Umiliki wa TBC,

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa kuwa shirika la utangazaji la taifa (TBC) linabadilisha mfumo wa Matangazo kutoka Analog kwenda Digitali, Hapohapo inasemekana wanaohusika kubadili mfumo huo ni kampuni ya Star times ndio maana matangazo yao yamekuwa mengi sana kwenye TBC.

Maswali:
1.
Hivi hii TBC inamilikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 au hawa Star times wana hisa humo? au star times inataka kutumia shirika hili la serikali kuuza ving'amuzi vyake?

2.Je mfumo wa digitali ukifanikiwa kwa mgongo wa kampuni ya Star times hatuoni kwamba TBC italazimika kuinyenyekea kampuni hii ili matangazo yake yaende hewani?

Itakuwa kama TTCL na airtel. zilifungishwa ndoa halafu jamaa wavuna weeee! walipoona TTCL kwishna .... wakatoa taraka!!
anyhow ni bora TBC ife maana tangu Tido Mhando aondoke imekuwa total disaster!! vipindi vinaboa, vemeegemea upande mmoja!!!

Si shangai kwani tulikwisha uzwa siku nyingi na magamba hakuna tulichobakiza.

si shangai kwani tulikwisha uzwa siku nyingi na magamba hakuna tulichobakiza.
siyo ustaarabu kuhusisha kila jambo baya na ccm, huo ni uvivu wa kufikiri na ujinga uliopitiliza katika upuuzi wa mawazo ya mwanadamu

Nani ahusishwe wakati wao ndo wameshika dola na ile ni mali ya umma ww vipi??????? yaonekana huelewi nchi inaendeshwa vipi

dah, pamoja na uzalendo nilionao kweli i wont care hata ikifanywaje ile station hata haioperate kitaifa tena iko bias sana, iko tu kwa maslahi ya wachache na si ya umma wote

Tido katika hili ndie anayepaswa kulaumiwa. Ameiingiza TBC mkenge maana alisaini mkataba kabla hata ya kwenda baraza la mawaziri na hadi sasa seriikali inahaha kujinasua toka Star Time maana imeshikwa pabaya katika hili. Tusubiri tuone mwisho wake

Tido mtamuonea bure kwani hakuna waziri mwenye dhamana na hili? Hao mawaziri wa magamba ndo wakulaumiwa

Upupu mwingine yaani mnaboa kupita kiasi.
TBC is whole owned by Government of Tanzania.
StarTimes is co shared by another company and TBC.
Sasa hapo TBC iko mikononi mwa nani?

Kwa taarifa yenu digital broadcaster will only be three nationalwides i.e Startime, Agape TV and another one coming soon the rest will be only making programes.
Sijaona tatizo hata moja! The only way you can convince learned people is if there is broadcasting service contrat that may be shord btn TBC and Startimes which u haven't say anything here.
Kama hatuna point tunyamaze wakuu.

siyo ustaarabu kuhusisha kila jambo baya na ccm, huo ni uvivu wa kufikiri na ujinga uliopitiliza katika upuuzi wa mawazo ya mwanadamu

CCM ndiyo inayoongoza serikali na serikali ndiyo inayosimamia vyombo vilivyo chini yake. Kunguni ndani ya nyumba ya mtu utawahusisha na nani kama siyo mwenye nyumba?

Upupu mwingine yaani mnaboa kupita kiasi.
TBC is whole owned by Government of Tanzania.
StarTimes is co shared by another company and TBC.
Sasa hapo TBC iko mikononi mwa nani?

Kwa taarifa yenu digital broadcaster will only be three nationalwides i.e Startime, Agape TV and another one coming soon the rest will be only making programes.
Sijaona tatizo hata moja! The only way you can convince learned people is if there is broadcasting service contrat that may be shord btn TBC and Startimes which u haven't say anything here.
Kama hatuna point tunyamaze wakuu.

Mh. yaliyotolewa hapo ni maswali, what we need to know ni facts kuhusu umiliki wa TBC, Your comment is too emotional kiasi haieleweki kama unachokisema comes from your mind or is just coming from your mouth, Umejibu kishabiki zaidi. Tujaribu kutoa hoja zenye mashiko.

Wewe kwa mawazo yako unataka nani ahusishwe na mambo mabaya ambayo serikali yetu pendwa imetusababishia sisi watanzania ama mmoja mmoja au kwa ujumla wetu? Mazuri kama yapo mbona yote yanahusishwa na ccm hata yale ya TANU na ASP!

siyo ustaarabu kuhusisha kila jambo baya na ccm, huo ni uvivu wa kufikiri na ujinga uliopitiliza katika upuuzi wa mawazo ya mwanadamu

Tuwe wakweli serikali hii na chama chake cha Magamba ndio chanzo cha kila baya humu nchini.

siyo ustaarabu kuhusisha kila jambo baya na ccm, huo ni uvivu wa kufikiri na ujinga uliopitiliza katika upuuzi wa mawazo ya mwanadamu

Sasa wataka watu wahusishe TBC na nani

kama si CCM? Wewe ambae huna ujinga uliopitiliza mbona haujatueleza ihusishwe na nani? Umebaki kutukana tu!

Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa kuwa shirika la utangazaji la taifa (TBC) linabadilisha mfumo wa Matangazo kutoka Analog kwenda Digitali, Hapohapo inasemekana wanaohusika kubadili mfumo huo ni kampuni ya Star times ndio maana matangazo yao yamekuwa mengi sana kwenye TBC.

Maswali:
1.
Hivi hii TBC inamilikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 au hawa Star times wana hisa humo? au star times inataka kutumia shirika hili la serikali kuuza ving'amuzi vyake?

2.Je mfumo wa digitali ukifanikiwa kwa mgongo wa kampuni ya Star times hatuoni kwamba TBC italazimika kuinyenyekea kampuni hii ili matangazo yake yaende hewani?

Hujafanya utafiti unakurupuka tu kushutumu na kutuhumu. Unajuaje labda wana mkataba maalum wa kufanya kazi hiyo kwa malipo tofauti na hivyo unavyofikiria? Kwani kuuza ving'amuzi si ni agency ambayo ina makubaliano maalum?

Jamani tuume na kupuliza! lakini ukweli siyo huo
Iko hivi
Star Media ya Nje Imeungana na TBC ya tanzania wakazalisha kitu kinaitwa Star Times ili kutoa huduma za Digital broadcasting kwa TZ hivyo TBC ina share Star Times ,Ni ngapi kwa ngapi hilo sina takwimu kwa sasa.

Kwa lugha nyinge ni kuwa Star Media+TBC=Star Times

Kazi njema.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom