Umoja wa Afrika ( AU) wampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo ndoto za mwalimu Nyerere za kuiunganisha Afrika

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,716
141,579
Kamishna wa AU mh Bade kwa niaba ya Umoja wa Afrika amempongeza kwa dhati Rais wa Tanzania Dr Magufuli kwa kuzitekeleza kwa vitendo ndoto za mwalimu Nyerere za kuiunganisha bara la Afrika.

Bade ametoa pongezi hizo jijini Arusha wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la makao makuu ya mashirika ya Posta Afrika ( PAPU)

Jengo hilo litamilikiwa kwa ubia kati ya PAPU na serikali ya Tanzania ambapo PAPU itamiliki 60% na GoT kupitia TCRA 40%

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa barani Afrika na Tanzania tumeongozwa na Waziri wa ujenzi na mawasiliano mh Kamwele.

Chanzo: ITV habari!
 
Sijui Sera yanu ni IPI,kila kitu kupinga tu,kuna siku mtapinga kuwa ninyi si wakiume,mchawi mpe sufa zake,viva jpm
Kweli kaiunganisha Afrika kwa kuchoma vifaranga kutoka Kenya na kumzuia raia wa Misri hasiwe mtendaji mkuu wa vodacom Tanzania.
Habari nzima imejaa vitu vinavyoashiria fake news (likiwemo jina la waziri). Unaunganishaje nchi za Afrika kwa kuchoma vifaranga toka nchi jirani yako (ukiwa ni mfano mmoja tu)?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini Mwalimu Nyerere alipinga hoja ya akina Kwame Krumah & Co. ya United States of Afrika, hivyo sielewi alitaka kuiunganisha Afrika ipi?
 
Kama huku anakofanya Rais Magufuli....... Mnakuwa na ubia kwenye vitega uchumi!
 
Kamishna wa AU mh Bade kwa niaba ya Umoja wa Afrika amempongeza kwa dhati Rais wa Tanzania Dr Magufuli kwa kuzitekeleza kwa vitendo ndoto za mwalimu Nyerere za kuiunganisha bara la Afrika.

Bade ametoa pongezi hizo jijini Arusha wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la makao makuu ya mashirika ya Posta Afrika ( PAPU)

Jengo hilo litamilikiwa kwa ubia kati ya PAPU na serikali ya Tanzania ambapo PAPU itamiliki 60% na GoT kupitia TCRA 40%

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa barani Afrika na Tanzania tumeongozwa na Waziri wa ujenzi na mawasiliano mh Kamwele.

Chanzo: ITV habari!

Ahaaaa ahaaaa mzee Mgaya, hivi bado kuna viongozi wanaongea ndoto za Nyerere karne hii!? Hawajui ilibidi atoke madarakani huku wananchi wakiwa wanavaa viraka, na kunywa chai ya sukari ilikuwa anasa? Angewaunganisha hao waafrika si angeishia kuambukiza umasikini wetu na ukondoo kwa kichaka cha amani?
 
Sijui Sera yanu ni IPI,kila kitu kupinga tu,kuna siku mtapinga kuwa ninyi si wakiume,mchawi mpe sufa zake,viva jpm

Sent using Jamii Forums mobile app

We dogo bendera fuata upepo bana, umesikia neno watu kupinga kila kitu, na ww umelibeba kichwakichwa, sasa hivi kila mada watu wakija na mitazamo tofauti, unakimbilia kutumia neno la fashion kuwa kuna kupinga kila kitu! Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
 
Ahaaaa ahaaaa mzee Mgaya, hivi bado kuna viongozi wanaongea ndoto za Nyerere karne hii!? Hawajui ilibidi atoke madarakani huku wananchi wakiwa wanavaa viraka, na kunywa chai ya sukari ilikuwa anasa? Angewaunganisha hao waafrika si angeishia kuambukiza umasikini wetu na ukondoo kwa kichaka cha amani?
Bwashee 1985 ulikuwa hunywi chai wewe?

Mwaka huo mchungaji Msigwa alikuwa akituuzia mitumba mikali pale Miyomboni Iringa mjini.....maisha yalikuwa mazuri bwashee!
 
Kunywa chai yenye sukari ilikuwa anasa achia mbali viraka vilivyokuwa vimetuandama. Nakumbuka nilipokuwa mtoto chai ilikuwa inapikwa siku kuna wageni, ila uji wa chumvi ndio ilikuwa habari ya mjini. 1984 siwezi kusahau mtoto wa jirani yetu aliniazima suruali niendee kanisani, niliishia kuifunga na kamba ikawa imeweka celebration japo haikushonwa na celebration!
 
Mwaka huo hali ilikuwa nzuri tofauti na 1980 baada ya ile vita ya kumtoa Nduli Amini!
 
Back
Top Bottom