Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 251
Leo ni Siku ya Akina Mama Duniani, magazeti ya leo yamepambwa na simulizi za Wanasiasa Wanawake, mmoja wapo akiwa Bi. Ummy Mwalimu, aliyeonekana kwenye Ukurasa wa Mbele wa Habari Leo, bila maelezo kumhusu.
Kati ya mambo ambayo sibarikiwi nayo ni kitendo cha wanasiasa kuchukua sifa zote zinazotokana na kazi ngumu za wataalamu wetu na Watanzania wengine wa kawaida.
Zama hizi za #HapaKaziTu iliyobadilika na kuwa #HapaSifaTu viongozi wa kisiasa wamekuwa mstari wa mbele kutumbua majipu, utumbuaji ambao kwa kiwango fulani ni upuuzi mtupu unaojaza inzi bure bila kubadilisha hali ya mambo.
Da Ummy, Waziri wa Afya, Mwanasiasa Mkuu wa Wizara ambayo inahitaji siasa kidogo iwezekanavyo hayuko nyuma kwenye hili. Hazipiti siku mbili tatu bila kumuona gazetini ama kwenye multimedia, pengine akitumbua majipu au akifanya tu 'majukumu yake'!
Kwenye majipu sikuwa na tatizo sana, lakini siku ambayo Ummy alitolewa Ukurasa wa Mbele wa Gazeti akihamisha vitu kwenye Ofisi za Wizara zilizoamriwa kuhama Muhimbili niliingiwa na shaka.
Kawaida Ofisi za Serikali ni nyeti, uhamishaji wa nyaraka na vitu hufanyika kwa umakini na hadhari ya hali ya juu.
Mwanasiasa huyu kapatapi utaalamu huo wa kudeal na nyaraka nyeti kama hizo za wizara, zinazohusu afya za watu, tena akibeba boksi analojisikia kwa wakati wake?
Siku kadhaa nyuma bidada alionekana akifanya usafi kwenye Ofisi za Wizara, Usafi ambao wala haukuwa ule wa Magufuli, usafi huu uliripotiwa kama utaratibu wa kawaida tu wa Waziri huyo.
Sasa nikajiuliza, kwa 'jobu diskripsheni' ipi? Kwa viwango gani vya usafi wa maofisini ambavyo Ummy anavijua? Hata glavu hajavaa, sina uhakika kama anafahamu uhusiano kati ya umeme na hayo maji anayodekia, lakini ati anafanya usafi kuonesha ni mchapakazi.
Mbaya ni pale magazeti Makubwa yanaposhadadia habari hizo kwa namna ambayo bila shaka ni ya kununua, mfano picha zake akifanya usafi kutoka kwenye gazeti moja la kila siku kwenye kurasa mbili tofauti za toleo moja, ukiwemo Ukurasa wa Mbele.
Sina shida na utumbuaji majpu, lakini sifa kama hizi zinatupotezea muda na kusema ukweli hatuzihitaji.
Kama Waandishi wana hamu ya kutujuza ya Serikalini waweke 'mgawanyo' wa majukumu yao hadharani, tujue mnakaa wizarani saa ngapi, mnaenda Majimboni saa ngapi na shughuli za Chama mnafanya saa ngapi, na yote kwa rasilimali na mishahara ipi.
Pia mnaweza kuanza kuongea na watendaji wa Wizara, yaani badala ya kumuona bibie akiuza sura, ningependa niwaone Maafisa Watendaji wa Wizara wakifanya yao kazini, wananibariki kuliko hawa 'wasema hovyo'.
Ummy, fanya siasa zako, ila acha sifa!