu wake!Sitaunga mkono chama chochote ambacho hakiamini katika kumwaga damu ili kuiondoa Ccm madarani hivyo kuua polisi ni jambo la msingi sana!!!!!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa huwa hawafanyi mambo kwa papara. Wamekuwa wanaichora serikali kwa matukio mfululizo ya mauaji kupitia jeshi la polisi hadi kufikia hatua ya kuusambaza kwa bomu mwili wa Mwandishi wa habari kuwa kama udongo tifutifu.

  Jambo ambalo nalisoma kutoka nyuma ya pazia kutoka Umoja wa nchi za Ulaya, ni ukimya wa serikali hasa Mkuu wa nchi kutia pamba masikioni na kushona midomo kutotoa tamko lo lote huku ulimwengu ukishtushwa na tukio hilo lisilo la kawaida.
  Pia mizengwe ya tume ya kuchunguza mauaji ambayo imegubikwa kwa usiri mkubwa na kutokuwa tayari kuyakubali maoni ya wengi uundwaji wa tume ya haki itakayoongozwa na majaji wa mahakama ambayo huwa na uwazi zaidi.

  Rais Kikwete alishaulizwa mauaji ya awali mara baada ya uchaguzi na wanadiplomasia alipowaalika kwenye hafla ya mwaka Mpya Ikulu. Jibu la Kikwete kama kawaida lilikuwa zuri mno kwamba
  "nawahakikishieni kwamba mauaji haya ni mwisho, tutahakikisha jambo kama hili halitokei tena." Mwisho wa kumnukuru.

  Leo yanaendelea kwa kasi ya ajabu, je, nyuma ya pazia kuna kutokea shinikizo la bajeti wanayochangia kwa serikali kutokuwa makini kwa kusababisha mauaji hayo?

  Tunasubiri kama Kikwete atatoa pamba masikioni na kufungua mdomo wake kulitolea kauli, labda kwa kuogopa shinikizo la kuhofia kusitizwa hisani ya bajeti toka kwa watu hawa wa Ulaya.
   
 5. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jamani mti mkubwa unapoanguka, huvunjavunja miti midogo na vichaka, saa ya ukombozi imefika
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Serikali ilivyofanyia usanii na kuupuuzia msiba wa Mwangosi, sasa tunachosubiri ni kiherehere chake cha kuchangamkia misaada toka nje kwa nchi za Umoja wa Ulaya, hapa wamekabwa kooni, hakuna ujanja.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Balozi hawezi kukuambia mara moja hatua watakazochukua, wao wanatumia zaidi akili na uwajibikaji wa pamoja. Kikwete asipotumia akili ya ukweli na uwazi unaodaiwa na Umoja wa nchi za Ulaya kuhusu kifo cha Mwangosi wanaweza kusitisha ahadi za bajeti anayojivunia.
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tusubiri tuone maana upepo ukivuma sana madhara yake huonekana kila mahali
   
 9. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapa walio karibu na hawa viranja wa sirikali na sisiem wanaanza kukonyezana kope kwamba tumeshikwa pabaya. Misengwe ya wafadhili inaweza kuwaharibia mzimu wao.
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mwanzo » Maoni ya mhariri

  NA MHARIRI

  23rd September 2012

  [​IMG]
  Maoni ya Katuni


  Ubalozi wa Umoja wa Ulaya juzi ulitoa taarifa ya kueleza masikitiko na kuchukizwa kwake na kuuawa kwa mwandishi wa habari na mpiga picha wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daudi Mwangosi na ofisa wa jeshi la polisi mkoani Iringa hivi karibuni.


  Ni taarifa ambayo imepolekewa kwa mikono miwili siyo tu na asasi za habari nchini bali wapenda amani na demokrasia kote nchini, kuwa hiki si kilio cha wanahabari na wanaharakati peke yao, na siyo tu cha Watanzania bali kimewagusa wawakilishi wa mataifa tofauti duniani. Ni ujumbe ambao utakuwa umepokewa katika sehemu husika, kuwa mauaji kama hayo hayavumiliki katu.

  Kifo cha Daudi Mwangosi kimewagusa watu wengi kwa sababu suala zima la kueleza kuwa ni ajali iliyotokea katika kutuliza ghasia, ambayo polisi walielezea wakati wa kupigwa risasi kwa watu kadhaa huko nyuma, ikiwemo mjini Arusha mapema mwaka jana, halikuwepo.


  Ni mazingira ambako mtu asiye na silaha, ambaye polisi wanafahamika kumchukia kwa vile muda wote yupo wanapoanza kutumia nguvu bila sababu au zinazovumka mpaka, hivyo kufikisha udhibiti wa kupatikana na kutolewa habari katika janga la mauaji ya uso kwa uso. Ni doa ambalo itachukua muda kwa vyombo la dola kulisafisha.


  Kwa maana hiyo hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Ulaya, wa taarifa inayoeleza kinagaubaga kuwa vitendo vya aina hiyo havikubaliki, kama ambavyo mauaji mengine ya raia kwa mfano wafanyabiashara kutoka Morogoro waliokamatwa wanapigwa risasi na polisi hayakubaliki, ni ya kufurahisha.


  Naweka mazingira ambako iwapo kilio hiki kitaendelea, kama wenye madaraka hawana njia nyingine za kutoa hoja isipokuwa kutaka watoa habari waache kufanya kazi ili hali ionekane ni shwari, watakuwa na lawama zaidi. Watajikuta wanatengwa kwa kiasi fulani na jumuia ya kimataifa inayopenda demokrasia.


  Licha ya kuwa inafahamika kuwa siyo lazima kila ubalozi ufanyie kazi tukio la ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi ambazo wanawakilisha, ni jambo jema ikiwa wengine ambao siyo wa nchi za Umoja wa Ulaya wakiangalia kama kuna haja ya kutoa ujumbe kwa serikali na wanaharakati kuhusu hisia zao kwa suala hilo.


  Ni pale tu ambapo sauti za nje zinasikika ndipo watawala katika Afrika wanapata habari kuwa kuna tatizo, vinginevyo wanaendelea na tabia za kawaida, kwani suala zima la uwajibikaji ni sumu kwao, ndiyo maana wanafurahia mahusiano katika asasi mpya duniani. Hawataki zile za kimaadili.


  Viongozi wengi na hata wasomi katika Afrika wameonekana kuchangamkia kuvurugika kiasi fulani kwa nafasi ya nchi za Magharibi, yaani Ulaya na Amerika ya Kaskazini, katika uchumi wa dunia, na kuzidisha umuhimu wa nchi kubwa zenye viwanda kwa viwango vya kati kama Brazil, Russia, China, India na Afrika Kusini, sababu muhimu zaidi ikiwa ni kutotaka masharti ya kimaadili.


  Hivyo kutolewa taarifa kama hiyo ya Umoja wa Ulaya kuhusu mauaji ya Mwangosi kwa watawala wetu ni uingiliaji katika mambo ya ndani, kama alivyokuwa akieleza mara kwa mara akiwa madarakani, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. Aliainisha kanuni za msingi za diplomasia kihistoria kuwa ni kuheshimu na kushirikiana, kwa adabu, ulipotumwa.


  Kwa vile asasi za vyombo vya habari ni sehemu ya utamaduni wa jumla wa wasomi nchini, na karibu kila eneo utasikia mabaya na changamoto za utandawazi, lazima ifahamike kuwa itikadi hizi zina mapana na marefu yake, kuwa huwezi kutaka uhuru kamili wa vyombo vya habari huku unatetea kubana uhuru wa soko.


  Huwezi kutaka serikali kamili ya kidemokrasia huku unafurahia kuzuiliwa kwa makundi tofauti ya watu, wakiwemo Watanzania walioko nje ya nchi, kuwa na uraia wa nchi mbili, kuona hilo ni kuvuruga sura ya Utanzania. Ni vyema vyombo vya habari vikaanza kutafsiri uhuru wa habari na jamii katika eneo la itikadi, kwani kinachogomba na kufikia kuuawa kwa waandishi wa habari ni kuwa dola inakuwa katika mashaka kama shughuli zao zikiendelea, kwani huenda zikafikia mageuzi ya kisiasa, ambayo hayatakiwi.


  Hata hivyo juhudi za hayati Mwangosi na wengine ambao wamedhurika au kupoteza maisha wakiwa wanafanya tu kazi zao za kila siku ikiwa ni pamoja na kuonyesha matukio katika mikutano ya hadhara hazikuwa bure.


  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Rais Jakaya Kikwete alipuuza madai kuwa eneo hilo limeuzwa kwa matajiri wa Marekani, akawaasa wapinzani ‘kufanya zaidi wakitawala,' hisia ambayo katika saikolojia inaonyesha kuanza kukubali ukweli kuwa upinzani una uwezo wa kufika madarakani kama si leo, kesho.


  Alikuwa ni kiongozi wa mapinduzi ya Urusi mapema karne iliyopita, Vladimir Lenin aliyesema kuwa ‘mabepari wakiona aibu hiyo inaharakisha mageuzi.' Mambo haya ni ya msingi na yafaa yakaangaliwa kwa mapana jatika kujenga misingi bora na imara ya kidemokrasia.


  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  Sasa Watawala wa NCHI watasikiliza na kuheshimu UHURU wa VYAMA PINZANI ?
   
 12. N

  Njele JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Tutaendelea kunyamaza tu kwa vile bado tunafakari kupata jibu la kuwaambia hawa diplomatic kwamba tunarudia kauli tuliyowaambia mwaka jana kwamba kosa kama hili halitarudia tena, lakini kwa sasa limejirudia kwa vile nimekuwa na majukumu mengi ya kutalii nchi za nje, sasa nitajaribu kuwaambia wahusika wapime wenyewe juu ya tuhuma hizi. Kujipima wenyewe ndio falsafa ya mfumo wa uongozi wetu wa mtu binafsi kujiwajibisha mwenyewe ndio ufanisi wa uongozi wetu.

  Vinginevyo uwajibikaji wa pamoja hutupa kivuli kizito kumtazama mtu usoni kama ule msema ukitaka kumwua nyani usimtazame usoni, sisi hili latushinda kwa vile kwenye vikao tunakaa tumetazamani vigumu ukishamwangali mtu usoni halafu umwajibishe, bora ajipime mwenyewe na kufanya uamuzi.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwanza vyombo vya habari vinatia kichefuchefu pamoja na waandishi wake. Habari hii ambayo ina uzito mkubwa kutoka jopo la nchi zinazoifadhilia Tanzania bajeti imetiwa kapuni na vyombo vingi vya habari na wanahabari mbalimbali, ni IPP tu ndiyo iliyoweza kuiweka hadharani. Je, ni kutokana na zile bahasha za kaki zinafanya kazi yake waandishi wa habari wajipakae kiwi machoni? Wanahabari wanasusia kutoa habari hizi kwa hoja zipi?
   
 14. K

  Kompis Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Penye uzia tia rupia teh teh teh teh teh teh!! Napita tuu wajameni!""
   
 15. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,844
  Trophy Points: 280
  JK kabanwa kila kona ...lazima atoe tamko akiwa kama mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na mkuu wa nchi(watu). Sijajua kama katumia busara kukaa kimya kwani sometimes mtu mzima ukiona mambo si sawa ni bora kukaa kimya kuliko kutoa kauli yoyote...
  ila nikiangalia kwa upande wa pili inawezekama jamaa wameanza kuionesha serikali kuwa wapo na kukaa kwao kimya isifike wakati wakawadharau hasa kutokana na ishu ya ubalozi wa amerika na sakata la hivi majuzi kwani hawa jamaa lao huwa ni moja........
   
 16. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni sera za serikali ya CCM ya "Penye uzia penyeza rupia" na ile ya "Gawanya utawale." Sera hizi za wakoloni hawa (CCM) zimeudhoofisha umoja na mshikamano wa wanahabari kwani baadhi yao wamehongwa nyadhifa serikalini ili 'kuwaziba midomo' wasiendelee kuwabughudhi manyang'au hawa CCM. Kikwete na CCM yake wako very smart katika kudeal na makundi yanayojitokeza kuwaumbua, na silaha kuu anayoitumiani hii katiba mbovumbovu, iliyochoka na iliyozeka ya chama kimoja - CCM inayompa madaraka ya kuhonga vyeo kwamanufaa yake na chama chake.

   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tuwaambie nchi za Ummoja wa Ulaya wafunge account za pesa zilizofinchwa huko hadi wahusika watakapojieleza kwa bunge la Tanzania wamezipataje.
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  hawa hata wakifanya kazi na muovu ni kwa kwa sababu ya convinience tuu na si vinginevyo.wanajua CCM si chama na serikali ni kimeo ila kwa vile nchi ni strategic na hapakuwa na chama mbadala kipindi cha nyuma.Na pia wananchi wakionekana kuridhika na hiyo hali basi huwa wanapata shida wasemea.Sasa utaona jinsi mamabo yataanza badilika fasta against serikali.Kama jamaa wa madini wanajitoa ni wazi kuwa wanataka idhoofisha CCM mpaka mwisho.
   
Loading...