baba anjela
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 430
- 310
Kuna tatizo kubwa Afrika, Yaani hata kwa kuunganisha Nguvu zetu kwa pamoja kuja na chanjo moja imeshindikana, tunabaki kuwapa pongezi kubwa wazungu kwa kutuletea chanjo.
maisha ya mwafrika yapo mikononi mwa mzungu. Sasa tuna Uhuru gani? Uhuru wa kupandisha bendera na kushusha basi. Uhuru wa kuchagua raisi basi.
Jambo kubwa linalo tutafuna afrika ni disunity.( kukosekana kwa umoja). Jambo ambalo wazungu wanalitumia kama mlango wakuendelea kututafuna. Bado mataifa yetu ni machanga,kusimama kila taifa peke yake ni ngumu kusonga mbele.
Tuna kila sababu ya kupata umoja wa Afrika wenye maono ya kulikomboa bara la Afrika. Na si huu umoja uliobebwa na kivuli cha mzungu. Tutaendelea kuwapigia magoti wazungu mpaka lini?
Linapokuja jambo la afya ,usalama ,uchumi.. Afrika lazima tuwapigie magoti wazungu, sasa Uhuru wetu ni UPI??... Vita na magonjwa havitokuja kwisha africa,ili wazungu waendelee kutafuna Mali zetu. Leo mama Africa anagombaniwa na kila mwanaume. Hana uwezo wakujisimamia.
Baba Africa uko wapi?