Ummy Mwalimu: Watoa huduma za afya wasikimbie wagonjwa, sio kila homa kali ni Corona

Kiswahili ni kigumu. Sasa kama ni corona wanaruhusiwa kukimbiwa? Hata kama ni corona, mtumishi wa afya hatakiwi kumkimbia mgonjwa.
Ila anapaswa kurisk Maisha yake (kwa sababu ya uzembe wa Boss wake ambaye hajampatia vifaa husika) ? Hawa nao wana familia na wanatamani kuishi.
 
Ukisikia polisi kumkimbia kibaka na mwanajeshi kujificha akimuona muasi ndo hii. Sasa daktari anamkimbia mgonjwa ili ahudumiwe na muhudumu wa bar!
 
Ningekuwa Muhudumu wa afya nchini tanzania walahi ningeshaacha kazi I swear
Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema watoa huduma wa sekta ya afya hawatakiwi kuwakimbia wagonjwa na badala yake, wanatakiwa kuzingatia Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi katika kutoa Huduma (IPC)

Ummy amesema sio kila homa kali au kikohozi ni CoronaVirus hivyo watoa huduma hawatakiwi kuwakimbia wagonjwa kwasababu kuna magonjwa mengine kama Kisukari, Moyo, HIV na TB.

Pia, Waziri huyo amewataka kuendelea kuwa makini kwa kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo kunawa mikono pale wanapotoa huduma.

Msikilize akizungumza hapa:

View attachment 1428061
 
Kiswahili ni kigumu. Sasa kama ni corona wanaruhusiwa kukimbiwa? Hata kama ni corona, mtumishi wa afya hatakiwi kumkimbia mgonjwa.
Hebu jaribu kuva viatu vya... Umeletewa ana madonda kibao unaambiwa umsafishe mikono mitupu...
 
Hivi kwa akili zako unadhani hata hao madaktari wa nje watakubali kufanya kazi bila protective gears?

Labda kama ni mazombi...
Nimesikiliza maneno ya waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwaasa wahudumu wa Afya kutowakimbia wagonjwa wa Corona tayari. Sijashangazwa na Hali hiyo kwa sababu wabongo kila kitu huwa tunafeki na hapa pia ndipo utapata majibu kwamba hata madegree ya udakitari waliyonayo watu Ni upuuzi mtupu.

Nimepata kuona baadhi ya video zikionyesha wagonjwa wakibeba maiti baada ya wahudumu wa Afya kuikimbia. Lakini pia nimesikiliza audio ya mtu aliyedai kuwa Ni mgonjwa wa Korona aliyelazwa Amana hospital akilalamikia huduma duni kutoka kwa madaktari na kusema kuwa wanawakimbia na kuogopa kuwahudumia.

Kwa Hali inavyoendelea na Kasi ya maambukizi ilivyo Ni vema Serikali ianze kuangalia utaratibu wa kuomba msaada wa madaktari kutoka nje maana Hawa tuliona waliaokariri vitabu tu Kuna siku wote watazikimbia hospital.
Ni Hayo tu.
 
Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema watoa huduma wa sekta ya afya hawatakiwi kuwakimbia wagonjwa na badala yake, wanatakiwa kuzingatia Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi katika kutoa Huduma (IPC)

Ummy amesema sio kila homa kali au kikohozi ni CoronaVirus hivyo watoa huduma hawatakiwi kuwakimbia wagonjwa kwasababu kuna magonjwa mengine kama Kisukari, Moyo, HIV na TB.

Pia, Waziri huyo amewataka kuendelea kuwa makini kwa kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo kunawa mikono pale wanapotoa huduma.

Msikilize akizungumza hapa:

View attachment 1428061
Tumewasamehe kwa kutojihusisha hata kidogo katika ugunduzi wa tiba na chanjo as if wamesomea umeme ila hili la kukimbia wagonjwa hatutawasamehe
 
Waziri hatakiwi kuongea hayo aliyoyaongea. Anatakiwa kuongea jinsi Serikali ilivyojiandaa kwa vifaa tiba ili kuwahakikishia usalama wao, watoa tiba. Watoa tiba wana akili, ni binadamu. Hata uwaambie vipi, kama mazingira ya kazi ni hatarishi, hakuna atakayekusikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa afya mh Ummy Mwalimu amewataka wahudumu wa afya katika hospitali za serikali na binafsi kutowakimbia wagonjwa wa Corona.

Kadhalika waziri Ummy ametoa wito wagonjwa wa Corona na wale waliopona wasinyanyapaliwe kwa namna yoyote ile.

Source: Mtanzania
Wewe unaweza kumtia kavukavu demu mwenye ngoma?
 
EWZXn5uXYAIszQT.jpg
 
Back
Top Bottom