Umma watahadharishwa kuhusu kusambaa kwa Katiba feki ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umma watahadharishwa kuhusu kusambaa kwa Katiba feki ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Jul 13, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Na Muhibu Said
  13th July 2010

  Hii ni dalili kuwa kuna upungufu wa nakala za Katiba ya nchi na wananchi wana haja ya kujua katiba inasema nini hasa, ndio maana kumekuwa na soko la katiba kiasi cha watu kuchapisha katiba hiyo 'fake'. Ili kuondokana na tatizo la kuwa na katiba amabzao sio halisi, serikali haina busi kuhakikisha kuwa katiba inapatikana kwa urahisi na kusomeka na wananchi wote. Ni juzi tu nilikuwa natafuta nakala ya katiba nikashauriwa niende kwenye tovuti ya bunge, lakini sikuona kiunganishi kinachohusika. Kuna haja ya wananchi kuijua katiba vizuri na kuijadili.

  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imesema kuna nakala feki za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Toleo la mwaka 2008 katika lugha ya Kiswahili) zilizochapishwa, kusambazwa na kuuzwa na kuwataka wanaofanya hivyo kusitisha shughuli hiyo mara moja, kwa vile ni ukiukwaji wa sheria.

  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisema nakala hizo, ambazo zinaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi zina makosa mbalimbali kiufundi.
  Alisema Toleo halisi la Katiba iliyorekebishwa na iliyo katika lugha ya Kiswahili ni la mwaka 2005 na siyo la mwaka 2008 kama ilivyoonyeshwa kwenye nakala potofu, pia hazina idhini ya uchapishaji kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na jina la mchapishaji.

  Masaju alisema katika nakala hizo, imeongezeka Ibara ndogo ya (3) katika Ibara ya 139, ambayo haipaswi kuwapo. Alisema rangi ya nakala na muonekano wa nakala hizo kwa nje ni tofauti na nakala halisi, kwani nakala halisi ina rangi ya zambarau iliyokolea wakati nakala isiyo rasmi ina rangi ya damu ya mzee (maroon) na kwamba, nembo ya taifa iliyopo katika nakala hizo ni tofauti na nembo halisi ya taifa.


  Alifafanua kwamba nembo iliyowekwa haina alama ya mlima Kilimanjaro, maua ya nembo yamekanyagwa na bibi na bwana badala ya kuwa pembeni yao na kwamba nguo walizovaa bibi na bwana ni tofauti na mavazi yao katika nembo halisi ya taifa.
  Masaju alisema mbali na kasoro zilizobainika kwa nje, ndani katika mpangilio wa ibara, kuna tofauti kuhusu mpangilio wa maelezo ya pembeni na kwamba, katika nakala hizo, maelezo hayo yako upande wa kulia tofauti na nakala halisi, ambapo maelezo hayo yako upande wa kushoto.

  Kutokana na hali hiyo, aliutaka umma kufahamu kuwa nakala hizo ni batili, hazitambuliki kisheria na ni potofu na kuwataka kutonunua, kupokea au kuzitumia. Pia, amewataka wanaozichapisha, kusambaza na kuziuza au kuzigawa, kusitisha shughuli hiyo mara moja, kwa vile ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

  "Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea kufuatilia na kuchunguza suala hili ili kubaini chanzo chake na hatimaye hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika wote," alisema Masaju.

  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...