-umiza moyo..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

-umiza moyo.....

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Sanda Matuta, Jun 19, 2009.

 1. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Namshukuru mwenyezi,sifa na takbira.
  Labana afanya kazi,akifata yake dira.
  Humpa naye mridhi,jazha nema ongezea.
  Humnyima kwa uwazi,yule anaye mkusudia.
  Huyu ndio Mwenyezi,Mungu tunaye msujudia.

  Mbingu yake ardhi,kwa ajabu ameumba.
  Adam wake mwenzi,Hawa kumuwekea.
  Mwanamke akamuenzi,sifa zake jaalia.
  Kwenye zake tenzi,vitabuni utakuta.
  Quraani ina mengi,yale kwenye Bibilia

  Hili Swali watenzi,majibu nina yatakaa.
  Moyo kitu thamani,nani anza umizaa?
  Turudi kule bustanini,Maisha yalipoanza
  Adam kwenda porini,mwanamke aka data
  Kam-ruhusu shetani,chokochoko zake leta.

  Amwambia,”hakutamani,ndio maana anatoka.
  Usikute ana mpenzi.huko anako kwenda.
  Anafanya kama kazi,aliyoka kataza Rabuka.
  Wewe ana kuhini,huku yeye ajirusha
  Haya mengine mengi,kichwani aka mjaza.

  Aka-umia moyoni,simanzi zika mjaa.
  Moyo wake maskini,ndio ukawa wa kwanza.
  Hasira ndio kiini,uchamungu kumtoka
  Kulipiza aka-tamani,moyo Adamu kuvunja
  Shetani haku muhini,kumpa tunda kumega.

  Moyo kauumiza nani,shetani au lasulallah
  Hawa akapata poni,mumewe akamtaka
  Adamu yu mafunzoni,akamuhasi Rabuka.
  Kwa matendo ya chumbani,wakalivunja agano
  Malenga mnipe yakini,nani kauumiza moyo?
   
  Last edited: Jun 19, 2009
 2. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Mkulu SM

  kulikoni,mbona sintofahamu kila mahara??
   
 3. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimetunga kwa kubuni,beti zangu nimeweka.
  Malenga mlio pwani,bara hata Amerika
  Nina itaka yakini,majibu yenu kupata.
  Ya niingie akilini,mtima wangu tulizaa
  Binaadamu na Shetani,nani moyo kauumizaa?
   
 4. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  wakulu kweli hakuna majibu ya Hili?????
   
 5. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  unakaribia mwaka sasa,hamna wakujibu,Mkuu sanda jibu mwenyewe lete vituz.........
   
 6. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Umelipenda Eenh.........!!!?????jaribu basi kidogo na wewe,mie nikiandika bado nitazidisha ugumu,liache hivyo.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  aisee mbona sikuwa nimeiona.. nitapata muda kujibu!
   
 8. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nasunasubiri jibu
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Moyo uloumizwa,hakika wote twabuni,
  Maana tunda kumeza, mwishowe ni huzuni
  Hili lilishasemezwa, na mola kule bustanini
  Jibulo kama waweza,huna budi kubaini,

  Adam kuumbwa kwanza, Eva akaja badae
  Kisa Adamu kuwaza, akaeje mwenyewe?
  Rabuka akampooza,kwa kumpa mwenziwe
  Hapo ikamwisha waza, pasipo mfanowe

  Haikuishia hapo, wawili mle bustanini
  Mola akawapa onyo,mlemle bustanini
  Wakalielewa onyo,japo wasiweke manani
  Ikajakuwa songo, walipokosa umakini

  Joka a.k.a Shetani , saa ngapi asiwarubuni
  Na vile walivyodhani, wamo daima rahani
  Kumbe sivyo asilani, pembeni kuna kisirani
  Ukawa ndio ushindani , joka akaingia nafsini

  Na kama ilivyo ada, joka kiumbe hatari
  Adam kutokuwaza , kuzingatia tahadhari
  Akamwacha mamie Eva, asemeshwe na kikari
  Utashangaa vipi aliweza,ilhali Adam yu askari

  Tunda lilipoangazwa, hakika likavutia
  Eva hamu kajazwa , Adam akampatia
  Adam akapumbazwa, Tunda kalumangatia
  Utasemaje kaumizwa, ilhali alijitakia?
   
 10. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  WOS,
  i salute!!!!!
  wewe mkali mno......................!!!!
   
Loading...