Uchaguzi 2020 Ummy Fussi wapiga kura wa jimbo la Mpwapwa tuna imani kubwa kwako usituangushe.

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,689
Sisi wananchi wa jimbo la uchaguzi la Mpwapwa tuna imani kubwa na wewe Mhe. Ummy Fussi kwani tunategemea utampokea kijiti cha uongozi wa uwakilishi Mhe. George Malima Lubeleje ambaye amefanya kazi kubwa sana ya kutuwakilisha kwa zaidi ya miaka 30 lakini sasa utu uzima umemfika.

Mhe mtalajiwa Ummy Fussi wa mtaa wa mwanakianga tunamategemeo makubwa sana kwako kwani ni mwana mama utakayeyaendeleza mazuri yaliyofanywa na mheshimiwa Lubeleje, hakika tunaamini kabisa wakinamama mnaweza kama alivyoweza mwana mama jasiri Mhe. sana Une Mwaimu wa Tanga mpaka juzi Rais amemsifia na wapiga kura wake wa Tanga wanamwita Iron Lady.

Mhe Ummy Fussi mwana mama wa kijiji cha Bumila na mkazi wa mtaa wa mwanakianga Mpwapwa utakapompokea kijiti Mhe. Lubeleje sisi wa Bumila wenzako tunaomba katika kipindi chako cha uwakilishi ukafanye yafuatayo bila kukosa:-

1. Ukapiganie tujengewe zahati itakayohudumia vijiji vya Bumila, Chibwechangula na Lupeta na ijengwe katikati yaani kijiji cha Chibwechangula.

2. Ukapiganie ijengwe barabara ya kutoka Mbuyuni Kongwa hadi Mpwapwa kiwango cha lami ambapo barabara hiyo itasaidia hata wanachi wa jimbo la uchaguzi la Kibakwe, Barabara hiyo Mhe Lubeleje kaipigania weeeee, lakini hakufanikiwa tunaomba wewe mwana mama jasiri ukafanikiwe. Hayo ni kwa uchache tusikupe majukumu mengi kwanza.

Hakika wana mama huu ni mwaka wenu msiende mkatuangushe wananchi wenzenu wa Mpwapwa tunaomba Mh. Ummy FUSSI ukafanye kweli hakika akina mama mnaweza.
 
Kumbe barabara haijajengwa!

Yaani tangu 2014 Mh.zabena muhita mhaji akiwa bungeni alipomuuliza kuhusu ujenzi wa barabara hii Mh.JPM,Hadi leo holaaaa

Amakweli kidumu chama cha mapinduzi
 
Mchagueni Mbowe yule mwenye Fuso.

Jamani Manase bado yupo hapo Mpwapwa?
 
Kumbe barabara haijajengwa!

Yaani tangu 2014 Mh.zabena muhita mhaji akiwa bungeni alipomuuliza kuhusu ujenzi wa barabara hii Mh.JPM,Hadi leo holaaaa

Amakweli kidumu chama cha mapinduzi

Umefanya vema kumkumbusha, mkuu. Miaka 30 ya Lubeleje haijaleta kitu lakini hawa hawa ndio huambiwa “upinzani unachelewesha maendeleo”. Sijui haya yamechelewa kwa sababu gani.

Nami namwambia hiyo barabara ikae tu, sio muhimu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom