Umoja wa Mataifa umesema janga la Corona limegeuka kuwa mzozo wa haki za binadamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la virusi vya corona ni mzozo wa kibinadamu ambao unageuka kwa kasi kuwa mzozo wa haki za binadamu.
Coronavirus - UN-Generalsekretär Guterres (Imago/L. Rampelotto)

Katibu Mkuu huyo amesema katika ujumbe alioutoa kwa njia ya vidio leo, kwamba kuna ubaguzi katika utoaji wa huduma za umma kukabiliana na ugonjwa wa covid-19, na kuzungumzia pia ukosefu wa usawa wa kimuundo ambao unazuwia upatikanaji wa huduma hizo.

Guterres amesema janga la corona limesababisha pia athari zisizolingana kwa baadhi ya jamii, kuongezeka kwa matamshi ya chuki, kulengwa kwa makundi ya walio hatarini, na kusababisha hatari ya matumizi ya nguvu iliyopitiliza kwa upande wa idara za usalama, hali inayoodhofisha hatua za kiafya.
 
Iko wazi kabisa namna matibabu na njia za kuukabili zimekiuka kwa namna flani haki za binadamu.

Mfano mdogo tu wa Lockdown kama njia ya kuukabili, haki ya kufanya kazi, kujipatia kipato, kujikimu, kutoka sehemu moja hadi nyingine zimekiukwa.
 
corona limesababisha pia athari zisizolingana kwa baadhi ya jamii, kuongezeka kwa matamshi ya chuki, kulengwa kwa makundi ya walio hatarini, na kusababisha hatari ya matumizi ya nguvu iliyopitiliza kwa upande wa idara za usalama, hali inayoodhofisha hatua za kiafya.
Bila shaka tumeona wazi, watu weupe baadhi yao wakiashiria hayo dhidi ya watu weusi! Lakn hatujashangaa kwa sababu ni kawaida yao, wengine wameshasemaga africa ni Tundu la uchafu!!
 
Back
Top Bottom