Umoja wa Afrika, SADC, EAC na UN mpeni Rais Magufuli tuzo ya heshima

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Kiongozi anayefanikiwa kuwaondolea hofu watu wake, kuwaongoza katika kipindi kigumu na kuwavusha salama ndilo hitaji LA Dunia kwa sasa.

Kiongozi anayepanga mikakati, kuisimamia na kufanya maamuzi magumu yenye manufaa kwa nchi take, Huyo ndiye kiongozi bora.

Pamoja na hatua madhubuti alizozichukua JPM ili kuyanusuru maisha ya watanzania dhidi ya Covid-19 pamoja na kulinda uchumi wa familiya na Taifa kwa ujumla, Viongozi wengi duniani wameshindwa kabisa.

Mheshimiwa JPM alijitoa mhanga na kuyaweka rehani maisha yake kwa maslahi ya watanzania wote.
Kitendo cha kujitolea kwa kumteua msaidizi wake wa Kiafya ili awe katibu Mkuu Wizara ya afya ni uzalendo, utu na upendo wa kiwango cha juu.

Profesa Mabula sasa anawahudumia watanzania wote ili kuzinusuru afya za watanzania wote badala ya afya ya Rais pekee.

Kwa upendo, utu na uongozi wa aina hii, Mheshimiwa JPM anastahili Tuzo ya Heshima na kuwa mfano kwa viongozi wengine kutanguliza maslahi ya umma. EAC, SADC, AU na UN, mtendeeni haki JPM kwa kumpa tuzo
 
Sijui unafikiri nini, labda tuzo ya kutotoa taarifa, watu wa nje na baadhi mashirika wanamtaka atoe takwimu, nae hatoi halafu apewe tuzo ni ndoto!
 
Daaah......this is too much!
Unalazimisha upewe tuzo na hizo orgs kwa kutumia vigezo vyenu.
Anzisheni zenu, mjipe kwa vigezo vyenu!
Mbona rahisi!

Everyday is Saturday......................... :cool:
 
Back
Top Bottom