Umoja Colleges-Volunteer Opportunities Wikipedia Authors, Researchers and Translators

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Habari za wakati,

Umoja College ni taasisi binafsi ya utafiti na elimu yenye ofisi zake katika Mkoa wa Kilimanjaro.Umoja College inatoa huduma za elimu,utafiti na ushauri katika nyanja za teknolojia, biashara na ujasiriamali. Umoja College huibua na kutafiti masuala mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha mabadiliko ya kifikra na kimtazamo.Kama sehemu ya mradi wake wa kuhakikisha kunakuwa na taarifa sahihi kuhusu nchi yetu mtandaoni na kuchangia katika kuhakikisha kwamba taarifa hizo ni sahihi na zilizothibitishwa.

Katika kutimiza lengo hilo, Umoja Colleges inatekeleza mradi mkubwa a Tanzania Digital ambao unalenga kuhuisha na kuongeza taarifa mbalimbali zihusuzo Tanzania na Lugha ya kiswahili katika mtando. Baadhi ya shughuli hizo ni kutafsiri vitabu na programu za kompyuta, kuandika makala mbalimbali kwa ajili mitandao mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kuchangia katika kutafsiri katika kamusi za lugha mbalimbalimbali.

Mradi huu unatekelezwa katika mfumo wa Mafunzo na Utekelezaji na kwamba Washiriki watakuwa kama wanafunzi na iwapo watafanikiwa katika kuonesha uwezo wao wataunganishwa na fursa zaidi ila unapoomba fursa hii tambua kwamba fursa hii ni 100% volunteer na kwamba ni muhimu (sio lazima) umiliki kifaa cha electronic (ikiwezekana Computer) Ili uweze kufanya kazi yako kwa urahisi. Kumbuka hii ni kazi ya kujitolea (Haina mshahara ila kunaweza kuwa na occasional payment kwa kutegemea availability na utendaji kazi)

Nafasi za kazi zinazohitaji watu ni kama ifuatavyo:
  1. Online Article Authors for Wikipedia (Articles must meet Wikipedia Standards)
  2. Software Translators (Kutafsiri Softwares katika lugha ya kiswahili)
  3. Books and Articles translators(Kutafsiri vitabu na makala kwa lugha ya kiswahili)
  4. Researchers (Kufanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali kwa ajili ya kuongeza maarifa)
Iwapo ungependa kushiriki katika project hii tafadhali tuma Wasifu wako kwenda masokotz@yahoo.com
 
Back
Top Bottom