Umoja Wa Mataifa Wathibitisha Matatizo Ya Binaadamu Afrika Mashariki

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
ocha_medium.jpg

Shirika la misaada ya kibinaadamu la Umoja wa Mataifa imetoa taarifa likisema watu wapatao milioni 11.4 wamekimbia makazi yao katika nchi 12 za Mashariki mwa Afrika.


Ripoti hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa mataifa inayoratibu Mambo ya Kibinaadamu katika Afrika Mashariki, OCHA, imesema wakimbizi wameongezeka kwa asilimia 14 hadi watu milioni 1.4 ndani ya miezi sita iliyopita.


Ripoti imesema wimbi kubwa la wakimbizi limeripotiwa nchini Ethiopia, Kenya, Sudan na Uganda, wengi wao wakitokana na mgogoro wa Sudan Kusini.


Kenya ina wakimbizi wanaokadiriwa kufikia laki 6 na serikali pamoja na UNHCR wamekuwa wakiwawezesha wakazi wa maeneo ya mijini kwa wakimbizi wanaohitaji ulinzi maalumu ukiwemo usalama, elimu, matibabu na wale wanaoandikishwa kwa ajili ya makazi mapya katika nchi hizo.

Chanzo:Timesfm
 
Back
Top Bottom