Ummy Mwalimu: Wizara ya TAMISEMI itanufaika na tozo za miamala ya simu

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,291
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema wizara hiyo itanufaika na tozo za miamala ya simu kwa kujenga vyumba vya madarasa 10,000 na kukarabati shule kongwe za msingi 2,100. Ameeleza kuwa hadi sasa kuna uhaba wa madarasa 100,005 kwenye shule za msingi na sekondari nchini.

My Take:
Nakumbuka kuna Mdau mmoja humu alisema tatizo la Tozo lilianzia kwa Ummy Mwalimu.

Nadhani sasa picha inakuja kuwa ile pesa inatakiwa na Tamisemi.

Nadhani kwa sasa wanaotukamua kwenye huduma za mawasiliano ni Ummy+Mwigulu+Ndugulile ambao wanaomshawishi Mama Samia na yeye anawakubalia tu.
 
Bila kusahau ma-V8 ya kumwaga na semina za kutosha zenye posho za kufuru! Mmefika mahali mmewaona watanzania ni wapumbavu kabisa! Mnaweza kuwafanyia lolote na wasifanye chochote; ni makondoo fulani hivi.
 
Tanzania ingekuwa ni binadamu basi ingekuwa Yahya, mara usalama wa taifa, mara anafanya kazi benki n.k

Miaka 60 ya uhuru bado tunakosa vyumba vya madarasa kwani sisi hatuna mipango ya muda mrefu, sensa ya kila baada ya miaka 10 huwa inafanyika kwa minajili ipi?
 
Back
Top Bottom