Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi hakuna kusafiri nje ya mkoa bila kibali

Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu ametangaza kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa mkuu wa mkoa ,wilaya au mkurugenzi yoyote kusafiri nje ya mkoa wake bila kibali cha rais, makamu wa rais au waziri mkuu.

Ummy amesema serikali inataka kuona viongozi hao wanabaki kwenye maeneo yao ya kazi ili waweze kusimamia vyema miradi itakayojengwa kutokana na fedha zilizotolewa na IMF kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Corona nchini kiasi cha trilioni 1.3.

Huyu hajui hata sheria na kanuni za utumishi wa umma yupo yupo tu anakenua meno kama chizi.
Bi ummy unapaswa ufanye marejeo ya sheria, kanuni na taratibu zipi? Zinakataza na kwann?????
Mm DMO meatu... nimemkaimisha ofisi DRCHco kwakuwa naenda likizo yangu ya mwaka ambayo ipo kisheria! Wewe unanikataza! Mm cyo ofisi! Mm no mtu mwenye cheo cha DMO kazini kwangu!
Sasa napaswa kupewa kibali cha nn hapo?
 
Kaombe kibali wewe acha kulialia
 
Kila Kiongozi ni lazima a control Nyumba yake,Watumishi wote ni vyema wawe na vibali maalumu Kama anatoka kwenye kituo chake cha kazi! Siyo Mwananchi anatembea umbali mrefu kuja kumuona Kiongozi ili amuelezee matatizo yake yanayo msibu alafu akifika anakuta Kiongozi hayupo na hakuna Maelezo ya kujitosheleza kumpa Mwananchi wala wakumsaidia!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Usipende ku comment mambo usiyoyajua mkuu. Kiongozi ni mtu.. ofisi ni tofauti na kiongozi......
Raisi amemtuma GWAJIMA DR. kwenda URUSI kumwakilisha.kwenye mkutano ule gwajima hakuwa kama gwajima wazir Bali alisimama kumuwakilisha raisi hivyo gwajima ni raisi pale urusi
 
Ruhusa sawa, lakini kibali hadi kipitishwe na rais, huko msibani wanakusubiri wewe tu...... bora utaratibu ule ule utumike, mfano kama mkuu wa mkoa amepata dharura ya kusafiri amtaarifu waziri wa tamisemi, DED na mkuu wa wilaya wamtaarifu mkuu wa mkoa.....
Na hii ni kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma
 
Eti mazuzu, Mnajikutaga mnajua sana mambo, kumbe ni zero kabisa
Unaona sawa kabisa ofisi ya Raisi kutoa vibari vya kusafiri wakuu wa mikoa tena ndani ya nchi, hata kama kuna umuhimu wizara husika inaweza, matumiazi ya ovyo ya ofisi ya Raisi hayo kuna ya muhimu sana anaweza kufanya hilo sio mojawapo
 
Usipende ku comment mambo usiyoyajua mkuu. Kiongozi ni mtu.. ofisi ni tofauti na kiongozi......
Raisi amemtuma GWAJIMA DR. kwenda URUSI kumwakilisha.kwenye mkutano ule gwajima hakuwa kama gwajima wazir Bali alisimama kumuwakilisha raisi hivyo gwajima ni raisi pale urusi
Haya Maelezo yako nenda kajitetee nayo kwa Ummi Mwalimu,yeye ndiyo ametoa maagizo hayo,Mimi nilikua nakazia tu! Pole Kama agizo la Ummi Mwalimu litakuaathiri!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
hahahahaha....Mbona Rais ni mkubwa sana kudeal na hilo....kwanini usiwekwe utaratibu tu wakawa wanaufuata?...

wekeni vimachine vya kupunch kwa finger print in and out kwa MaRC na watendaji wote wa serikali then in monthly basis ukaguzi unafanyika....

Hivi vimachine viwekwe kwenye taasisi zote za umma na serikali yenyewe na viwe linked na payroll systems kila mtu anaposhindwa kupunch anakutana na maumivu kwenye mshahara tena makato yawe doubled...
Hili wazo walichukue wapumbavu hao
 
Haya ni matokeo ya viongozi wetu kua wengi sehemu moja alafu wanalingana kimamlaka alafu hawana majukumu makubwa yakufanya.Wangekua na majukum makubwa yakuwaweka busy hayo mambo yakuzurura wala yasingeonekana kama ni tatizo.Lakini pia kama tungekua na katiba bora inayotenganisha mamlaka za hawa wateuliwa vyeo vingine wala visingekua na haja yakuripoti kwa waziri mkuu au ofisi ya raisi.Kuna mambo hayako sawa kabisa ila tunafanya kwamazoea matokeo yake ndo kunaibuka matamko kila leo.
 
Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu ametangaza kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa mkuu wa mkoa ,wilaya au mkurugenzi yoyote kusafiri nje ya mkoa wake bila kibali cha rais, makamu wa rais au waziri mkuu.

Ummy amesema serikali inataka kuona viongozi hao wanabaki kwenye maeneo yao ya kazi ili waweze kusimamia vyema miradi itakayojengwa kutokana na fedha zilizotolewa na IMF kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Corona nchini kiasi cha trilioni 1.3.

Siku zote wakuu wa mikoa ruhusa zao zinatoka ofisini kwa Waziri Mkuu na DED kwa RC, sioni jipya
 
Haya ni matokeo ya viongozi wetu kua wengi sehemu moja alafu wanalingana kimamlaka alafu hawana majukumu makubwa yakufanya.Wangekua na majukum makubwa yakuwaweka busy hayo mambo yakuzurura wala yasingeonekana kama ni tatizo.Lakini pia kama tungekua na katiba bora inayotenganisha mamlaka za hawa wateuliwa vyeo vingine wala visingekua na haja yakuripoti kwa waziri mkuu au ofisi ya raisi.Kuna mambo hayako sawa kabisa ila tunafanya kwamazoea matokeo yake ndo kunaibuka matamko kila leo.
Tabu tupu kila mtu anajiona ni mkubwa sn
 
Kila Kiongozi ni lazima a control Nyumba yake,Watumishi wote ni vyema wawe na vibali maalumu Kama anatoka kwenye kituo chake cha kazi! Siyo Mwananchi anatembea umbali mrefu kuja kumuona Kiongozi ili amuelezee matatizo yake yanayo msibu alafu akifika anakuta Kiongozi hayupo na hakuna Maelezo ya kujitosheleza kumpa Mwananchi wala wakumsaidia!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Tuna mfumo mbovu sn ndiyo maana hatuna maendeleo
 
Back
Top Bottom