Ummy Mwalimu: Asilimia 31.8 ya watoto chini ya miaka mitano Nchini wana Utapiamlo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,626
51,581
Waziri wa Afya ndugu Ummy Mwalimu amesema kuwa Katika nchi yetu ya Tanzania, watoto chini ya miaka mitano asilimia 31.8 wana utapiamlo.

Waziri akaendelea kusema kuwa, hali hiyo inahatarisha maendeleo ya ukuaji ubongo wa watoto hao kitu kinachoweza kupelekea udumavu wa akili.

Mimi binafsi nimeogopa sana kwa takwimu hizi. Hawa watoto ndiyo Taifa la kesho, Je taifa litakuwa ni taifa la namna gani kama 31.8% ya watoto wachanga leo ni wadumavu.

Hapo ndipo ninapojiuliza, Je serikali hii ambayo inajitapa kuwa tumeingia uchumi wa kati, huo uchumi wa kati unatusaidia nini kama asilimia 31.8 ya vichanga vyake vipo katika hatari ua udumavu wa akili sababu ya utapia mlo?

Watu wanapolalamika kuhusu maendeleo ya watu vs Maendeleo ya vitu wanakuwa wanamaanisha vitu kama hivi. Kiukweli, hizi takwimu zinatisha.

Serikali ianze kuwekeza kwenye maisha bora ya wananchi badala ua kuwekeza kwenye miradi ya tembo mweupe kama vile uwanja wa ndege Chato na daraja la baharini huko Dar es Salaam.

Kwa vyovyote vile Taifa inabidi litokwe na machozi kuona 31.8% ya vichanga vyake huenda vikadumaa akili sababu ya utapiamlo.

Serikali iweke priorities zake sawa

kwani mlikuwa hamumuelewi HASHIMU RUNGWE na swala lake la lishe kwa Watanzania? watanzania walio wengi wamedumaa na chanzo chake ni lishe duni kuanzia utotoni mpaka uzeeni...

Aisee kumbe ukichunguza sera ya Rungwe ina maana sana.
Kama 31.8% ya watoto wana utapiamlo kuna uwezekano wa IQ zao kuja kuwa chini. Sasa hawa baadae ndo watakuwa viongozi wetu n. k
Tukija kuwa na Taifa la mambumbu, wataweza kucompete kweli na mataifa ya watu wenye akili zilizishiba?

Serikali wekezeni kwenye basic needs kwa nguvu zaidi kuliko kujenga maviwanja ya ndege huko Chato
 
Hili ni tatizo la miaka mingi sana, lishe duni na udumavu ni janga la Taifa na nguvu kubwa ilitakiwa kuwekwa huko kuokoa kizazi na Taifa.
Hili ni moja la tatizo ambalo linatakiwa lishughulikiwe kwa haraka na misingi iwekwe vinginevyo tutaendelea kuwa Taifa ombaomba lisilojiweza kwa kila kitu...
 
Ndugu Membe, Lissu, Zitto na Mbowe.

Hili suala la utapiamlo na udumavu kwa watoto lazima mlishikie bango na kuliandalia majibu ili muweze kuwashawishi wananchi kuwa mnayo majibu ya suala hilo.
CCM wameshindwa kunusuru kizazi

Average IQ ya Taifa itakuwa chini sana kwa sababu ya watoto mamilioni kwa mamilioni kudumaa kwa kukosa lishe bora.

Huu ni msiba mkubwa sana kwa Taifa
 
Hili ni tatizo la miaka mingi sana, lishe duni na udumavu ni janga la Taifa na nguvu kubwa ilitakiwa kuwekwa huko kuokoa kizazi na Taifa.
Hili ni moja la tatizo ambalo linatakiwa lishughulikiwe kwa haraka na misingi iwekwe vinginevyo tutaendelea kuwa Taifa ombaomba lisilojiweza kwa kila kitu...

Umesema fact
Haya ndo mambo ya kupewa priority
 
Waziri wa Afya ndugu Ummy Mwalimu amesema kuwa Katika nchi yetu ya Tanzania, watoto chini ya miaka mitano asilimia 31.8 wana utapiamlo.

Waziri akaendelea kusema kuwa, hali hiyo inahatarisha maendeleo ya ukuaji ubongo wa watoto hao kitu kinachoweza kupelekea udumavu wa akili.

Mimi binafsi nimeogopa sana kwa takwimu hizi. Hawa watoto ndiyo Taifa la kesho, Je taifa litakuwa ni taifa la namna gani kama 31.8% ya watoto wachanga leo ni wadumavu.

Hapo ndipo ninapojiuliza, Je serikali hii ambayo inajitapa kuwa tumeingia uchumi wa kati, huo uchumi wa kati unatusaidia nini kama asilimia 31.8 ya vichanga vyake vipo katika hatari ua udumavu wa akili sababu ya utapia mlo?

Watu wanapolalamika kuhusu maendeleo ya watu vs Maendeleo ya vitu wanakuwa wanamaanisha vitu kama hivi. Kiukweli, hizi takwimu zinatisha.

Serikali ianze kuwekeza kwenye maisha bora ya wananchi badala ua kuwekeza kwenye miradi ya tembo mweupe kama vile uwanja wa ndege Chato na daraja la baharini huko Dar es Salaam.

Kwa vyovyote vile Taifa inabidi litokwe na machozi kuona 31.8% ya vichanga vyake huenda vikadumaa akili sababu ya utapiamlo.

Serikali iweke priorities zake sawa

Huyu mama amesahau kwamba nchi hii takwimu hazitolewi ?
 
kwani mlikuwa hamumuelewi HASHIMU RUNGWE na swala lake la lishe kwa Watanzania? watanzania walio wengi wamedumaa na chanzo chake ni lishe duni kuanzia utotoni mpaka uzeeni...
Rungwe ni Genius acha tu! Ile Sera yake yaa kumwagilia kwa ndege ilikua nzuri sana sana
 
Kuna dhana ya kusema kua,mtoto asipewe mulo mwingine ,anyonye ziwa la mamaake hadi miezi 6.

Dhana hii mm sikubaliani nayo.
Wamama wenye wa kitanzania afya zao za mgogolo.unategemea atakua na maziwa yakutosha?

Kama mama mwenyewe anautapiamulo mtoto ataponaje.
 
Halafu Kuna majitu yanaimba uchumi wa Kati kutwa kucha.

Uchumi wa kati wakati 31.8% ya watoto wachanga wana utapiamlo.
Huo uchumi wa kati ni uchumi wa kati upi?

Hilo ndo tatizo la kushangilia uchumi wa kwenye makaratasi halafu kumbe wananchi wana njaa, na watoto wanadumaa akili kwa ukosefu wa lishe bora!
 
Pale unaposikia baba kajenga nyumba 20 anakarabati kijijini kwa Bibi,watoto wanalalia mlo mmoja,matokeo yake ndio haya
Duh, huu mfano umeuweka vizuri zaidi
Kuna statement moja hayati Benjamin William Mkapa alisema kwamba kwake yeye binafsi, kama kila mtu ndani ya nchi anaweza kuafford chskula bora bila wasiwasi wowote, basi kwake hayo ni maendeleo makubwa sana.
Wakati huo sikumuelewa, lakini baada ya takwimu hizi za Ummy Mwalimu, Naona Mkapa alikuwa sahihi 100%
Huwezi kujisifu kujenga daraja la baharini wakati 31.8% ya watoto wako wachanga wapo hatarini kudumaa akili
 
Back
Top Bottom