Ummy Mwalimu: Yeyote anayeuza dawa za asili zisizosajiliwa zikiwemo za nguvu za kiume tutamshughulikia

Me Nmemsikiliza Kigwa Ameelezea Vzr2, Tatizo Lililopo Kwa Watz Wengi Ni Uwelewa Hafifu Ya Afya Kwa Ujumla. Tendo La Ndoa Linahtaj Afya Nzr, Chakula Bora, Stress Free Na Ucwe Na Uchovu Wa Mwili. Tatzo Hli Huwakuta Watu Waishio Mijini Kwa Kukosa Utulivu, Vyakula Bora Na Uchovu Kutokana Na Mihangaiko Ya Kila Cku. Magonjwa Km Kisukari, BP Na Watu Wengine Hawana Tabia Ya Kuchek Afya Kla Mara So Utakuta Anazunguka Na Typhoid, Malaria Au UTI Kwa Muda Mrefu Bla Kujua Pia Kupelekea Mwili Kuwa Mchovu. Watu Walioko Vjjn Hupumzka Mapema, Hupata Vyakula Asili Mf.Ndiz,mihogo,matunda,mboga Za Majani, Karanga,nazi Nk Kwa Urahc Kuliko Mijn Ambako Chakula Ni Wali, Ugali, Maharage Na Nyama. Ndo Maana Watu Wanaamua Kutafuna Naz, Karanga Na Mihogo, Vjjn Hufanya Hvyo Wakiwa Mashambani. So Ni Swala La Kula Chakula Bora, Kupata Muda Wakupumzka, Kuchek Afya, Kupunguza Stress Za Kaz,madeni,kodi Za Nyumba Nk.
 
ndani ya wiki hii,vibao/bango zote zinazohusu hizo biashara zitaanza kutolewa maana wengine wengi wao wameweka hadi namba za simu

*Akifa shekhe kazi ya Mungu*
*Akifa mlevi sababu ya Pombe*
 
Mti shamba una siri zangu za kibiashara zinazonifanya nitoke halafu nije kuusajili kwako uujue ukawauzie wazungu?
 
Michakula ya mafuta hasa hasa chips ni sheeeda kweli ndio Chanzo cha nguvu kupotea jaribu kula chukuchuku utaona mabadiliko
 

Sakata la upungufu wa nguvu za kiume ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya wanaume miaka ya sasa, limeibua sintofahamu bungeni baada ya mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF) kutaka kujua serikali imejipanga vipi katika kukabiliana nalo.

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangala amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema serikali haina jibu la moja kwa moja kuweza kuwapa wananchi, kwani tendo la ndoa hufanyika faragha baina ya wanandoa.

Dkt. Kigwangala aliendelea kusema kwamba pamoja na usiri uliopo kuhusu tatizo hilo, lakini kuna vitu wanaweza kufanya ili kukabiliana nalo, ambapo huweza likasaidia kuokoa ndoa yao na kuweza kuwapatia watoto.

"Nianze kukubaliana na Mhe. Hatibu Said Haji kwa swali la msingi, changamoto za ukosefu wa nguvu za kiume zinazowapata wanaume wengi sasa hivi, zinatokana na ukosefu wa furaha, msongamano wa mawazo na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari, shinikizo la damu, ukiwa na matatizo haya huwezi kuwa na furaha katika tendo la ndoa", alisema Dkt. Kigwangala.

Naibu huyo wa Wizara inayohusika na masuala ya Afya aliendelea kwa kuwataka wananchi watafute furaha binafsi ili kuweza kuwa na hamasa ya kufanya jambo hilo, na kuacha kuamini kwenye dawa za asili ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela bila kuzingatia usalama wake kwa afya ya mtumiaji
 
Back
Top Bottom