Ummy Mwalimu: Wanaume acheni woga pimeni tezi dume, kuna vifaa vya kisasa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
TATIZO la saratani nchini limetajwa kuongezeka kwa kasi, ikibainishwa kuwapo wagonjwa wapya 42,060 kwa mwaka huku 28,610, sawa na asilimia 68 hufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Taarifa za mwaka 2021 za Taasisi ya Saratani Ocean Road zinaonyesha saratani zinazoongoza kwa wanaume ni tezi dume huku wanawake ni ya mlango wa kizazi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, aliyasema hayo jana jijini hapa alipotoa tamko la Siku ya Saratani Duniani.

Alisema kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Tanzania imeshuhudia ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani zinazochangiwa na mtindo wa maisha kulinganishwa na ilivyokuwa awali ambapo wagonjwa wengi walikuwa ni wale wenye saratani zinazotokana na maambukizi ya virusi.

Alisema takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) za mwaka 2018 zinaonyesha kwa Tanzania watu 76 kati ya 100,000 hugundulika kuwa na saratani.

“Takwimu kutoka kwenye kanzidata (Population Based Cancer Registry) zilizoanzishwa kwa kanda, zinaonyesha kwamba wagonjwa wapya 14,136 walifikiwa na huduma ambayo ni sawa na asilimia 33 ya makadirio ya wagonjwa wapya wote kwa mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia tano kulinganisha na takwimu za mwaka 2020 ambapo jumla ya wagonjwa wapya 12,096, sawa na asilimia 28 walionwa,”alisema.

Alibainisha kwa wanaume saratani zinazowaathiri zaidi ni pamoja na tezi dume kwa asilimia 21, saratani ya koo (asilimia 11.8), saratani ya utumbo mkubwa na mdogo (asilimia tisa) na saratani ya mdomo na kinywa (asilimia 7.3).

“Tezi dume inaongezeka sana, nitoe wito kwa wanaume mjitokeze kupima, acheni kuogopa. Kwa sasa kuna kipimo cha kisasa sio kile ambacho mnakijua au kukifikiria… Na pia kwa wanawake mkijitokeza kupima saratani ya mlango wa kizazi na matiti, tutaweza kudhibiti kwa kiwango kikubwa," alisema.

Waziri huyo alisema kwa wanawake saratani zinazowaathiri zaidi ni pamoja na saratani ya mlango ya kizazi (asilimia 43), saratani ya matiti (asilimia 14.2) na saratani ya koo (asilimia 3.8).

Hata hivyo, alitaja sababu nyingine ya ongezeko la wagonjwa hao na magonjwa mengine yasiyoambukiza linachangiwa na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake, matumizi ya pombe kupita kiasi na ulaji usiofaa kama kutokula mbogamboga na matunda, matumizi ya chumvi na sukari kwa wingi.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Ummy aliagiza itengwe siku maalumu kila mwezi kwa ajili ya kupima saratani kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na uchunguzi.

Pia alisema katika kuongeza uelewa kwa jamii, serikali inaandaa mtaala wa mafunzo shuleni unaozungumzia magonjwa hayo na udhibiti wake.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikifanya kampeni maalumu na kuhimiza wananchi kufanya uchunguzi wa afya zao ili kubaini ugonjwa katika hatua za awali,” alisema.

NIPASHE
 
Nimesoma heading tu.
Swali: shemeji yetu kupitia kwa Ummy yeye anasemaje kuhusiana na ushauri huu wa waziri?
 
Watoe elimu namna ya upimaji yale mambo ya mtu mzima kupimwa oil muhali jamani
 
Vifaa vipo, Ila matibabu ni mtihani. Saratani ni saratani, kuua hakuna mjadala!
 
Ukiwahi kugunduwa tatizo unatibika kwa vidonge tu. Tatizo likishakuwa ni prostate cancer kinachofuata hapo ni miyeyusho tu.

Hapo mwanzo sikujuwa kwa nini Kikwete alikwenda kufanya oparesheni Marekani kumbe alikuwa sahihi sana.
 
Back
Top Bottom