UMOJA wa Kiislamu (Istiqama) wamtaka Mufti aache kushambulia vyama vya upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UMOJA wa Kiislamu (Istiqama) wamtaka Mufti aache kushambulia vyama vya upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Apr 14, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  UMOJA wa Kiislamu (Istiqama) Mkoa wa Dares Salaam, umemtaka Sheikh Mkuu nchini, Mufti Shaaban bin Simba, kuacha kuvishambulia vyama vya siasa vinavyoikosoa serikali na badala yake ashughulikie masuala yanayohusu maslahi na matakwa ya Waislamu hasa katika kipindi hiki cha vuguvugu la madai ya Katiba mpya.

  Msimamo huo ulitolewa jana na Sheikh Yasin Bahama, kwa niaba ya umoja huo wa mringano wa Kiislamu, wakati akitoa tamko kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na nafasi ya Waislamu katika mchakato huo.

  Tamko hilo limekuja ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu Mufti Simba ayalaumu maandamano yaliyofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mikoa ya Kanda ya Ziwa akisema yanahatarisha amani ya nchi.

  Ajenda ya maandamano hayo ilikuwa ni kuishinikiza serikali kuchukua hatua za dharura za kulinusuru taifa liondokane na maisha magumu hasa baada ya kupanda kwa bei za vyakula, bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo umeme, gesi na mafuta.

  Sheikh Bahama alisema mufti kama kiongozi wa waislamu wote nchini anapaswa ahakikishe kuwa katiba ijayo inawapa Waislamu fursa na haki za kutosha ikiwa ni pamoja na kuwa na Mahakama ya Kadhi.

  "Haya maisha magumu tunayapata wote sasa wanapotokea watu wanaishinikiza serikali ili hali iwe nafuu halafu anatokea mtu anawapinga (Mufti), kwa kweli ni jambo la kushangaza," alisema.

  Sisi kama Waislamu hatuoni tatizo lolote linalofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kuwa ni chama cha siasa cha upinzani, na lengo la vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali kwa kuwa ni haki yao kisheria.

  Tunawasihi Waislamu wote kwa pamoja tuhakikishe Katiba mpya inakuwa na Mahakama ya Kadhi. ….tushughulike na kudai haki zetu ziingie kwenye Katiba. Tuachane na kutetea CCM na serikali yake, tuachane na kushambulia vyama vya siasa kwani vipo kwa mujibu wa sheria", alisema Sheikh Bahama.

  Walisisitiza kuwa suala la kuwa na Katiba mpya ni muhimu kuliko kuangalia ni chama gani kinaongoza nchi kwa wakati huu, kwani chama kinachoongoza sasa kitafika mwisho wake lakini kama Katiba itakuwa mbovu basi haki na maslahi ya Mwislamu vitaendelea kudhulumiwa siku zote.

  Alisema kuwa Waislamu wana madai mengi na ya msingi wanayopaswa kuhakikisha wanatimiziwa kuliko kuangalia kwanini serikali ya CCM inasemwa.

  Waliwataka viongozi wote wa kidini nchini kuachana na masuala ya kisiasa na badala yake wawaongoze watu wao katika kufanya mema kwa ajili ya mwenyezi Mungu.
   
 2. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wadau hili mnalionaje, kuna ukweli wowote? Kama ni kweli basi angalau hawa wamefunguka wanaweza kutusaidia katika harakati za kuukataa udini katika siasa za tanzania (Source Tanzania Daima)

  Waislamu wampinga Mufti kuibeba CCM


  na Abdallah Khamis, Dodoma  UMOJA wa Kiislamu (Istiqama) Mkoa wa Dares Salaam, umemtaka Sheikh Mkuu nchini, Mufti Shaaban bin Simba, kuacha kuvishambulia vyama vya siasa vinavyoikosoa serikali na badala yake ashughulikie masuala yanayohusu maslahi na matakwa ya Waislamu hasa katika kipindi hiki cha vuguvugu la madai ya Katiba mpya.

  Msimamo huo ulitolewa jana na Sheikh Yasin Bahama, kwa niaba ya umoja huo wa mringano wa Kiislamu, wakati akitoa tamko kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na nafasi ya Waislamu katika mchakato huo.

  Tamko hilo limekuja ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu Mufti Simba ayalaumu maandamano yaliyofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mikoa ya Kanda ya Ziwa akisema yanahatarisha amani ya nchi.

  Ajenda ya maandamano hayo ilikuwa ni kuishinikiza serikali kuchukua hatua za dharura za kulinusuru taifa liondokane na maisha magumu hasa baada ya kupanda kwa bei za vyakula, bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo umeme, gesi na mafuta.

  Sheikh Bahama alisema mufti kama kiongozi wa waislamu wote nchini anapaswa ahakikishe kuwa katiba ijayo inawapa Waislamu fursa na haki za kutosha ikiwa ni pamoja na kuwa na Mahakama ya Kadhi.

  “Haya maisha magumu tunayapata wote sasa wanapotokea watu wanaishinikiza serikali ili hali iwe nafuu halafu anatokea mtu anawapinga (Mufti), kwa kweli ni jambo la kushangaza,” alisema.

  Sisi kama Waislamu hatuoni tatizo lolote linalofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kuwa ni chama cha siasa cha upinzani, na lengo la vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali kwa kuwa ni haki yao kisheria.

  Tunawasihi Waislamu wote kwa pamoja tuhakikishe Katiba mpya inakuwa na Mahakama ya Kadhi. ….tushughulike na kudai haki zetu ziingie kwenye Katiba. Tuachane na kutetea CCM na serikali yake, tuachane na kushambulia vyama vya siasa kwani vipo kwa mujibu wa sheria”, alisema Sheikh Bahama.

  Walisisitiza kuwa suala la kuwa na Katiba mpya ni muhimu kuliko kuangalia ni chama gani kinaongoza nchi kwa wakati huu, kwani chama kinachoongoza sasa kitafika mwisho wake lakini kama Katiba itakuwa mbovu basi haki na maslahi ya Mwislamu vitaendelea kudhulumiwa siku zote.

  Alisema kuwa Waislamu wana madai mengi na ya msingi wanayopaswa kuhakikisha wanatimiziwa kuliko kuangalia kwanini serikali ya CCM inasemwa.

  Waliwataka viongozi wote wa kidini nchini kuachana na masuala ya kisiasa na badala yake wawaongoze watu wao katika kufanya mema kwa ajili ya mwenyezi Mungu.
   
 3. J

  Joblube JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawa ndio waislamu wa kweli bana
   
 4. G

  Gurti JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umoja wa Kiislamu (Istiqama) Mkoa wa Dsm umemtaka Shekh mkuu kuacha kuviashambulia vyama vya siasa vinavyokosoa serikali, badala yake apiganie maslahi na matakwa ya waislamu hasa ktik kipindi hiki cha madai ya katiba mpya.

  Tamko hilo lilitolewa kwa niaba ya taasisi hiyo na Sheikh Yasin Bahama.

  Tamko hili limekuja siku chache tu baada ya Muft kupinga maandamano ya Chadema kwa madai ya kuhatarisha amani.

  Sisi kama waislamu, hatuoni tatizo linalofanywa na CHADEMA kwa kuandamana kwa amani. Wanashinikiza serikali iboreshe maisha ya Watanzania wote wakiwapo waislamu.

  Nimeleta habari kwa ufupi. Soma mwenywe kwa urefu.

  Source; Tanzania Daima ya leo. uk page 1 and 2.
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Kumbe wanajua maana yake.......:A S-key:
   
 6. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Big up wasomi wa Kiislam!
   
 7. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Bora huyo kasema kweli, hao ndio waislam wa kweli
   
 8. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hongera Sheikh Bahama, mimi siyo mwisilamu lakini nina marafiki zangu wengi ambao tunamadai yanayo fanana na tumeendelea kuwa wamoja katika masuala mengi.

  Suala la dini mara nyingi siyo suala la kuchagua, ni suala linalotegemea umezaliwa na kukulia wapi na kumchukia mtu kutokana na dini yake ni dhambi kubwa kwa Mungu. Mtu yeyote anayegombanisha watu kwa sababu za dini zao huyo mtu ni hatari na ni wa kuogopwa kama Ukimwi (Mufti Simba ni mtu wa kuogopwa!)
   
 9. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kwani toka mwanzo si lilikuwa genge la wana ccm waliojificha kwenye dini hao kina mufti simba, waislamu hawaungi mkono ccm si tuko nao makazini, majumbani na kwingineko na ndio maana mambo ya udini anayo kikwete na mufti wake simba. Waislamu huwa hawana mchezo na upumbafu si umeona zanzibar ambako wako wengi sana wamechana na kuchoma muswada wa katiba na kuona ni kinyesi kingine kimeletwa.
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu hii ngoma haikeshi kwa kuwa haikutokana na mawazo ya waislam wa chini ilipandikizwa.
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Sijaona source lakini kama ni kweli basi ni mwanzo mzuri!
   
 12. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  jeykey gamba lake la udini limevuka!!!
   
 13. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mimi muislam na nakubaliana na sheikh bahama 100%
  kul hakat lau kana murua{sema kweli ijapo kuwa chungu}
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
 15. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa nini mashehe watulazimishe sie waislamu tufikiri kama wao. Mbona wanatunyima uhuru wa kufikiri. Koruani inatushauri tufuate haki na tutetee haki na tuunge mkono sehemu inayodhulumiwa haki. Unafiki ndio utatupeleka jehenamu
  masalaam
   
 16. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nimeipenda sana hii. Kama Waislamu wataendelea namna hii tutapata katiba yenye tija kwa ajili ya watoto wetu na wajukuu zetu. Ile siku ya kulaumiwa na wajukuu wetu tutakuwa tumeiepuka.
  Mungu ibariki Tanzania.
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Professor ameanza kazi rasmi na bado watabaki waislam maslahi na mufti wao
   
 18. wasaimon

  wasaimon R I P

  #18
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ndio hiyo. Nimeipenda hii kwani CDM wanapopigania bei za vitu zishuke hawafanyi hivyo kwa wanachama wao pekee bali ni kwa ajili ya wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao au dini zao. Hongera UMOJA WA KIISLAM kwa kulitolea tamko hilo.
  Na wengine pia muige mfano huo sio kukaa kimya.


   
 19. k

  kibokogiziba Member

  #19
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi ntasema kweli daima kama nyie ni waislamu mambo yenu yamalizwe msikitini sio kushabikia vitu mnavyoletewa kwenye jf "nini kasema SAW pale weislamu au mashekh wanapopishana hoja ?" mnaletewa hoja chafu za kuwagawa waislmu wenzenu ili mseme fulani anafaa na fulani hafai mnaanza kwenye jf kuleta misemo na hadith zisizofaa, tumalize mambo yetu msikitini, kwani hilo gazeti la kiislamu? hata kama ni kweli kasema yabidi aambiwe mwenzie kakosea basi kuna njia ya kumkosoa. sasa mnajenga tabaka za ushabiki tu ktk jf. ni lini uliona wasiokua waislamu wameleta mabishano au makosa ya viongozi wao hapa jf ? tieni akili mtume SAW watu wamekojoa msikitini kakaa kimya anasubiri watu waondoke ili amfundishe akiwa peke yake "vp sisi tutumie majukwaa kwa kumsifu huyu na kumponda huyu" kumbukeni kauli ya tauhiiid mnayoshea. ALLAH atuongoze wote mimi na wewe na nimetumia njia hii sababu tu siwezi kukufikia ulipo na sipajui lakini tumfuate mtume kama alivyotufunza ili tumtii mola wetu.
   
 20. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #20
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mi nilishasema kuwa wapo waisalmu wengi sana wenye busara kama tunavyoona huku mtaani tunakofanya nao kazi. Lakini makamba alikuwa anatafuta genge la wahuni fulani na kuwanunua, kisha wanachafua haiba ya waisalmu. Pongezi sana kwa msimamo wenu...
   
Loading...