comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Umoja wa Mataifa kupitia nchi kadhaa umeomba mzozo wa Nchi za Marekani na Korea Kaskazini utatuliwe kwa mazungumzo sio kijeshi,Waziri Mkuu wa Japan bwana Shinzo Abe amesema suluhisho la mazungumzo linawezekana kuliko nguvu za kijeshi amesema hayo leo baada ya Korea kaskazini kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Korea kaskazini bwana Sin Hong- Chol kuonyesha Korea Kaskazini ipo tayari kuingia vitani bwana Chol amesema "zama za kutetemekea vikwazo, amri na vizungumkuti vya Marekani zimeisha na anaamini wafanyabiashara pia wakati wao umeisha" ameongeza kwa kusema wazi kwamba hawaogopi vitisho hivyo majeshi ya Korea kaskazini yapo katika umakini na maandalizi ya hali ya juu sana kwa lolote lile, amesema hayo hasa baada ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kufanya ziara katika rasi yenye ulinzi mkali wa kijeshi mpakani mwa Korea Kusini na Korea Kaskazini, vilevile bwana Sin Hong- Chol amesema wataendelea kufanya majaribio ya makombora yao ya nyuklia kila wiki, kila mwezi na kila mwaka kwa kuwa Korea kaskazini haiamuliwi mambo yake ya ndani na nchi yoyote kwani hawauzi kwa dola za Marekani nyuklia yao. Aidha Korea kaskazini imetishia kutumia makombora ya nyuklia kupiga ndani ya Marekani endapo Marekani itajaribu kufyatua risasi nchini Korea.
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema jaribio lolote la kuivamia Korea kaskazini litagusa maslahi yake hivyo vilevile Wang amesema " naona Marekani wapo tayari bila kusita kutatua mgogoro huu kwa njia ya Kidiplomasia" ameomba suluhisho liwe la diplomasia ya kisiasa na sio nguvu za kijeshi, nae Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema " machaguo yote yapo mezani"
Aljazeera.