Umoja ni nguvu: Wapinzani nchi hii bila kuungana wasahau kushika Dola

Vyama vya siasa vina itikadi, malengo na sera tofauti. Kazi yao ni kuwashawishi wananchi juu ya ubora wa mielekeo yao hiyo tofauti katika kuchochea maendeleo na ustawi wa taifa.

Hakuna mantiki kwa vyama hivyo kuungana eti kwa lengo moja tu - kuiondoa CCM madarakani. Vikishaungana vitaeneza itikadi ipi? Malengo gani? Na sera zipi? Vitawaaminisha wananchi vinasimamia nini hasa? Kama kweli CCM ndio chama bora kinachokubalika na Watanzania wengi, tatizo liko wapi?

Tatizo la kubwa la Tanzania sio “mabadiliko ya chama tawala tu”. BALI ni CCM kuwa chama dola kilichohodhi madaraka kidikteta na kuhujumu mfumo mzima wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Kwa kutumia vyombo na taasisi za dola, CCM imejihakikishia kukaa madarakani kwa nguvu bila ridhaa ya wananchi.

Kutoliona hilo ni kielelezo cha uongo na unafiki.

Lengo la chama.chochote Cha siasa ni kushika Dola,kwan ww hulitambui hilo??

Sasa kama Nia yao wapinzan ni kushika dola, watawezaje kushika dola ikiwa wamegawanyika??
 
Sasa mkuu, utawezaje kuiondoa CCM bila kuunganisha nguvu zenu?

Huo ndo ukweli, ndiyo maana wenzenu kama kina Mashinji, Wilbroad Slaa hawa wote walikuwa makatibu wakuu wa chama wamewakimbia kwenda CCM.

Mmoja kala UDC mwingine ni balozi, wanaganga njaa zao.

Wengine kama Nasari, Waitara, Msando, Lijualikali, Covid 19 wamechagua njia hiyo hiyo kuganja njaa, kwani hamuoni huu ukweli?

Hamna macho? Hamfikiriii? Je, hamna akiliiii?

Muambiwe vip Ili muelewe
Ndio ujue ni kwa nini Mbowe ni mwenyekiti mpaka leo, nae angekuwa na akili za kununulika angekuwa ni waziri kwa sasa. Kuna watu Nyerere aliwahi kusema wana bei, yaani wananunulika, ni kama hao uliowataja.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Mtumie akili,mnataka umaut umfike hapo hapo akiwa mwenyekiti kama maalim seif??

Uhai wa chama lazima uendane na succession plan
 
Mtumie akili,mnataka umaut umfike hapo hapo akiwa mwenyekiti kama maalim seif??

Uhai wa chama lazima uendane na succession plan
Naogopa kukuambia na wewe utumie akili, kwa sababu naweza kuwa nakuambia utumie kitu ambacho huna. Hoja ya viongozi kutoka na wengine kuingia siyo mpya kikubwa wapatikane watu sahihi.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Naogopa kukuambia na wewe utumie akili, kwa sababu naweza kuwa nakuambia utumie kitu ambacho huna. Hoja ya viongozi kutoka na wengine kuingia siyo mpya kikubwa wapatikane watu sahihi.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app

Sasa kama mbowe na chadema hawaon umuhim wa kutengeneza succession plan ya chama na kuandaa generation nyingine kwa baadae,huku wakitaka waende lee kubakia kwenye chama milele,Wana justification gan ya kuhubir demokrasia na kutaka katiba mpya??
 
Lengo la chama.chochote Cha siasa ni kushika Dola,kwan ww hulitambui hilo??

Sasa kama Nia yao wapinzan ni kushika dola, watawezaje kushika dola ikiwa wamegawanyika??
Kivipi unachukulia wapinzani kama chama kimoja cha siasa? Lengo la mfumo wa vyama vingi vya siasa ni kutupatia wananchi (Watanzania) uwezo wa kuchagua uongozi bora wa taifa kutokana na itikadi, sera na mipango ya vyama mbalimbali. Ni kama tunavyochagua bidhaa modeli tofauti tofauti tuseme aina za magari. Endapo waunda magari wakiamua kuungana na kutengeneza gari la aina moja tu au kwa lengo pekee la kumng'oa toka sokoni muuza magari mmoja maarufu tuseme TOYOTA, hii haitakuwa na manufaa yoyote kwa sisi wateja; itatupunguzia aina za "ladha" za bidhaa sokoni. Speaking from the citizenry perspective.

CCM moja imeshika na kuhodhi dola. Wapinzani nao ni chama kimoja kimoja kama ilivyo CCM; "hawajagawanyika". Kila kimoja kinatakiwa kitushawishi kuwa itikadi, sera na mipango yake ni bora kuliko vingine ili sisi wananchi tuwapigie kura nyingi waingie madarakani. Tatizo linalofanya vyama vya upinzani vishindwe kushika dola sio hilo unalolitaja. Be honest kama umeamua kuwa mshauri wa wapinzani. Nje ya hapo, itakuwa unawafanyia kejeli kwa vile, kama baadhi ya wadau walivyodai, hivi sasa CCM iko katika mikono maridhawa kwako.
 
Back
Top Bottom