Umiliki wa ardhi uwe wa Mtu binafsi au kampuni binafsi (inayomilikiwa na raia). Tuachane na hii ya kumilikiwa na Rais

Landson Tz

JF-Expert Member
May 8, 2011
295
221
Katika uchumi ardhi ni moja wapo ya rasilimali muhimu. Katika biashara na uwekezaji, ardhi ni kati ya rasilimali muhimu sana. Hivyo, umiliki wa rasilimali hii ni jambo la muhimu sana katika kutumia hii rasilimali muhimu. Juu au ndani ya rasilimali hii, rasilimali zingine huwekwa, za muda mfupi na/au za muda mrefu. Kama mtu/kampuni inataka kuwekeza kwenye majengo (real estate) lazima kuwe na ardhi, ukitaka kuwekeza kwenye kilimo lazima uwe na ardhi, hata ukitaka kujenga nyumba ya kuishi ni lazima uwe na ardhi, ukitaka kufuga lazima uwe na ardhi, mifano iko mingi.

Kuna mitazamo tofauti kuhusu namna bora ya umiliki wa rasili hii.

Namna ya kwanza ni “Kumilikiwa na jamii” (Rais kwa niaba ya raia)

Namna ya pili “Kumilikiwa na mtu bninafsi/ kampuni binafsi

Je! namna ipi ni bora zaidi ili kuchochea uwekezaji?

Kazi za ardhi kama rasilimali;tukijikita kwenye kilimo ardhi ni nyenzo muhimu sana ambapo miundo mbinu yote yakiwemo mazao vinakuwa juu ya ardhi. Kwa lugha nyingine huwezi kuvitenganisha. Kwakuwa baadhi ya miundombinu ya kilimo na mazao haviwezi kutenganishwa na ardhi hivyo mmiliki anapaswa awe mmoja badala ya ardhi ya rais miundombinu na mazao ya mtu binafsi au kampuni binafsi.

Matunda yatokanayo na ardhi; kilimo kinasababisha yapatikane mazao mbalimbali yakiwemo ya chakula. Katika kipindi hiki ambacho sio lazima ulime ili ule, chakula cha kutosha kinahitajika sokoni. Hivyo bila kujali ardhi iliyozalisha ina umiliki gani watu wanahitaji chakula sokoni. Hapo ndo hoja ya umiliki wa jamii inapungua nguvu. Kutokana na hali hiyo, tunahitaji kujua ni njia ipi ya umiliki wa ardhi inaweza kuongeza uzalishaji? Mimi naona njia umiliki wa ardhi wa binafsi unaongeza tija zaidi kuliko umiliki wa jamii.

Katika nchi yetu, tangu uhuru umiliki wa ardhi umekuwa ni wa jamii na kinachoendelea kwenye kilimo kila mmoja anaelewa. Wananchi wanaoshiriki kwenye kilimo wengi wao ni maskini ambao kimsingi hawana namna nyingine ya kujikimu. Na kama wangeweza kuwa namna nyingine basi wengi wao wasingelima. Sekta ya kilimo ndio inayoongoza kwa kufukarisha watu kwani kilimo cha sasa kinahitaji uwekezaji mkubwa unaohitaji mtaji mkubwa ila wameachwa maskini wahangaike nacho bila mafanikio.

Uwekezaji wa kudumu kwenye ardhi unatia moyo wawekezaji (wananchi) kama ardhi inakuwa inamilikiwa na mtu binafsi au kampuni. Ardhi kuwa mikononi mwa Rais kunapunguza marali ya uwekezaji. Rais na wanaomzunguka ni bianadamu na wana mapungufu, hivyo kuna uwezekano wa hujuma. Hujuma hizi zinaweza kuanzia kwa raia wengine na kuishinikiza serikali kufanya unyang’anyi kwa kusingizia maslahi ya umma.

UMILIKI WA ARDHI WA UMMA KUPITIA RAIS NI MSINGI WA UJAMAA – BADO TUMELEWA NA UJAMAA?

Ni katika mfumo wa Ujamaa ambapo ardhi umilikiwa na jamii. Katika mifumo mingine ardhi ni mali kama zilivyo mali nyingie na inapaswa itumike kikaimilifu kuzalisha mali zingine. Kwa mfumo wa Ujamaa serikali ushiriki katika shughuli za uzallishaji kama kilimo laakini mifumo mingine kama uliberali na ubepari serikali haishiriki katika uzalishaji. Kutokana na hali hakuna haja ya serikali yetu baada ya kuachana na Ujamaa kuendelea kung’ang’ani ardhi. Mimi naamini serikali ikimilikisha ardhi kwa raia itaongeza tija na uwekezaji utaongezeka.

Kama tutaendelea na mfumo huu wakati idadi ya watu inaongezeka (inakadiriwa kufikia milioni 100 (2050) kwa kasi ipo siku nchi itaingia kwenye njaa au kuagiza asilimia kubwa ya chakula kutoka nje. Maana waliachiwa kilimo kwa saa ni wale wasio na la kupoteza wanalima wakitaka na mara nyingi sio kwa biashara bali kwa matumizi ya kaya zao.

Kwa sasa miji inaendelea kukua, inahitaji chakula sokoni na si kumiliki ardhi. Tukibadili sera ya ardhi na kuanza kumilikisha kwa raia badala ya kuwakodisha naamini raia wenye nia na mitaji mikubwa wataingi kwenye kilimo na ufugaji hivyo kuleta tija katika sekta ya kilimo na kukuza ajira na kuongeza upatikanaji wa mazao kikiwemo chakula.

Mtazamo wa Landson Tanzania.
 
Upo sahihi kabisa! Sema wengi nchini Tanzania hawapendi kumiliki chochote. Hata akili zao mara nyingi wanazikabidhi kwa mamlaka fulani.
 
CCM wana sera mbovumbovu za kimaskini lakini kwa hili hapana. Ardhi ibaki hivihivi mali ya serikali. Vinginevyo ardhi nzuri yote itamilikiwa na wachache na vizazi vyao. Hii ya hati kuexpire baada ya miaka 33 au 99 ni nzuri sana.
 
Mimi naona ubaki ulivyo tafuteni njia itakayochochea/stimulate serikali itumie ardhi fully
 
Ingekuwa hivyo usingepata hicho kiwanja ulichonacho
Ujamaa unakusumbua.
Kwani kiwanja nilipewa bure au niliuziwa tena bei mbaya na raia wenzangu. Ardhi ya nchi hii sehemu kubwa inamilikwa kwa mfumo wa kupangishwa na serikali kwa raia. Pamoja na kuwa ardhi karibia yote imeshikiliwa na watu ila hawaiendelezi kwa sababu ya umiliki feki. Kama hujui chukua jembe lima popote pale hata porini uone kama mwenye ardhi hatajitokeza.
 
Na wengi kumbuka hawana hata fedha ya kununua kiwanja wanaishia kupanga mjini kwenye nyumba za watu. Ujamaa gani wa mwanaume kuishi kwenye nyumba ya mwanaume mwenzie.
Kama ni ujamaa usiishie kwenye ardhi!!
 
Mleta mada ukitaka kujua ubaya ya hiki unachoshabikia nenda hapo Kenya. Mfumo wetu wa kumiliki Ardhi ni mzuri sana. Ubaki ulivyo
Shida unayoiona ni kwa sababu Kenya na nchi nyingi za Africa hakuna ajira ndio maana ukitaka kumuona maskini vizuri nenda vijijin amabapo kila mmoja ana pakulima. Kama ardhi inamaliza umaskini nchini kusingekuwa na maskini hata mmoja. Ardhi ya kupangishwa na serikali ni kichaka cha kuwachia maskini kwa kisingizio cha kuwaita wakulima!

Ardhi ikiwekewa utaratibu wa kumuhakikishia anayoimiliki usalama wa mali zake ni kiwanda namba moja. Tusidanganyike karne hii ya 21, tunahitaji chakula sokoni kwa bei nafuu na si kumiliki ardhi. Wenye uwezo wa kuwekeza kwenye kilimo wapewe fursa watuzalishie chakula cha kutosha na sisi tufanye kazi nyingine.

Katika ulimwengu wa sasa (acha uzembe wa waafrika) ajira nje ya kilimo ni nyingi zaidi.
 
Katika uchumi ardhi ni moja wapo ya rasilimali muhimu. Katika biashara na uwekezaji, ardhi ni kati ya rasilimali muhimu sana. Hivyo, umiliki wa rasilimali hii ni jambo la muhimu sana katika kutumia hii rasilimali muhimu. Juu au ndani ya rasilimali hii, rasilimali zingine huwekwa, za muda mfupi na/au za muda mrefu. Kama mtu/kampuni inataka kuwekeza kwenye majengo (real estate) lazima kuwe na ardhi, ukitaka kuwekeza kwenye kilimo
Mmh hoja nzuri. Ila tuwasubr wataalamu wakusaidie kipi ni kizuri ardhi ikimilikiwa na serikali au binafsi
 
Mja

Mjadala mpana kubinafsisha hakuitaji kukurupuka shehk wangu, asilimia80% ya wanyonge watarud utumwani. Mjadala uendelee
Ardhi kimekuwa kichaka cha kutelekezea wanyonge, maana pamoja na ardhi kuwepo kwa utaratibu kwa miaka mingi bado idadi ya wanyonge imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka
 
Moja kati ya makosa yaliyofanywa na waasisi wa taifa hili baada ya kupata mamlaka ya kujitawala ni hili la mgawanyo wa ardhi kutokukamilika na la pili ambalo litakuja kutugharimu miaka ijayo ni kumezwa kwa Tanganyika kwenye muungano.

Umiliki wa ardhi unapaswa kuwa chini ya mtu binafsi kwanza kabla ya kuwekwa rehani kwenye mamlaka za kiserikali.

Utaratibu uliopo sasa wa ardhi yote kuwa mali ya Rais ulipaswa kuwepo kwa kipindi cha mpito wakati ardhi ikigawiwa kwa usawa na kumilikisha kila kipande cha ardhi kwa kila raia ambaye kimsingi ndio mmiliki asilia.

Ulaghai uliofanyika baada ya uhuru ni huu: kugawa mikoa wilaya kata na majimbo, kuzimilikisha Halmashauri huku mwananchi akichukuliwa kama mpangaji kwenye ardhi ambayo yeye ndio mmiliki!.

Uhuni huu haupaswi kuendelezwa na Wizara ya ardhi sasa bali wanatakiwa kupima na kumilikishwa ardhi kwa kila raia iwe ndio mtaji wake na rasilimali.

Kitendo cha mchakato kama huo kutoendelea ndicho kilichotoa mifano kama Kenya, mtu kama Kenyatta kujimilikisha zaidi ya nusu ya ardhi ya Kenya kwa upendeleo. Kule Uganda ardhi iliyokuwa chini ya miliki ya Kabaka haijaguswa hadi leo.

Labda tupate uzoefu nchi zingine zilizofanikiwa kwenye mgawanyo wa ardhi zilifanyaje?...

Chukulia Bara la Ulaya, nchi moja kama mfano( sitaitaja).
Baada tu ya vita vya pili vya Dunia kupitia ule mpango wa Marshall plan, nchi hiyo ilifanya utambuzi wa ardhi yote ndani ya mipaka yake, ikawatambua wamiliki wa awali wa kila kipande cha ardhi na kurasmisha ardhi yao, Kila mwananchi aligawiwa ekari nne, mashamba binafsi pia na viwanda vilitambuliwa na kumilikishwa kwa wenyewe na kuhakikisha kuwa hakuna aliyeachwa nyuma.

Baada ya mgawanyo huo unaogusa moja kwa moja watu binafsi na makampuni binafsi ardhi iliyobaki ndio iliwekwa chini ya umiliki was Serikali. Sijui sisi tunakwama wapi, hadi leo hata upimaji ardhi na kutoa hati ya umiliki bado ni mgogoro licha ya kuwepo Wizara ya ardhi..... Labda tumelaaniwa na aliyetulaani aliisha kufa.
 
Moja kati ya makosa yaliyofanywa na waasisi wa taifa hili baada ya kupata mamlaka ya kujitawala ni hili la mgawanyo wa ardhi kutokukamilika na la pili ambalo litakuja kutugharimu miaka ijayo ni kumezwa kwa Tanganyika kwenye muungano.

Umiliki wa ardhi unapaswa kuwa chini ya mtu binafsi kwanza kabla ya kuwekwa rehani kwenye mamlaka za kiserikali.

Utaratibu uliopo sasa wa ardhi yote kuwa mali ya Rais ulipaswa kuwepo kwa kipindi cha mpito wakati ardhi ikigawiwa kwa usawa na kumilikisha kila kipande cha ardhi kwa kila raia ambaye kimsingi ndio mmiliki asilia.

Ulaghai uliofanyika baada ya uhuru ni hui: kugawa mikoa wilaya kata na majimbo, kuzimilikisha Halmashauri huku mwananchi akichukuliwa kama mpangaji kwenye ardhi ambayo yeye ndio mmiliki!.

Uhuni huu haupaswi kuendelezwa na Wizara ya ardhi sasa bali wanatakiwa kupima na kumilikishwa ardhi kwa kila raia iwe ndio mtaji wake na rasilimali.

Kitengo cha mchakato kama huo kutoendelea ndicho kilichotoa mifano kama Kenya, mtu kama Kenyatta kujimilikisha zaidi ya nusu ya ardhi ya Kenya kwa upendeleo. Kule Uganda ardhi iliyokuwa chini ya milking ya Kabaka haijaguswa hadi leo.

Labda tupate uzoefu nchi zingine zilizofanikiwa kwenye mgawanyo wa ardhi zilifanyaje?...

Chukulia Bara la Ulaya, nchi moja kama mfano( sitaitaja).
Baada tu ya vita vya pili vya Dunia kupitia ule mpango wa Marshall plan, nchi hiyo ilifanya utambuzi wa ardhi yote ndani ya mipaka yake, ikawatambua wamiliki wa awali wa kila kipande cha ardhi na kurasmisha ardhi yao, Kila mwananchi aligawiwa ekari nne, mashamba binafsi pia na viwanda vilitambuliwa na kumilikishwa kwa wenyewe na kuhakikisha kuwa hakuna aliyeachwa nyuma.

Baada ya mgawanyo huo unaogusa moja kwa moja watu binafsi na makampuni binafsi ardhi iliyobaki ndio iliwekwa chini ya umiliki was Serikali. Sijui sisi tunakwama wapi, hadi leo hata upimaji ardhi na kutoa hati ya umiliki bado ni mgogoro licha ya kuwepo Wizara ya ardhi..... Labda tumelaaniwa na aliyetulaani aliisha kufa.
Asante kwa mchango mzuri,
Kitendo cha serikali kumiliki ardhi na kuikodisha kwa wananchi ni cha hatari sana katika msitakabali wa uhuru wa mwanadamu. Na ndio maana kuna watu wanaamini kuwa uhuru bado hatujapata, tulitoka kwa mkoloni mweupe tukaenda kwa mkoloni mweusi!! Swala la umiliki wa ardhi kuwa wa serikali, ni mfumo wa kijamaa na sasa je sisi ni wajamaa?
Maendeleo ya kilimo hayawezi kupatikana kama ardhi itakuwa ya rais.
Watu wanasema umiliki wa aina hii mzuri maana watu wote watakuwa na haki ya ardhi, lakini tujiulize sasa ni zaidi ya miaka 60 tangu uhuru, mfumo huu umesaidia nini katika kuondoa umaskini?
 
Hii migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima ni matokeo ya mgawanyo wa ardhi usio na usawa. Itakuja siku tu wananchi wataidai kwa nguvu.
 
Asante kwa mchango mzuri,
Kitendo cha serikali kumiliki ardhi na kuikodisha kwa wananchi ni cha hatari sana katika msitakabali wa uhuru wa mwanadamu. Na ndio maana kuna watu wanaamini kuwa uhuru bado hatujapata, tulitoka kwa mkoloni mweupe tukaenda kwa mkoloni mweusi!! Swala la umiliki wa ardhi kuwa wa serikali, ni mfumo wa kijamaa na sasa je sisi ni wajamaa?
Maendeleo ya kilimo hayawezi kupatikana kama ardhi itakuwa ya rais.
Watu wanasema umiliki wa aina hii mzuri maana watu wote watakuwa na haki ya ardhi, lakini tujiulize sasa ni zaidi ya miaka 60 tangu uhuru, mfumo huu umesaidia nini katika kuondoa umaskini?
Nimekumbuka uzi huu murua, JF admin uweke front page siku zote
 
Back
Top Bottom