Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
MWENYEKITI wa Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat, ametoa wito wa uchaguzi wa amani, wenye kujumuisha kila mmoja na wa haki nchini Tanzania.
Ametoa wito kwa washikadau wengine, Vyama vya Kisiasa na wafuasi wake kushiriki uchaguzi kwa amani na kujizuia kufanya vitendo vyovyote vya ghasia.
Ameendelea kuisihi serikali kuhakikisha mazingira mazuri yanayowezesha raia kupiga kura zao kwa njia salama na ya amani.
Pia amekumbuka safari ya kupigiwa mfano ya Tanzania katika utekelezaji wa demokrasia na amani na kutoa wito uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020, kuwa fursa mpya ya kuimarisha demokrasia na amani nchini humo.
AU umepeleka wataalamu wa uchaguzi nchini Tanzania kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 3, 2020 unaoongozwa na Goodluck Jonathan, aliyekuwa rais wa Nigeria.