Umoja wa Mataifa: Tunahofia sheria mpya ya uraia India, inabagua

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa ofisi hiyo Jeremy Laurence amesema “sheria hiyo iliyorekebishwa inataka kuongeza kasi ya mchakto wa uraia kwa makundi ya kidini ya awaliowachahe ikiwataja hususan Wahindu tu, Singasinga, Wabudha, Wajamatini, Waparsis na Wakristo ambao wakikimbia mateso huko Afghanistan, Bangladesh na Pakistan, ambao wamekuwa wakaazi kabla ya 2014. Lakini haitoi ulinzi huo huo kwa Waislamu, pamoja na madhehebu ya vikundi vingine vichache.”

Ameongeza kuwa sheria hiyo iliyorekebishwa itaonekana kudhoofisha ahadi ya kuhakikisha usawa iliyowekwa hapo kabla katika katiba ya India na majukumu ya India chini ya mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa na mkataba wa kutokomeza ubaguzi wa rangi, ambao India ni nchi mwanachama, mkataba ambao unakataza ubaguzi unaotegemea misingi ya rangi, kabila au dini.

Ijapokuwa sheria pana za uraia India zinabaki palepale, marekebisho haya yatakuwa na athari ya kibaguzi kwa wsku kuweza kupata fursa za utaifa.

Ofisi hiyo imesisitiza kuwa wahamiaji wote, bila kujali hali yao ya uhamiaji, wanastahili heshima, kulindwa na kutimiziwa haki zao za kibinadamu. Miezi 12 tu iliyopita India iliidhinisha mkataba wa kimataifa kuhusu Uhamiaji Salama, wa mpangilio na wa kawaida ambao ambao unayafanya mataifa kushughulikia mahitaji ya wahamiaji walio katika hali ya hatari, kuepuka kuwashikilia kizuizini na kufukuzwa, na kuhakikisha kuwa hatua zote za utawala wa uhamiaji zinazingatia misingi ya haki za binadamu. .

Wakati lengo la kulinda vikundi vilivyoteswa linakaribishwa, hii inapaswa kufanywa kupitia mfumo wa kitaifa wa uombaji hifadhi ambao umewekwa kwa misingi ya usawa na sio ubaguzi, na ambao unatumika kwa watu wote wanaohitaji kulindwa kutokana na mateso na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu, bila ubaguzi wa rangi, dini, asili ya kitaifa au sababu zingine zilizopigwa marufuku.

“Tunatambua kwamba sheria hii mpya itatahiminiwa na mahakama kuu ya India na tunatumai kwamba itafikiria kwa makini muingiliano wa sheria hiyo mpya na wajibi wa kimataifa wa India katika utekelezaji wa haki za binadamu.” ameongeza msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu.

Wakati huohuo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa wasiwasi na taarifa kwamba watu wawili wamekufa na wengine wengi wakiwemo polisi kujeruhiwa katika majimbo ya India ya Assam na Trippura wakati wa maandamano ya watu kupinga sheria hiyo.

“Tunatoa wito kwa mamlaka kuheshimu haki ya watu kukusanyika kwa amani na kuzingatoa sheria, kanuni na viwango vya kimataifa katika matumizi ya nguvu wanapokabiliana na waandamanaji. Na pande zote zinapaswa kujizuia na machafuko.”

Pia soma India: Bunge lapitisha muswada unaowatenga Waislamu kupata uraia wa nchi hiyo
 
Ase Ndio maana kina mo dewj walikimbia India maana kule waislamu wanabaguliwa sana na wahindu
 
Wahindi walio wengi waliokuwa waislamu walidai Nchi huru ya Pakistan

Pakistan na India zilikuwa Nchi moja kabla ya hapo

Baada ya kugawanywa kwa Nchi waislamu wengi walikuwa upande wa Pakistan

Waliobaki India wakawa wanabaguliwa na wahindu mpaka leo
... waislamu wa India waende Pakistan na Bangladesh ndio kwao. India ni ya wahindu na dini zingine ndogo ndogo.
 
... wenye nchi yao (90%) ndio wameamua hivyo Mkuu. Vinginevyo wabadili dini wawe wahindu kama ambavyo mhindu hatakiwi kuabudu akiwa Saudi Arabia labda asilimu kwanza.
Saudi Arabia haina raia wahindu. 100% Waislam. Kumbuka hilo.
 
... wenye nchi yao (90%) ndio wameamua hivyo Mkuu. Vinginevyo wabadili dini wawe wahindu kama ambavyo mhindu hatakiwi kuabudu akiwa Saudi Arabia labda asilimu kwanza.
Saudi Arabia mbona umeenda mbali hivyo, mhindu hatakiwi hata Pakistan, ambao ni ndugu mmoja na India..wanachofanya India kinafanywa na Pakistan muda mrefu sana, sema wahindu wao wameamua kulifanya kisheria na kiutaratibu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahindi walio wengi waliokuwa waislamu walidai Nchi huru ya Pakistan

Pakistan na India zilikuwa Nchi moja kabla ya hapo

Baada ya kugawanywa kwa Nchi waislamu wengi walikuwa upande wa Pakistan

Waliobaki India wakawa wanabaguliwa na wahindu mpaka leo
Kwnn wabaki,cc km wahindu wa kwa mtogole tunawatungia sheria kbsa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom