Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuwasaidia wakimbizi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,111
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jenerali Antonio Guterres jana ameyataka mataifa kuongeza jitihada zao za kuwalinda wakimbizi katika maeneo tofauti ya ulimwengu, katika kipindi hiki ambacho idadi ya wanaokimbia mataifa yao kwa sababu ya kujinusuru kiusalama imeongezeka.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la siku mbili kuhusu wakimbizi alisema katika wakati huu ambao hali imekuwa mbaya zaidi jumuiya ya kimatiafa lazima ifanye jitihada zaidi kubeba jukumu hilo pamoja.

Kongamano hilo litarajiwa kuainisha mipango kutoka kwa serikali zinazoshiriki, makampuni na asasi ili kuweza kuongeza mikakati ya kuwasaidia wakimbizi. Kamishna wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi Filippo Grandi alisema lazima kuwepo kwa nyenzo ambayo itaweza kufanya kazi kuwasaidia wakimbizi duniani kote na hasa mataifa masikini na yale yanayoendelea.
1576677618939.png
 
Back
Top Bottom