Umoja wa Afrika (AU) ulishakitambua Kiswahili. Kati ya AU na SADC ipi kubwa na yenye ushawishi zaidi?

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Kuna kipindi hapo nyuma ambacho AU ilikitambua rasmi Kiswahili kama lugha rasmi inayotambuliwa na inayoweza kutumiwa katika mikutano yote ya AU.

Nakumbuka hata aliyekuwa Mwenyekiti wa AU na aliyewahi kuwa Rais wa Msumbiji, Joaquim Chissano aliwahi kutoa hotuba nzima kwa lugha ya Kiswahili.

Swali la kujiuliza toka wakati huo tumechukua hatua gani kufaidika na hii lugha? Je badala ya hizi mbwembwe za sasa hivi za SADC, kwa nini tusingeendeleza pale tulipoishia au kukwama ukizingatia nchi zote za SADC pia tayari ni wanachama wa AU?

Sijui BAKITA wanakwama wapi? Siasa imekuwa nyingi lakini nadhani hawapewi ushirikiano na serikali.

Kwa nini Kiswahili hakipo kwenye Rosetta Stone?

Kwa nini Kiswahili siyo moja ya lugha kwenye electronic devices na software mbalimbali?

Kwa nini Hollywood wanatumia Wakenya badala ya Watanzania pale Kiswahili kinapohitajika?

Kwa nini wasanii wetu wasifundishwe kutumia Kiswahili fasaha kwenye nyimbo zao badala ya kuchanganya lugha?

Makaburu walijaribu kulazimisha lugha yao Afrikaans katika mitaala ya elimu ikaleta mgogoro mkubwa Afrika Kusini. Tukisambaze Kiswahili kwa kutumia mipango yenye akili.
 
Back
Top Bottom