Umoja wa Afrika Mashariki umejifunza nini kwenye matatizo yaliyopo umoja wa ulaya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umoja wa Afrika Mashariki umejifunza nini kwenye matatizo yaliyopo umoja wa ulaya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWANA WA UFALME, Dec 7, 2011.

 1. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona umoja wa afrika mashariki unaelekea kufuata mfumo ule wa umoja wa ulaya lakini swala la kujiuliza ni nini tumejifunza kutuka umoja wa ulaya?

  Sasa jamaa wanafikiria kuachana, na ni vizuri kuelewa kwanini wamefikia hapo,

  mwenzako akianza kunyolewa, wewe tia zako maji.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umoja wa nchi za Ulaya ilikuwa ni nguvu ya soda tu hapo awali hasa kuhusu uchumi. Nchi maskini kule ulaya zilikuwa na ndoto za kupaa kiuchumi kutokana na kunufaika na nchi tajiri hasa kutokana na kuwa na sarafu moja yenye kuwa na mzunguko nchi zote za Ulaya. Awali sarafu yake ilikuwa na nguvu sana.

  Matatizo yanaielemea umoja wa Ulaya hasa mzigo wa nchi ambazo pesa yake haikuwa na nguvu kabla ya kujiunga na baadhi ya nchi ambazo hazikuwa na uchumi mzuri .

  Nchi za Ugiriki na Itali ni moja ya mataifa yamekuwa kanyaga boya kwa umoja wa Ulaya. Kama mnakumbuka pesa ya Italia wakati huo ilikuwa ukiwa na shilingi moja ya Tanzania unapta kapu la pesa za Italia.

  Uingereza ilishaona hili ndio maana walisita kujiunga, pesa yao ingali na nguvu ile ile. Lakini Euro inazidi kuporomoka kila kukicha na ndoto za sarafu yake kuongoza soko la dunia limebaki jambo la kufikirika tu.

  Sarafu ya Marekani inaendelea kuimarika, papo hapo kuiporomoja Euro kwa kasi na muda si mrefu inaweza kulingana na kisha kuiteremshwa kabisa.

  Jambo hili ni muhimu tukajifunza hapa Afrika Mashariki, kuna mambo mazui ya kuungana kiuchumi, lakini kuna baadhi inabidi kuwa makini vinginevyo licha ya kuvuruga uchumi wa nchi kadhaa linaweza kuwa donda ndugu lenye kuhatarisha kisiasa kama ilivyotokea kuvunjia kwa umoja huo miongo kadhaa iliyopita.
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Kenya itatuletea zigo la madeni na matatizo pindi tukianzisha sarafu moja,mi hilo la sarafu sikubaliani nalo hata kidogo,nafikiri kila mtu sasa ni shahidi a yale yanyoikumba EU na Euro yao,wanachi wengi wa nchi kama Ufaransa,Ubelgiji ,Ujerumani wanataka nchi zao zirudi kutumia sarafu yao,jamani Waingereza hawakuwa wajinga walivyoikataa Euro ,kwanza sarafu ni utambulisho wa kitaifa.Haya mambo ya EAC ni ya wanasiasa na vibepari uchwarwa lakini sioni kama itamsaidia mtanzania wa kawaida,na muda si mrefu patakuwa hapatoshi hapa
   
 4. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Candid scope nimekubaliana na wewe kabisa katika uchambuzi huu
   
 5. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sure nafikiri tunaweza kuzoa matatizo zaidi kuliko faida. i.e costs outweigh benefits
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakuna lililo zuri ktk kurudisha EAC hasa nchi zetu zikiwa zote maskini.. Tunachotaka kufanya ni kuweka sinia la pilau mezani tugombanie badala ya kila mmoja wetu kutumia sahani yake... Jambo pekee ambalo tunaweza kulifanya na la maana ni kuwa na Free trade zone baina ya nchi zetu yaani mtu anakwenda nchi nyingine kufanya biashara kisheria kuondoa hii habari ya Ulanguzi wanaopitisha mali maporini inatuangusha kila miaka ku hike bei za bidhaa...Kwa hiyo kila nchi itafaidika na uzalishaji wake kuuza mali inapohitajika lakini haya ya kuunda chama cha maskini sidhani kama ni idea nzuri!
   
 7. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Kama bado tuna akili kichwani, tutajifunza kwa yanayotokea katika umoja wa ulaya. Maana huku kwetu wanasiasa wa kenya, uganda na rwanda wameweka tamaa mbele, ya kupata masoko, ardhi na maliasili kwa chee, bila kuangalia athari za kuharakisha mambo.

  ...Tofauti za kiuchumi, kijamii na kisiasa tulizonazo ni kubwa kuanza kufikiria masuala ya shirikisho kwasasa, yanayopigiwa debe na uganda. Eneo hili litakuwa kama kichwa cha kichaa, tukiingia kwenye hilo jambo kichwa kichwa.

  ...Ukweli ni kwamba, kwasasa tunatakiwa kuishia kwenye umoja wa soko, halafu tutaona huko mbele itakuwaje. Haraka haraka, haina baraka!
   
 8. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sure mkandara, hata sasa swala linalogonga vichwa wenzetu wa EU ni huu mchanganyiko wa waliochoka na wazima. sasa kwa mfano uingereza imeamua kufuata maslahi yake na kuachana na mambo ya kwenda kimuungano. Hapa kwetu hata swala la amani kwa hizi nchi zinazotuzunguka lina utata bado achilia mbali utofauti wa kiuchumi
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hivi kwanini tusikae na hayo ambayo tumeungano nayo sasa kwa miaka 50 tuone kama kuna faida ndio tuongeze jambo lingine ..

  nini haraka ..
   
 10. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sure Da si Lamu, hata nchi nyingi zilizokuwa na nguvu ndogo kiuchumi mwanzoni zilikimbilia EU kwa speculation ya kufaidi kiuchumi lakini kwasasa nchi hizi zimepoteza sovereign na zinaonekana ni mzigo ambao unahitaji kutuliwa kwa haraka sana hasa kwa hizi nchi kubwa kwenye umoja wao kama ujerumani na ufaransa
   
 11. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haha, tropical nakubaliana na hoja yako, sometimes tunajaribu kutafuta nguvu ya muungano kama suluhisho la matatizo yetu pasipo kujua tunaweza kutengeneza matatizo, na hapo ndipo umakini unapohitajika zaidi
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu mkandara kuna mengi mazuri ya kuirudisha jumuiya ya Afrika Mashariki. Tatizo ni kuwa hakuna watu hasa kwa upande wa Tanzania wanaoweza kuisadia nchi inufaike na jumuiya hiyo, kuna udhaifu mkubwa kwenye serikali yetu. Lakini ukiangalia upande wa Kenya siku zote wanapush kuelekea EAC kwa kuwa wanajua watanufaika sana. Kila shilingi ina pande mbili, kwa hyo ni namna tu ya kucheza karata. Ukianga FTA-CUSTOM UNION-MONETARY UNION....etc ni kuhusu uchumi, ndio maana wengine wanafanya hivyo.
   
Loading...