Umoja wa Afrika(AU) watenga bajeti ya matumizi ya Kiswahili

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
6,198
6,218
Umoja wa Nchi za Afrika umepitisha rasmi Lugha ya Kiswahili kuwa Lugha ya kazi kwa shughuli zote za umoja huo sambamba na hilo pia imetenga Bajeti maalumu kuhakikisha lugha ya kiswahili inatumika kikamilifu kwa shughuli zote za umoja huo.
pia ripoti mbalimbali zimeanza kuchapishwa kwa lugha ya kiswahili.

Hakika Lugha ya Kiswahili inazidi kushamiri na kupewa umuhimu mkubwa duniani.

Kama AU, SADC n.k zimedhamiria kutumia lugha ya kiswahili kwenye shughuli zake za kila siku, nashangaa sana kuona baadhi ya vyombo vyetu vya kutoa haki kwa wananchi bado vinajivuta ktk matumizi ya lugha ya kiswahili.

Chanzo:
Chanel ten Habari.
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
8,277
15,052
Ni habari njema sana. Lakini hofu tu ni kwamba lafudhi na misamiati ya nchi jirani ndiyo inaenda kutawala. Watanzania tumekuwa zaidi ya wavivu na wazembe!
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
6,198
6,218
Ni habari njema sana. Lakini hofu tu ni kwamba lafudhi na misamiati ya nchi jirani ndiyo inaenda kutawala. Watanzania tumekuwa zaidi ya wavivu na wazembe!
mbele ya safari tutaanza kulaumu.....ohhhh kiswahili ni chetu....ohhh kilimanjaro ipo kwetu....!!!

Tatizo kama ulivyo sema ni uvivu wa kushindwa kuchangamkia fursa.

Wajanja watakuja kukihodhi halafau tutabakia kulaumu.

Bado kuna taasisi za Serikali zinasuasua na kubeza matumizi ya kiswahili!!! nashangaaa sanaa!!

Kama taasisi za kimataifa zinakitumia kiswahili vipi kuhusu taasisi/mamlaka za ndani zinasuasua au kubeza?!!
 
MAKA Jr

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
216
144
Umoja wa Nchi za Afrika umepitisha rasmi Lugha ya Kiswahili kuwa Lugha ya kazi kwa shughuli zote za umoja huo sambamba na hilo pia imetenga Bajeti maalumu kuhakikisha lugha ya kiswahili inatumika kikamilifu kwa shughuli zote za umoja huo.
pia ripoti mbalimbali zimeanza kuchapishwa kwa lugha ya kiswahili.

Hakika Lugha ya Kiswahili inazidi kushamiri na kupewa umuhimu mkubwa duniani.

Kama AU, SADC n.k zimedhamiria kutumia lugha ya kiswahili kwenye shughuli zake za kila siku, nashangaa sana kuona baadhi ya vyombo vyetu vya kutoa haki kwa wananchi bado vinajivuta ktk matumizi ya lugha ya kiswahili.

Chanzo:
Chanel ten Habari.
Haya ndio mambo sasa.
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom