Umoja wa Ulaya (EU) kuipatia Serikali ya Tanzania Tshs bilioni 307.9

Wakati huohuo serikali inadaiwa 1.4 + trillion na wastaafu wa Tazara.
 
Kwa hiyo EU siyo MABEBERU tena.

Au fedha hizo tutazipata bila MASHARTI yoyote.
Hawa ni marafiki zetu, wadau wa maendeleo wakitupa pesa, ngoja sasa waseme sijui democracy sijui covid, hapo tunawaita mabeberu waliotuibia sana sisi nchi tajiri ni sovereign e.t.c! :D😆😅tunawageuka 360°.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Ni jambo la heri EU wanatusaidia kwenye masuala mengi. Nadhani ni bora zaidi kuutambua mchango wao kuliko kuwaita mabeberu.
 
Masikini Hawezi Kukopeshwa!
Sisi Tunakopeshwa Sababu Ni Matajiri
Tanzania Ni Tajiri Sana
😅😄😃😂😁😀🤣😂😁😄😃🤣😉😏🙄😶
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Dah muwe mnaangalia taarifa ya habari bas mara picha,picha imetumwa mnataka mkataba tena
Anataka kuzimia huyo maana aba roho mbaya sana. Na hapo ndipo inadhihirisha hali halisi ya watanzania, wamejaa wivu kwenye maendeleo mbaya zaidi hata maendeleo yanayohusu taifa lake.
 
Hawa wazungu wanatuchezea akili kwelikweli.

Kwa hivi vihela vyao $132 million wanaona ndiyo thamani ya waTanzania takriban 55 million?

Tanzania hii haina uwezo wa kulima mazao na kupata 132 million na zaidi kwa mwaka, ili ikidhi mahitaji yake badala ya kuuza thamani ya utu wao?

Halafu angalia tuhela huto tunavyosambazwa, kiasi kwamba hata kitakachofanyika hakionekani. Si bora wangesema hela hiyo ongezea kwenye ujenzi wa SGR au Stieglers ili ujenzi uende na kumalizika haraka?

Maeneo yenyewe wanayosema yatasaidia kuboresha maisha ya waTanzania na kufikia uchumi wa viwanda-
  • sekta ya uchumi
  • uboreshaji wa sera mbalimbali
  • miundombinu ya barabara
  • viwanja vya ndege
  • nishati
  • kilimo
  • mazingira
  • miradi ya sekta ya nishati
  • miradi ya matumizi endelevu ya nishati ya kupikia
  • mradi wa kusaidia mnyororo wa thamani katika ufugaji wa nyuki
  • kuboresha mazingira ya biashara na ushirikiano kitaalaamu
  • maendeleo katika sekta binafsi na ajira
  • muingiliano wa uchumi na biashara
  • mabadiliko ya hali ya hewa

Hivi vihela $132 million vitasambazwa kote huko, na kuwalipa 'consultants' wao watakaokuja hapa; halafu Tanzania ipate kuboresha maisha ya wananchi wake na kufikia uchumi wa viwanda?

Hawa watu wanatuona hatuna akili kabisa
Kama wanataka kutupa msaada kweli, wafungue masoko yao tuwauzie mazao yetu.
 
Kwa hiyo EU siyo MABEBERU tena.

Au fedha hizo tutazipata bila MASHARTI yoyote.
Hawa wazungu wana akili sana. Mnatiliana saini, kisha hela inatoka kwa awamu. Ili itoke ni lazima utimize masharti.

Hela ya New Millenium Challenges ilitiwa saini dola milioni 800. Ikatoka awamu ya kwanza na ýa pili. Awamu iliyofuatia, dikteta alipoharibu, ikasimamishwa, baadaye ikafutwa moja kwa moja mpaka leo.

Ni sawa na ule mkopo wa bank ya Dunia, uliidhinishwa lakini kutoka ni kwa awamu, baada ya kupima kama mmetekeleza masharti. La sivyo, mnabakia na makaratasi tu!!
 
Thibitisha, inawezekana EU hawana tatizo na Watanzania bali viongozi walioingia madarakani kifisadi
Angalia hiyo pesa maeneo inakopelekwa - hali ya hewa, sera, mazingira ya uwekezaji. Na masharti kibao. Wasipotekeleza, hakuna hela, wanabakia na makaratasi.

Mikataba huwa inatiwa saini mingi lakini pesa kutolewa mpaka utekeleze masharti ya msaada.
 
Back
Top Bottom