barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Umoja wa Afrika umekubaliana "kuandaa mpango" ambao utafanikisha kujiondoa kutoka katika mahakama ya kimataifa ya ICC. Hayo yamezungumzwa kwenye mkutano wa siku mbili mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mwenyekiti mpya wa AU, rais wa Chad, Idris Deby amesema ICC inawalenga viongozi wa Afrika. Amesema AU inasubiri ICC kutahmnini wasiwasi uliooneshwa na umoja huo. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambaye aliwasilisha pendekezo hilo amesema yeye pamoja na naibu wake William Ruto wamekuwa wakikabiliwa na "kesi zenye msingi dhaifu wa uchunguzi na zenye kuchochewa kisiasa" kutoka kwa ICC. ICC imesema inasaka haki na usawa kwa waafrika walioathiriwa na mizozo.
Chanzo:#SalimKikeke BBC Swahili-London
Chanzo:#SalimKikeke BBC Swahili-London