Troll JF
JF-Expert Member
- Feb 6, 2015
- 7,804
- 12,233
Waziri wa Afya akiwa anakutana na wanahabari mchana huu kuzungumzia mlipuko wa ugonjwa wa EBOLA nchini.
Hadi sasa wameripotiwa wagonjwa 43 wa Ebola na wanne wameripotiwa kufa huko Congo.
Shirika la Afya Duniani (WHO) wametahadharisha kuenea kwa ugonjwa huu kwa nchi jirani na Congo.
Kila Wiki, tuna timu yetu inayowasiliana na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu EBOLA hapa nchini.
Tumegawa vidonge na vifaa kinga kwa vituo vyote katika Mikoa yote inayopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Msafiri yeyote anayetoka Kongo DRC kuja Tanzania lazima tumpime na kujiridhisha hana EBOLA.
Tumeweka " register" maalumu ambapo wasafiri wote wa kwenda na kutoka Congo DRC wanatakiwa kujaza.
Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu ila wachukue tahadhari.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kuwapima wasafiri wote kwenye mipaka yetu na Congo DRC.
Changamoto kubwa ya kudhibiti EBOLA isiingie nchini ni uwepo wa "njia za panya" nyingi huko mipakani.
Hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa EBOLA [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG]. Tumechukua tahadhari katika mikoa yote inayopakana na Congo DRC.