Umoja wa Mataifa: Komesheni vitendo vya ukatili na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake

mdau wetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
548
Points
0

mdau wetu

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
548 0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka nchi mbalimbali duniani kuchukua hatua za kukomesha ukandamizaji dhidi ya wanawake. Akizungumza kwa mnasaba wa kuwadia siku ya kimataifa ya kukomeshwa ukandamizaji dhidi ya wanawake, Ban Ki moon amezitaka nchi mbalimbali kutekeleza ahadi zao za kukomesha ukandamizaji dhidi ya wanawake chini ya sheria za kimataifa. Amesema kuwa, kuongezwa shughuli za kisiasa za serikali mbalimbali ni moja ya malengo ya kukomeshwa ukandamizaji huo dhidi ya wanawake. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 17 Disemba 1999, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa kauli moja kwamba ifikapo tarehe 25 Novemba ya kila mwaka, kutaadhimishwa kama siku ya kimataifa ya kukomesha ukandamizaji dhidi ya wanawake.


Sosi: Radio Tehran, Iran
 

Forum statistics

Threads 1,392,805
Members 528,696
Posts 34,118,388
Top