Ummy Mwalimu: Atakayevurunda kwa fedha za Maendeleo ya Taifa, hatutamuhamisha kituo, tutamfikisha TAKUKURU

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Mkurugenzi atakayefanya ubadhirifu kwa fedha ambazo serikali ilipokea na kutoa kwa ajili ya maendeleo ya taifa na kupambana #COVID19 hawatawahamisha vituo.

Amesema hawatakuwa na mchezo katika fedha hizi, mtu akivurunda atafikishwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kuchukuliwa hatua.

Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Mapambano ya COVID-19 ulizinduliwa na Rais Samia Oktoba 9.
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
The poor man is there, he doesn't have a word, the cake is being eaten, the poor man is just begging, O God, I beg you to let me have food.
 
Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Mkurugenzi atakayefanya ubadhirifu kwa fedha ambazo serikali ilipokea na kutoa kwa ajili ya maendeleo ya taifa na kupambana #COVID19 hawatawahamisha vituo.

Amesema hawatakuwa na mchezo katika fedha hizi, mtu akivurunda atafikishwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kuchukuliwa hatua.

Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Mapambano ya COVID-19 ulizinduliwa na Rais Samia Oktoba 9.
Fanyeni vitendo maneno haya haya kila siku! Ukiona haya maneno ya vitisho yanakuwa mengi ujue mzigo ushaibiwa mda tu. Atakuja kushatikiwa mtu aliyeiba million 15 na watanzania kuaminishwa huyu ndo kafanya msipate maendeleo. Nao wao roho ya kinyonge kupokea taarifa na kuendelea kumsubiri mkombozi wao ambaye wanadhani anaweza tokea kila baada ya miaka mitano.
 
Hii kazi aliiweza yule jamaa Marehemu, wengine sinema tu mnaleta...unaongelea kuwapeleka watu takukuru huku unachekacheka...

Nchi ina mafisi hii hatari, ili uwatulize kesi za uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, kuwafirisi na ubabe mwingi ndio dawa yao hakuna kingine..
 
Kama kweli huyo Ummy anamaanisha,aende kuwakamata wezi jimboni kwake ambao walifikishwa huko TAKUKURU
TAKUKURU ya Tanga yenyewe inabidi iundiwe TAKUKURU ya kuwachunguza. Niwala rushwa hata serikali inajua na watumishi wake wakuu wawili walisimamishwa kwa tuhuma za rushwa
Ummy acha maigizo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom