MWEZI MMOJA BILA MWAMBA;BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA LAMUENZI HAYATI DAKTARI JOHN POMBE MAGUFULI.

Leo 10:40hrs 18/04/2021

Ni heshima kubwa sana kiitifaki katika Baraza kuu la Umoja wa mataifa kumuenzi Rais wa nchi aliyefanya mambo makubwa kwa nchi yake lakini akatutoka akiwa Madarakani,kikao cha kumuenzi Hayati Rais John Pombe Magufuli kiliandaliwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikiudhuriwa na Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Viongozi wa kikanda wa Umoja wa Mataifa,ni heshima kubwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupewa heshima hiyo kubwa na Umoja wa Mataifa.

Heshima ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli imetolewa mwezi mmoja tangu kufariki kwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 17/03/2021,Umoja wa Mataifa ilishusha bendera nusu mlingoti wakati wa maziko ya Hayati Daktari John Pombe Magufuli na Jana tarehe 17/04/2021 imeendelea kumuenzi Daktari John Pombe Magufuli kwa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kukutana na kuenzi maisha ya Hayati Daktari John Pombe Magufuli hapa duniani na mambo mema aliyoyafanya Daktari John Pombe Magufuli kwa dunia,bara la Afrika akiwa Mwenyekiti wa SADC na kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utumishi wake kwa nchi ya Tanzania.

Umoja wa Mataifa umeutangazia Ulimwengu kuwa hapakuwahi kuwepo Rais katika Afrika tangu kuondoka kwa uzao wa akina Kwame Nkrumah,Nelson Mandela na Julius Nyerere mwenye kariba,maono,uhodari na Uzalendo kwa nchi yake kama Hayati Rais John Pombe Magufuli,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitaja moja ya Jambo la kukumbukwa alilofanya Hayati Rais John Pombe Magufuli ni kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati miaka 4 kabla ya muda uliotarajiwa yaani 2025,pia alisema katika awamu ya Rais John Pombe Magufuli mchango wa kulinda amani la jeshi la Wananchi wa Tanzania uliongezeka mara dufu katika Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika salamu zake kumkumbuka Rais John Pombe Magufuli alisema wanatambua utumishi uliotukuka wa Rais John Pombe Magufuli,alisema Hayati Rais Magufuli alipambana kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana na kukabiliana na vitendo vya rushwa ambavyo vilikuwa vimeshindikana,Katibu Mkuu huyo alisema Rais John Magufuli alipata umashuhuri kwa maendeleo ya miundo mbinu ambayo ni zana muhimu katika maendeleo ya kiuchumi kufikia uchumi wa juu, Tanzania ilifika azma yake ya kuwa nchi ya kipato cha kati miaka minne kabla ya lengo lake la 2025,

Thamani ya miundo mbinu tunayoiona,thamani ya miradi mikubwa tunayoiona Bwawa la Umeme,Ununuzi wa ndege,ufufuaji wa atcl na ttcl,Ujenzi wa barabara nane,Ujenzi wa Daraja la Tanzanite na Daraja la Busisi,Ujenzi wa meli kubwa tisa,pato la taifa la trillioni 1.8 kwa mwezi alilokuwa akikusanya Rais John Magufuli,thamani ya huduma za jamii alizozianzisha Ujenzi wa Zahanati 400 nchi nzima,Ujenzi wa masoko mapya katika mikoa yote 30,Ujenzi wa vituo vipya vya mabasi katika mikoa yote ya Tanzania,ukijumlisha thamani ya hayo yote ukagawanya na idadi ya Watanzania Milioni 60 utapata kipato cha dola 2300 ambacho kimetuingiza Watanzania katika uchumi wa kati.

Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Hayayi Rais Daktari John Pombe Magufuli wa Tanzania ilitekeleza miradi mikubwa ya kimkakati iliyobuni ajira kwa Watanzania wengi kama mradi wa SGR kutoka Dar hadi Morogoro na kutoka Morogoro hadi Dodoma na tayari mradi mpya umeanza kutoka Tabora hadi Mwanza,mradi mwingine ulioajiri Watanzania wengi ni mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere ambalo likikamilika litatoa fursa ya kilimo cha umwagiliaji cha mpunga kitachozalisha zaidi ya tani laki mbili na kuuza duniani kote,ni kati ya vitu ambavyo viliivutia Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kama taifa lenye kipato cha kati,

Mbali na uongozi thabiti wa Rais John Pombe Magufuli katika kudhibiti matumizi ya fedha ya umma pamoja na kupambana na wale wanaotaka kufuja fedha ya umma, taifa la Tanzania limeimarika kiviwanda, Serikali ya CCM ya awamu ya tano imefanikiwa kuanzisha zaidi ya viwanda elfu nane katika kipindi cha miaka mitano,Benki ya Dunia, WB, tarehe 1 Julai 2020 ikaiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati, Shukrani kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli na hivi leo tunamuenzi kwa mema yake aliyoyafanya enzi za uhai wake hapa duniani.

Luka 19:40

Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.

Nami nasema Huyu mwamba Daktari John Pombe Magufuli amefanya yaliyoshindikana,Ushindi wa ccm kuanzia serikali za mitaa vijiji na vitongoji,udiwani kata zote bara na visiwani,ubunge,hii alama ni ngumu kufutika,ninukuu ilani ya CCM 2020-2025.

"Ni ukweli usio na shaka kuwa, ili CCM iendelee kukubalika na kuaminiwa na wananchi na kupewa ridhaa ya kuongoza nchi yetu, upo muhimu mkubwa kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, kuwa karibu na wananchi kwa kuwatembelea, kusikiliza kero zao na kushirikiana nao katika kuzipatia majawabu. Ni muhimu pia kwa CCM wakati wote kuwa kimbilio, msemaji na mtetezi wa wananchi wote na hasa wanyonge. Hii ni muhimu kwa kuwa, kwa asili yake, CCM ni Chama cha wakulima na wafanyakazi kinachowatetea wale ambao sauti zao sio rahisi kusikika."
ILANI YA CCM YA MWAKA 2020: 2025


Ndugu zangu ukwel ni mmoja tu ili CCM iendeleee kuaminiwa na pengine kuongeza Wanachama njia ni moja tu Serikali Kuu kutekeleza ilani ya CCM kama ilivyoandikwa na kunadiwa Tanzania nzima na Hayati Daktari John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan na utekelezaji wa miradi yote ambayo imeanzishwa na Hayati Rais John Magufuli ikiwa sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa Watanzania,miradi hiyo isimamiwe kwa bidii na iishe vinginevyo 2025 tutapigwa usoni na Watanzania kwa kutumia Ilani yetu tunayoishika mkononi bila kuitekeleza.

Alale pema peponi Rais John Pombe Magufuli,Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki Rais wetu mpya,Mama Samia Suluhu Hassan.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Jpm alikuwa mtanzania halisi na mpiganaji nchi amewaachia wairudishe enzi za mwinyi
 
Back
Top Bottom