'Umim' unaisigina EAC alfajiri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Umim' unaisigina EAC alfajiri!

Discussion in 'International Forum' started by The Quonquerer, Jun 3, 2010.

 1. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na Prudence Karugendo [/FONT]​

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]LIPO wazo la kuunda Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki (EAC). Wazo hilo, kama siyo la kusadikika, linaenda mbele zaidi kutupa matarajio ya kuwa na nchi moja ya Afrika Mashariki hapo baadaye. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Hili ni wazo lisilo na tofauti na lile lililoshikiwa bango na kiongozi wa kudumu wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, la kutaka kuwa na nchi moja ya Afrika. Wakati Gaddafi akiota nchi moja ya Afrika kila alalapo, rafiki yake Yoweli Kaguta Museveni wa Uganda naye amekuwa akiota nchi moja ya Afrika Mashariki kila alalapo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na hawa viongozi marafiki wanalo jambo moja linalowafanya wasifanane tu bali kuonekana mapacha katika nyanja ya utawala, nalo ni kupenda kuwa watawala wa kudumu. Zamani watawala wa aina hiyo walikuwa wakijitawaza kuwa watawala wa maisha, ila kwa sasa neno hilo ni kama wanalionea aibu na kuamua kutumia njia nyingine ambayo bado inawahakikishia utawala wa kudumu (wa maisha). Wanajifanya wa kudumu badala ya wa maisha, kitu kinabaki kilekile. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki naona watu wanaliangalia kwa mitizamo tofauti tofauti. Wapo wenye mawazo kuwa shirikisho ambalo baadaye linaweza kugeuka kuwa nchi moja manufaa yake ni kuwa na nchi moja kubwa itakayokuwa imara kiuchumi, pengine kuwa na nguvu kubwa za kijeshi na kadhalika. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Lakini kwa upande wangu nayakataa mawazo ya aina hiyo. Nayakataa katika misingi ya kwamba sisi watu wa eneo hili bado tuna roho dhaifu, roho zetu bado zinatawaliwa na umimi, roho hizi kamwe hazituwezeshi kujenga shirikisho. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Tusiangalie penye shirikisho tukadhani hiyo ni neema inayoweza kutokea kila pahala kama inyeshavyo mvua. Shirikisho linajengeka katika mioyo ya watu waliojitoa na kuusahau umimi na kuliwaza shirikisho tu badala yake. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Shirikisho linahitaji watu wenye roho za shirikisho, watu wanaowaza kishirikisho, kufikiria kishirikisho, kuamua kishirikisho. Watu wenye mtizamo wa sisi Afrika Mashariki, na wala siyo sisi Watanzania, sisi Wakenya au sisi Waganda na kadhalika. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Tutakapokuwa tumefikia uungwana wa aina hiyo ndipo nitakapoamini kuwa suala la Shirikisho la Afrika Mashariki linaweza likaongelewa. Lakini kwa jinsi mambo yalivyo kwa sasa bado naona ni kama ndoto za Alinacha zinazotufanya tuwe na mawazo haya ya kusadikika. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Udhaifu huo tulio nao ndio uliokuwa unanisukuma kulikataa shirikisho la nchi za Afrika Mashariki, udhaifu wa kutamani kitu kimoja wakati hatuna mawazo ya umoja. Ni wazi kwamba hatuna mawazo ya umoja kuanzia kwenye nchi zetu hizi moja moja, sasa mawazo ya kujenga umoja wa shirikisho tutayatoa wapi? [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Maana watu wenye mawazo ya umoja kamwe hawawezi kung’ang’ania madaraka iwe ni kwa mtu mmoja mmoja au chama. Ung’ang’anizi wa madaraka katika hizi nchi zetu zinazojigamba kuunda shirikisho unatoa picha gani? [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Hebu tuangalie yanayoendelea katika nchi zetu hizi. Kwa upande wa Tanzania kuna Chama cha Mapinduzi chenye tamaa ya kutawala milele, nchini Rwanda kuna Kagame mwenye tamaa ya kutawala milele, Uganda kuna Museveni ambaye naye anatamani kutawala milele. Kenya kuna Kibaki anayeshindwa na kukatalia Ikulu. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Huo wote ni udhaifu unaoletwa na umimi. Na haijawahi kutokea udhaifu na udhaifu ukaunganishwa kikapatikana kitu kilicho imara. Sanasana kitakachopatikana ni udhaifu mkubwa zaidi. Na kama ni hivyo kwa nini tuungane kuutafuta udhaifu mkubwa zaidi? [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Nadhani kinachotushawishi, tulio wengi, kulitamani shirikisho na baadaye kuwaza nchi moja ni mafanikio ya nchi zilizoungana kama vile Amerika (USA). Ila tunasahau kuwa katika wengi kuna mengi, wapo vilevile wanaolitamani shirikisho kwa maslahi yao yaliyo tofauti kabisa na maslahi ya wananchi wa eneo hili. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Wapo wanaotamani kutawala eneo kubwa ambalo ndani yake kuna mlima mkubwa kuliko yote Afrika, Kilimanjaro, ziwa kubwa kuliko yote Afrika, Victoria, na kadhalika. Sidhani kama hayo ndiyo mambo tunayoyatamani wananchi wa eneo hili katika shirikisho letu au katika nchi yetu, tunatamani zaidi ya hapo. Kwa ufupi tunatamani kuungana kwetu kutuboreshee maisha yetu. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kikwazo kinachojitokeza ni kwamba tunakosa uungwana wa kuliangalia shirikisho katika mtizamo wenye kuleta manufaa kwa watu wote wa Afrika Mashariki, na badala yake tunatawaliwa na uchu wa kila mmoja kuliangalia kutokea kwenye nchi yake na si ajabu hata kwenye mkoa wake akizingatia ni namna gani nchi yake au mkoa wake utakavyonufaika na shirikisho hilo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Tatizo hilo ndilo lililomfanya hata Waziri wa Kenya anayeshughulikia Uhusiano wa Afrika Mashariki, Amason Kingi, kuhoji usahihi wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kubaki Arusha. Pamoja na hoja alizozitoa majuzi, kinachojitokeza zaidi ni yeye kutaka kuvutia upande wa nchi yake kwa kuona kuwa makao makuu kuendelea kubaki Arusha yanainufaisha zaidi Tanzania. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Yeye anaona makao makuu ni bora yakawa Nairobi, sehemu ambayo umbali wake na Arusha ni wa pua na mdomo. Kwa hiyo Kingi hana mawazo ya Afrika Mashariki kichwani mwake, ila kilichomo ni Kenya yake. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Rwanda nayo ikaja na madai yake ya kwamba Arusha ni pembeni mno. Kwa kujibu hoja hizo Waziri anayeshughulikia Uhusiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Diodorus Kamala, naye akaonyesha udhaifu ule ule wa umimi. Yeye alionyesha kwamba iliyochokozwa ni Tanzania kana kwamba Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanapaswa kuwa mali ya Tanzania. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Maana alivyoongea si kama mtu wa Afrika Mashariki bali zaidi kama Mtanzania. Hakuonyesha kutetea Makao Makuu yale kubaki Arusha kwa faida ya watu wa Afrika Mashariki, ila alionyesha wazi kutetea faida ya Tanzania. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Sasa na tuangalie mvurugano huo, Wakenya wanasema Makao Makuu bora yawe Nairobi, Watanzania wanacharuka hawataki mjadala wowote kuhusu hilo. Wanadai Makao Makuu ni Arusha, basi. Eti mkataba unasema hivyo! Sijui huo ni mkataba wa kwenye Biblia! [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Wengine wana mawazo ya kwamba kwa vile Rwanda na Burundi ni washirika wapya katika jumuiya hiyo basi hawapaswi kuwa na kauli. Yote hiyo inachangiwa na umimi, kitu ambacho ni hasidi mkubwa wa ushirika au jumuiya, ambacho hakiwezi kutuacha tukafanikisha kitu kama hiki tunachojaribu kukiunda. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Inabidi tuelewe kuwa kama kumeonekana umuhimu wa kuwashirikisha Rwanda na Burundi vilevile ni lazima upo umuhimu wa kusikiliza kauli zao. Ni ujinga kusema kwamba wao ni wageni hivyo wasitoe kauli hata kama ni ya manufaa. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Pia wapo wenye mawazo ya kwamba ikiwezekana Rwanda na Burundi wanaweza wakafutwa tukabaki kama tulivyokuwa mwanzo, Tanzania, Uganda na Kenya. Ila tusisahau kwamba mawazo ya aina hiyo yanatuelekeza kwa Charles Njonjo, ukishaanza dhambi ya kufuta hutaacha mpaka uhakikishe unabaki peke yako. Kwa hiyo wenye mawazo ya kuzifuta Rwanda na Burundi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki wajue ni kama wameishaifuta jumuiya yenyewe. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kama kweli tuna dhamira ya kuwa na shirikisho inabidi tujifunze kufanya mambo yetu kishirikisho kuanzia wakati huu. Maamuzi yetu yawe ya kishirikisho, mitizamo yetu iwe ya kishirikisho na fikira zetu ziwe za kishirikisho. Mfano mkataba unaosema kwamba makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakuwa Arusha haujatoka kwa Mungu, kwa maana hiyo siyo haramu kuuongelea. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Pengine wakati unasainiwa Rwanda na Burundi walikuwa hawajaonyesha nia yao ya kujiunga. Hivyo kujiunga kwao ni lazima kuonyeshe kuimarika kwa Jumuiya, na si kuimarika kwa kuongeza eneo la Jumuiya na idadi ya watu tu, bali pia mawazo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Sasa kwa nini mawazo yao ya kushauri ni wapi wanaona makao makuu yangefaa yawepo yapuuzwe kwa kigezo cha kwamba wao ni wageni? Kama wageni hawapaswi kuchangia lolote tumewakaribisha wa nini kwenye jumuiya yetu? [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Nikizungumza kama mtu anayeitakia heri Jumuiya ya Afrika Mashariki, ningeulizwa swali ni wapi naona panafaa kuwa makao makuu ya jumuiya hii, bila kuuma maneno, jibu langu lingekuwa Kampala. Si Arusha, Nairobi wala kwingineko. Hiyo ni kutokana na ninavyoijua jiografia ya eneo letu. Kampala ndipo sehemu inayofikika kwa urahisi kuliko sehemu zote kutokea pande zote za jumuiya hii. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Nakizungumzia kwa kutumia njia zote za usafiri, barabara, reli, anga na hata usafiri wa majini. Kwa hiyo ni rahisi kwa kila mwanajumuiya kuyafikia makao makuu yake kiurahisi kuliko yalivyo sasa mjini Arusha. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Wanaosema kwamba Arusha kunafaa inabidi watueleze sababu nzuri ya mtizamo wao, kulingana na mahitaji ya jumuiya, iliyo tofauti na muwamba ngoma, inayoweza kumfanya mtu wa Burundi kupaona Arusha ni sehemu sahihi kwake kuliko Kampala kwa mfano. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Suala la amani kwa upande wa Arusha hilo halimo tena kwenye ajenda tukitilia maanani hali halisi ya usalama ilivyo katika mji huo ambao vivutio vyake vimeugeuza kuwa kitovu cha uharamia katika eneo hili la Afrika Mashariki. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Najua kuna Watanzania wenzangu watakaonishangaa, lakini hapa mimi naongea kama mtu wa Afrika Mashariki nikijaribu kuuweka bayana ukweli. Kuupuuza ukweli huo itakuwa ni kuufanya mchakato mzima unaoendelea uonekane kama mchezo wa kuigiza au mpango wa kutegana ili kufanyiana hadaa. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na hicho ni kitu ambacho hakifai kwa watu ambao tayari wanajiona ni waungwana. Ni aibu kushindwa kuweka mambo katika mpangilio sahihi wakati huu ambao ni zaidi ya miaka 200 tangu wenzetu wafanye kitu kama kile kule Marekani. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]prudencekarugendo@yahoo.com [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]0784989512[/FONT]
   
 2. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hebu tuangalie yanayoendelea katika nchi zetu hizi. Kwa upande wa Tanzania kuna Chama cha Mapinduzi chenye tamaa ya kutawala milele, nchini Rwanda kuna Kagame mwenye tamaa ya kutawala milele, Uganda kuna Museveni ambaye naye anatamani kutawala milele. Kenya kuna Kibaki anayeshindwa na kukatalia Ikulu.  My take: Ndiyo maana hii kitu haifai. Kuhusu makao makuu, kokote hakufai! Si Kampala wala wapi. Wadau, kuna makala ya "Mnafungua milango tutoke au waingie" ya leo, naomba kama kuna mtu anaweza kui-post aimwage..it's a cool piece. Kama hii ilijadiliwa nyuma, my apologies.. i wasn't even aware, maana sijaona tarehe ya chapisho lake.

  Even more related:

  Watanzania tusiachie ardhi EAC

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]NIMESOMA kwa makini, Maoni ya Mhariri wa gazeti dada la Rai – Mtanzania Jumapili la Aprili 19 mwaka huu juu ya ushirikiano mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wenye nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. [/FONT]​

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kimsingi Mhariri ametuonya Watanzania na viongozi wake kuwa macho na nchi hizi nyingine juu ya njama za kutaka kupora ardhi ya Tanzania. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Ni ukweli usiopingia kuwa nchi hizi hazikuingia katika umoja huu kwa nia njema, bali kuna ajenda ya siri ambayo ni kutaka kupora utajiri wa Tanzania, hasa ardhi. Ushahidi wa haya ni kauli mbalimbali zinazotolewa na viongozi na hata wananchi wa nchi hizo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Ni dhahiri wenzetu hawa walipoona wamekosa kutimiza malengo yao kwa haraka, wanaibembeleza Tanzania ikubaliane na baadhi ya masuala, kama hili nyeti la ardhi liwe ni sehemu ya mkataba wa Jumuiya, halafu pawapo utaratibu wa mkazi yeyote wa kutoka nchi hizi akikaa kwa miaka isiyopungua mitano katika nchi mwanachama eti ni tiketi ya kuwa pia wa nchi husika. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Ni dhahiri vipengele vibovu kama hivi vikikubaliwa, hasa na Serikali ya Tanzania, tutakaoumia ni sisi Watanzania, kwani umati wa wananchi kutoka nchi hizi utamiminika Tanzania kutokana na jiografia na utulivu wake. Si rahisi Mtanzania kupenda sana kwenda kuishi katika nchi hizi zenye machafuko na mifumo isiyoeleweka vizuri ya utawala kama Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Isitoshe, hawa wenzetu wana chembe chembe za ukabila na ubinafsi sasa tuwe macho wasije wakapanda mbegu hizo kwa wananchi wetu wanaokaa kidugu kwa amani na utulivi kwa miaka mingi. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Ni ukweli usiopingika kwamba hapa kwetu Tanzania, pamoja na matatizo ya hapa na pale bado Watanzania ni wamoja na wanapendwa tofauti na wenzetu. Huko Rwanda hakuna demokrasia inayoeleweka, hadi leto Wahutu na Watutsi hawaaminiani, Burundi ni hivyo hivyo, huko Uganda kuna rais ‘wa maisha’ na Kenya tumeona uchaguzi wa 2007 ulivyovurugwa kwa maslahi ya watu wachache. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Leo hawa ndugu zetu wanapotaka tuishi kama kitu kimoja ni kwa kanuni ipi? Watanzania na serikali yetu tunastahili kujipongeza kwa kuungana dhidi ya njama hizi uchwara za hawa ndugu zetu za kutaka kutengeneza kila kinachoitwa Himaya ya Bahima katika ukanda huu. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Cha ajabu ni nini kwa Tanzania kukataa ardhi yake kuwa sehemu ya mali za pamoja katika EAC? Mbona hata katika Umoja wa Ulaya (EU) kuna mataifa kama Uingereza yalikataa kuwa na sarafu zao? [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kama umoja wenyewe wa EAC ni huu wa kuviziana na haueleweki basi ni bora uvunjike na kila nchi iwe kivyake kama zamani, tukishirikiana katika baadhi ya mambo huku tukiunganishwa na Umoja wa Afrika (AU) nzima. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Hongera sana Serikali ya Tanzania, Watanzania wenzangu na Mhariri wa Mtanzania kwa ushirikiano dhidi ya njama za hawa wenzetu. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kindamba Kengeja, [/FONT]
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Katibu wa UVCCM, [/FONT]
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Msakuzi Kaskazini, [/FONT]
  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]0753034570.[/FONT]
   
 3. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  kelele ya chura haimzuii ngombe kunywa maji, isitoshe, huenda yule chura akanywewa pamoja na hayo maji.. tafakati hayo
   
 4. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  R out of ur mind? Kama Kiswahili hujui, andika Kikamba au Kigikuyu or any other Kenyan language! Inawezekana vipi chura kunywewa na maji????? ebo! and what's ngombe?
   
 5. S

  SpinDoctor Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kanyabwoya, achana na huyu Smatta.....tokea akimbilie Tanzania mwaka 2007 hataki kurudi kwao. Kwahiyo atabwabwaja sana hapa.... Kwani hujui karibia asimilia 90% ya ardhi ya Kenya inamilikiwa na the Kenyattas, Moi's....na ma-settlers?
   
 6. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 405
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Kwa ukweli ni uroho wa madaraka umewatawala viongozi wetu, kila mmoja ana fikra ya kuwa raisi wa hiyo nchi kufikirika, maana wote watakuwa washamaliza terms zao na hapo watautaka uraisi mpya, ili muradi waendelee kuitwa maraisi
   
 7. W

  WaMzizima Senior Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani ni lazima kuwa na Rais tunaweza kuwa na 'council of presidents', kama sikosei Switzerland wanatumia huo mtindo na hiyo bodi yao ina watu 12. Au tunaweza kuwa na rotating presidency ambapo kila nchi itapata miaka yake minne ya kuongoza au kuwa na waziri mkuu ambaye ni lazima aongoze coliation govt ambayo itakuwa na vyama toka nchi zote tano.

  Kuna namna mbalimbali za kuwa na serikali imara hivo mi sioni kama hawa kina Museveni ni tatizo, cha msingi ni sisi watu wa Afrika Mashariki kuwa tayari kuungana. Hii common Market ni good start kisha tuunganishe fedha zetu na kuwa na sarafu moja tuuite 'AFRO' kisha baada ya hapa kuwe na mchakato wa kuziunganisha hizi nchi kisiasa. Ni lazima kuwa na kura ya maoni na kupata baraka za wananchi wa nchi zote kwanza.
   
 8. K

  Koba JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Another post from ant EAC know nothing Kanyabonya,anajifanya expert wa EA politics kumbe ushuzi mtupu,hatuhitaji hizi backward thinking,your likes mnaturudisha nyuma and we wont allow that,EA means more opportunity for all members,spreading unfounded fear doesnt work bro...kila siku land land land lakini hata huna idea how our lands law works,ooooh Kenyans will make Tanzania a dump market lakini huna idea sasa TZ wana export Kenya more than they imports,practically ungekuwa businessman,student or any professional may be you could appreciate EA....long live EA!
   
 9. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa na hapa lazima serikali ifanye kazi yake kuweka mambo sawa ule mji sio wa amani tena kama ilivyofikiriwa

  Ni hoja yenye maana kwao lakini ni ya ajabu sana kutoka kwa wakati huu, ilikuwa na wakati wake na umeshapita

  Ni hoja dhaifu sana na inaleta shaka kubwa uko mbeleni kuwa litakuwa shirikisho gani hili
   
 10. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Bado mashaka tele kuhusu maisha ya jumuiya hii kwani wenzetu wamekuwa na magutu mengi mno ki fikra na kuona kula kitu lazima kiwe na manufaa kwa upande wao Kiuchumia kwa namna moja au nyingine:  Sponsorship Packages [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Your sponsorship can be made by transfer to the East African Community account set out hereunder;
  Account Name: East African Community
  Bank Name: Kenya Commercial Bank, Arusha Branch
  Account No: 020 402 003206
  Contact Person: Frederick Owiti
  Email: fowiti@eachq.org

  Tel: +255-27-2504253/8
  http://www.eacinvestmentconference.com/3rd/sponsorship.html

  Vs   
 11. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na ule msimamo wako wa kutetea ushoga yaani ufiraji bado unaendelea nao? Na sababu gani zinakufanya utetee hivyo vitendo. Mimi nina wasi wasi sana na akili yako kabla kujibu hoja zako. Mtanzania gani anatetea kuhalalishwa kwa ufiraji? Wewe siyo mtanzania! I don't take you seriously!
   
 12. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Stop diverting the thread, what Koba has said is the plain truth, you hate something you don't understand, take time and go to the EAC website and read what the community is all about and what it has to offer, maybe you'll learn one or two things about this community. Its for all of us, not just the politicians and the corrupt civil servants, or Kenyans (as you tend to think). Open your mind and stop being so conservative, its 2010 for heavens sake, the fear of the unknown will never benefit you as a person and your country as a whole, it will only drag you down. people are dying to join or form communities, while you stay here with last decades arguments about people eyeing your land and minerals, life is beyond this, Its not always about Tanzania or Kenya for that matter, its about progress of our nations as a whole. This borders will always separate us, but dont let them create hate between us because you weren't there when the white man was demacating this lands and creating borders for themselves, so love your country but dont let that love blind you from the fact that we were once one, and we are stiving to get back to where we were long time ago, for our benefits. And if you refuse, we will probably drag you with us.

  Ijumaa kareem
   
Loading...