Umilikishaji wa hati kuwa inua wananchi wa Temeke kiuchumi

Apr 9, 2022
66
32
Na. Mwandishi wetu, Dar

Kamishina Msaidizi wa ardhi kanda ya Dar es Salaam Bw. Idrisa Kayera amesema serikali imesisitza kuwa lengo kuu la umilikishaji hati miliki za ardhi litafanya kila kitu kuwa na uhakika wa usalama wa umiliki wa ardhi na hivyo kuwainua wananchi kiuchumi Kwa kuwa hati miliki inamsaidia mwananchi kuaminiwa na taasisi za fedha na kukopesheka.View attachment 2330818

Hayo ameyasema kwa wakazi wa Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam ambao wamekua wakifurahia zoezi la Urasimishaji Ardhi kwa kuwa limewawezesha kila mwananchi kutambuliwa kwa kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria na kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.

Akizungumza kuhusu mazoezi ya namna hiyo ya urasimishaji wa ardhi, Kayera amesema kuwa jumla ya wananchi 87,842 wametambuliwa.

Bw. Kayera aliendesha zoezi hilo la urasimishaji mbele ya wakazi hao kwenye mkutano wa wazi uliofanyika Kata ya Mbagala Manispaa ya Temeke.

"Hivi karibuni tuliweza, kuendeleza zoezi la urasimishaji, sasa limeendelea kufanyika zaidi tofauti na miaka ya nyuma kwani hapo awali lilikuwa kero kwa wananchi" amesema Bw. Kayera.

Amesema wamekuwa wakiwafuta wananchi na kufanya zoezi hilo kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali na kuepusha migogoro.

Kayera amesema ni moja ya zoezi bora kabisa lililofanyika machi mwaka huu ambapo katika siku hiyo aliweza kuwapatia hatimiliki za ardhi kwa wakazi 32 huku wengine 310 wakapokea kuanzia l jumatatu ya Mach 28 katika mlolongo huo ambapo hati zote zilikuwa tayari .

Katika wakati huo aliendelea kufafanua kuwa kuna jumla ya makampuni 24 yanayofanya urasimishaji katika kata 14 za manispaa ya Temeke ambapo ina mitaa 46 ambayo tayari imefikiwa.

Amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo, jumla ya viwanja 8,685 vimepimwa na kuidhinishwa na Wizara ya Ardhi, huku viwanja 24,714 vimewekewa (Beacon) na viwanja 12,865 vimewasilishwa wizarani.

Katika wakati huo Afisa Mipango Wilaya ya Temeke Veronica Igoko aliyemwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, aliwaomba wajumbe wanyumba 50 watoe ushirikiano wa kutosha katika zoezi la Anuani za Makazi .

Amsesema urasimishaji wa makazi unaendelea na ifikapo Agusti 23, 2022 kutakuwa na zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa.

"Nawasihi sana wananchi waendelee kuchangia gharama za upimaji ili muweza kupata hati miliki , hii itarahisisha wakandarasi kufanya wajibu wao kwa urahisi na kuwawezesha wataalam wetu kurahisisha zoezi la ufuatiliaji na uwajibikaji na hatimaye hati ziendelee kutolewa."

Mwenyekiti wa Kibonde Maji kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema zoezi hilo limefanyika kwa weledi mkubwa na kuwa limesaidia wananchi.

Mkazi wa Yombo Vituka Bi. Pelepetua John Kibaja ni miongoni mwa wakazi waliopewa hati, amesema kuwa zoezi la kupata hatimiliki yake lilikua rahisi kwani alifuatilia ndani ya mwezi mmoja na kufanikiwa.

"Napenda kumshukuru Mungu kwa kupata hati hii nilitegemea ningekutana na changamoto nyingi, lakini haikua hivyo nimefanikiwa kupata kwa muda mfupi," amesema Bi. Pelepetua. Mkazi wa Maji Matitu Kata ya Muanzini Herieth Rugemalira amefurahia kupata hatimiliki yake ya ardhi .

"Nafuraha kwani niwanaume wachache wanaoweka majina ya wakezao katika utambuzi huu wa hati, ila mimi na mmewangu tulifuatilia pamoja na tumepata hati yetu inayotuonesha tunamiliki kiwanja chetu wote," amesema Herieth.

Katika zoezi hilo kata za Chamanzi, Toangoma, Makangarawe pamoja na Mbagala Kuu, Mianzini, harambe, Buza, Kijichi pamoja na kata zingine za Yombo Vituka na Kibondeni
 
Back
Top Bottom