Umoja ni nguvu, hata kama ni wa sisimizi...

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Ndugu zangu,

Nawaita wazalendo wa nchi hii popote mlipo, msikubali tuchezewe tena na hawa wapumbavu, walafi wa mali za nchi yetu.

Nawazungumzia hawa waliomo miongoni mwetu wanaotaka kunadisha mali zetu kwa maslahi yao wenyewe.

Ujinga wao ni kwamba hawana subira, wameanza kurukia miradi waliyokwishaiuza na kwa bahati yao mbaya Magufuli kawatapisha kabla ya kumeza walichokwishaanza kukitafuna.

Kuondoka kwake tu, wameona warudi kwa nguvu kuendeleza pale walipoachishwa utafunaji wao huo, bila hata ya aibu wala kificho.

Hii ni dharau kwa wananchi wa nchi hii. Wanatumia udhaifu wetu wa kutowakatalia na wao kudhani wanao uhuru wa kufanya lolote bila ya kuhojiwa.

Kama yapo mazuri aliyoyafanya Magufuli, moja kati ya hayo ni kutoruhusu wajinga hawa kutapanya mali zetu, na kwa kiasi kuamsha hisia za wananchi juu ya jambo hili.

Sasa mimi naomba, kwa wale wote wanaochukizwa na tabia hizi za baadhi ya viongozi wetu kutumia nafasi zao kujiingiza katika kuhujumu taifa hili, tuwakatalie hawa watu kwa kila njia na nguvu tunazoweza kuzitumia. Kupaza sauti ni njia moja wapo. Tuwataje waziwazi bila ya woga ili wananchi wajue.

Licha ya hiyo ya kuwaaibisha, napendekeza pawepo na umoja wa watu, kundi kubwa la watu linalochukizwa kabisa na tabia hizi za wezi hawa. Kundi hili litafute njia za kuwadhibiti hawa, na liwe na mikakati ya kuwaelimisha wananchi mara kwa mara juu ya uhujumu wa hawa watu. Kuueleza waziwazi ili wananchi wajue mipango yao ya uhujumu.

Watu kama akina Ngugai, Muhongo, na nasikitika, Zitto naye yumo? Hatuwezi kushindwa kupambana nao ikiwa tumedhamiria kuinusuru nchi yetu.

Naomba mchango wa mawazo, jinsi ya kwenda mbele na mpango huu.

(Sikuhariri).
 
Mtajua wenyewe wazalendo nachowaomba tu wakumbushe hao wakubwa zako walete ajira hela ambazo zingekuwa zipigwe Basi wahitimu tulipwe mishahara
 
Mtajua wenyewe wazalendo nachowaomba tu wakumbushe hao wakubwa zako walete ajira hela ambazo zingekuwa zipigwe Basi wahitimu tulipwe mishahara
Tayari umekwishatoa mchang muhimu wa mawazo mkuu 'Ngege JOHN".

Wapigaji, "ile pesa ilete ajira". Sawa kabisa.

Sasa kuna kichwa, nivipi hiyo pesa italeta ajira badala ya kuingia mifukoni mwa mafisadi. Msaada wako unahitajika hapo.
 
Tutazunguka kote
Tutakosoa yote
Tutajadili yote
Tutalaumu wote
Lakini bila kuwa na katiba mpya, imara na huru, tutaendelea kucheza mdundiko tu ndugu yangu
Unakumbuka tulilia sana kupata dikteta wa kutunyorosha? Kama kungekuwa na katiba huru asingetusumbua kiasi hiki
 
Tutazunguka kote
Tutakosoa yote...
Wataichelewesha sana hiyo katiba, huku wakitafuna.

SAWA.

"KATIBA" iwe ni sehemu ya "Kuzunguka kwetu; kukosoa yote, kujadili yote, na kulaumu wote"

Lakini kuendelea kuwafumbia macho hawa watu ni kosa kuliko makosa mengine yote tunayoweza kufanya.

Kunyamaza kwetu ni ruhusa kwao kuendelea na uharifu.

Kunyamaza kwetu, ni sawa na kuwapa sifa waendeleze zaidi uhaini wao.

Mbona vibaraka wao hawaogopi kuja humu na kuwasifia, na kuyafanya maovu kuwa sifa za ujasiri?
 
Back
Top Bottom