Umiliki wa Mali - Mume na Mke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umiliki wa Mali - Mume na Mke

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kishazi, Jun 15, 2010.

 1. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana JF,

  Kuna swali napenda sana lijadiliwe. Endapo mume au mke kastruggle akanunua mali kama magari, nyumba au viwanja, na thamani mbali mbali. Je, kati ya haya ni lipi sahihi katika umiliki:

  1. Kuandikisha mali kwa jina lake mwenyewe
  2. Kuandikisha mali kwa jina lake na la mkewe au mumewe
  3. Kuandikisha mali kwa jina lake, la mkewe au mumewe na watoto wote.

  Nimekutana na huu mjadala mahali na nikaonelea ni vema niulete kwa great thinkers. Nafahamu humu ndani kuna wataalamu wa maswala ya haki sawa, kuna wataalamu wa mahusiano ya ndoa na kuna wataalamu wa kufikiria between the lines. Na nimelileta humu jamvini kwani nafahamu kuna watu wengi sana hapa nchini na si ajabu duniani wamekutana na changamoto zinazohusiana na umiliki wa mali.

  Kwa sasa nimeweka kapuni maoni niliyoyasikia katika mabishano na maoni yangu pia ili niweze kutoa mwanya kwa watu wengine kufikiria tofauti. Kwa maana nyingine nisitoe muongozo wa mjadala.
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mali ni za wote.Andikisheni kwa majina yote mawili ya mke na mume.Labda kama mmekubaliana kuwa na ndoa ya mkataba na kuwa kila mtu na vitu vyake asiingilie vya mwenzie.
  Kwa ujumla ni makubaliano
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kama mmebahatika kupata watoto mie naona ni vyema kuandika majina ya watoto...
  kama hamna watoto nadhani ni jambo jema mkiweka Mr & Mr Kishazi
  hata linapotokea la kutokea ..ndugu /jamaa na marafiki wakishika Document za family zinakuwa zinaeleweka vyema...
   
 4. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie vyote vimeandikwa majina ya watoto, kila mmoja kabakiwa na chake ulichomkuta nacho kwa jina lake.
   
 5. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Suala la Mali limekuwa tatizo sana kwa dunia ya sasa...

  Kama walivyochangia wengine hapo juu, majina ya watoto yaandikwe maana ndio victims wakubwa in case of anything... la kama hakuna watoto na nyie ni mwili mmoja then viandikishwe kwa Mr. & Mrs.

  Angalizo: Wosia bado muhimu kwa msisitizo
   
 6. T

  Tall JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.Kwa mujibu wa kifungu (a) chini ya kifungu cha 60 cha sehemu ya nne ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971,mali ikinunuliwa kwa jina la mme au mke inachukuliwa ni mali yake.
  2.kifungu cha (b) chini ya kifungu cha 60 cha sehemu ya nne ya sheria hiyo hiyo kinasema kuwa,mali inapoandikwa majina yote mawili inaonyesha,wote mnahaki sawa.
  USHAURI:1. Kama unaona mwenzio amekaa kidhuluma dhuluma basi jenga hoja mbadilishe majina yawe ya wote.
  2. Kama ni mtu mwema na ndugu zake nao watu safi, basi hapo jina lisikutie shida,bado kila mmoja wenu ana haki sawa chini ya kifungu cha 56 ya sheria ya ndoa na talaka ya mwaka 1971 .

  hivi ni kwa mujibu wa ninavyoelewa na ninavyoona inafaa.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa nini mali zenu muwaandike watoto? Wao pia si wanapaswa kutafuta zakwao? Gari langu/letu, halafu niandike jina la mtoto wangu/wetu...manaake nini? Na kama hao watoto tayari wana ndoa zao na familia zao hapo inakuwaje?
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  wapo chini ya miaka 10! ni makubaliano kati yangu na mwenzangu na tupo sawa nao.
   
 9. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Anything we acquire after marriage has got to have both names...vingine vya usingle ife ni vyake/vyangu...kwa majina tu.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu, mali yoyote inayopatika katika ndoa ni mali ya wanandoa wote na hivyo inapendeza zaidi na ni wajibu kwa mali hiyo kuandikwa kwa jina la wanandoa. Hili litasaidia sana pindi kwa bahati mbaya mwanandoa mmoja anapofariki. ndugu kuacha kumbugudhi yule aliyebaki kwa kutaka kurithi mali za "ndugu yao." Kwa hiyo kama mmefanikiwa kupata kiwanja, mmejenga nyumba, mmenunua gari au mmefungua biashara basi ni vizuri hivi vyote vikaandika katika majina ya wanandoa na pia hakuna ubaya kuyaweka hata majina ya watoto wenu. Vinginevyo ukiandika jina lako peke yako utampa wakati mgumu mwenzio kama bahati mbaya mmoja wa wanandoa akafariki na ndugu kuanza kutaka kurithi mali za ndugu yao, lakini ukiwa na hati miliki inayoonyesha majina ya wote katika Title deeds au ownership ya gari au biashara basi wanandugu hawatakuwa na ubavu wa kuanzisha kasheshe dhidi ya mali isiyowahusu.
   
Loading...