Ummy Mwalimu na Faustine Ndugulile mmeamua kuua wananchi kwa maamuzi ya kukurupuka?

Keyura

Member
Aug 14, 2015
83
109
Wanajamvi, sina nia ya kuichafua wala kuishutumu Serikali kwa hatua mbalimbali wanazochukua kwa ajili ya kujikinga na maradhi ya Covid-19. Lakini hapa serikali ilipofikia naona imeamua kwa makusudi kuua wananchi kwa maamuzi ya kukurupuka hasa kwa kuwahamisha watu waliojitenga mahotelini na kuwaweka sehemu moja kwenye hosteli almaarufu za Magufuli.

Kuwapeleka wasafiri hosteli za Magufuli mliangalia kigezo gani je mmewahukumu wasafiri wote ni wagonjwa? Ukitazama kunamapungufu makubwa kwenye hostel zenyewe kama vyoo watu wanachangia inamaana wizara haijui kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa kusambaa? Kama mtu kabakiza siku tatu, mbili moja je kulikuwa na haja gani kumuhamisha mtu usiku kwa usiku kwenda hostel za Magufuli?

Mtu alipofika alichagua hoteli ya kukaa kwa gharama anyoona yeye inamfaa baada ya kuchagua kuna maana gani ya kumuhamisha mtu kijihadi na kumpeleka maeneo hatarishi zaidi?

Kama nia ni kuwaweka watu sehemu ili kuwapunguzia gharama na kuwamonitor kwa hili mawaziri na kamati zenu mmekosea sana kwa kiwango cha lami kwani hamkuangalia mazingira na risk itakayokuja kutokeza huko mbeleni. Je wasafiri waote mmewapima ili kujiridhisha na usalama wao?

Ni kwanini muwapeke watu hosteli za magufuli bila kujua kwanza kama ni wazima au la? Maana tangu watu wafike wanapimwa joto je mtu akiwa na COVID-19 na kafika jana na akafanya kuzambaza ni sekunde tu hosteli zoote ni kilio na kusaga meno hivi hamuoni ni risk ni kubwa kuliko hapo walipokuwa awali?

Sasa mtu anamaliza leo mnatarajia kumpa cheti leo je kama huko kooote amekaa bila kuupata ugonjwa na kafika leo na kaupata na mnampa cheti kwa kuhitimu kukaa isolation place for 14 days na akatoka nao hamuoni kama mnaongeza ujasiri wa kusambaza ungonjwa kwa haraka zaidi kuwa na cheti maalumu cha kuzambaza ugonjwa?

Kibaya zaidi watumishi wa ustawi wa jamii waliochaguliwa kusimamia hili zoezi wamekuwa na kauli mbaya na kejeli hv hamjui hawa mnaowakejeli wanaweza kuwa salama na ninyi mkawa ni hatarishi kwa maisha yao? Kwa upande mwingine mnaowaweka na kuwatamkia maneno machafu ni watumishi wenzenu wa serikali? Kama mtampa cheti maalumu za kukaa karantini hamuoni ni tiketi ya kuja kuusambaza nanyinyi mkaupata?

Makonda nawewe ulikuwepo; kama ulihusishwa au haukuhusishwa hili suala lipo mikononi mwako na hawa wananchi mnawaweka hapa wapo wa mataifa mbalimbali hivi hamuoni kama mnalichafua taifa kwa kufanya maamuzi yasiyokuwa na tija bali ni kutafuta sifa za kiutendaji?
 
Dunia nzima uchumi umesimama shughuli zimesimama, wewe unakuja Tanzania unafuata nini? Au ndio unausambaza kwa makusudi? Au unaenda China kufuata mzigo kweli kipindi hiki. Si unafanya makusudi kabisa? Au wewe ndio unaijua pesa sana.
 
Mh Makonda kasema tutoke tukaafanyè kazi. Sasa kaz yangu ni kusafiri kufata mizigo kuleta bidhaa.

Nmetii ushauri wa Rc
Dunia Nzima uchumi umesimam shughuli zimesimama, wewe unakuja Tanzania unafuata nini? Au ndio unausambaza kwa makusudi? Au unaenda China kufuata mzigo kweli kipindi hiki. Si unafanya makusudi kabisa? Au wewe ndio unaijua pesa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akilinjema,
Wengi wanatoroka hizo karantine. Kuna mmoja katoroka wakamkuta Iringa huko. Manake kama anaui ameshaambukiza Familia yake yote tena kwa makusudi.

Tena huyu ni mwanamke bila Huruma kabisa. Mwingine alivyotoroka hadi leo hajaonekana wanasema ni wa Malawi.
 
Saint Ivuga,
Kukaa kwenye zile hosteli ni gharama kubwa na kulikuwa kibiashara au kisanii zaidi. Kwa jinsi vyuma vilivyokaza, hata mimi ningelazwa kwenye zile hosteli, siku ya tatu ningesepa zangu na hakuna kima angejua niko wapi.

Ukweli ni kwamba waliosepa zao kimya kimya ni wengi sana, tena wengi wao ni watu wazito fulani au mashuhuri na hakuna mtu wa kumfuatilia mwenzake.
 
Hamrishiki wabongo hii sasa too much hotelini watu walilia humu gharama kubwa haya hosteli mnalalamika tena hambebeki..

Pili nahisi wamepelekwa huko mana kuna tarifa zilitoka humu watu wanaekwa karantinj ila wanatoka wanajichanganya kwny baa za hoteli so huko hosteli ndio penyewe huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulitarajia vyuo kufunguliwa tarehe 20 mwezi huu, sasa ni dhahiri likizo imeongezwa na baadae wanafunzi hawatokuwa salama kuzitumia hostels hizo kwa muda.
 
Kwa sasa tumeanza kutumia hosteli mpya mpya za UDSM, Pakijaa tutawapeleka hosteli zingine hapo hapo main campus UDSM, baadaye hosteli za Mabibo, baadaye zaidi hosteli za vyuo vingine vya umma. Katika hili tumejipanga.

Kwa kuwa mmejipanga, basi tuambieni likizo ya vyuo itaendelea hadi lini.... awali mlisema mwezi mmoja ambao leo bado siku 14 tu.
 
Pole sana, itakuwa ni muhusika au una ndugu yako yuko kalantini sio kwa hasira hizo. Lakini pia kuna watu walilalama kwamba huko hotelin gharama ziko juu sana na kuna waliokuja na mawazo kwamba hostel za UDSM zitumike kuwahifadhi hawa watu ili kuepusha kama sio kupunguza gharama so hii imefanyika hivyo bado mnalalamika, nadhani tukubaliane kwamba sio rahisi kumfurahisha kila mmoja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom