Ng'azagala
JF-Expert Member
- Jun 7, 2008
- 1,286
- 221
Wana forums
kwa manufaa ya nchi yetu ningependa tujadili suala hili la umiliki wa ardhi kati ya system mbili Lease hold ambayo inatumika sasa na nyingine ni Free hold. nimeona makundi mbalimbali yakijadili haya masuala hasa NGO ya HAKIARIDHI na wamekuwa wakisisitiza kwamba Tanzania ihamie kwenye Free Hold System iachane na Lease hold. ni vizuri tukajadili kwa upana hasa tukiangalia hali ya uchumi wa mtu binafsi, na uzuri na ubaya wa kila system katika nchi yetu.
kwa kifupi Tanzania tunatumia lease kwa maana mwananchi anakodishiwa ardhi kwa miaka kadhaa kisha anaweza kuomba kuongeza muda wa umiliki lakini wakati wote ardhi inakuwa chini ya mamlaka ya serikali (President)
Free hold ni umiliki usio na mipaka wa mwananchi binafsi, na kwa sababu ardhi ni pesa! mara nyingi wenye pesa ndiyo watamiliki ardhi bila mipaka. Hii ilitumika wakati wa ukoloni na bado inatumika sana nchi za kibepari na hata nchi nyingi za afrika kama Zimbabwe, Kenya nk. Ukifuatilia historia ya Tanzania utaratibu wa Free hold ulikuwepo wakati wa ukoloni na ulipigwa marufuku na Mwl Nyerere baada ya Uhuru kwani tayari wazungu walikuwa wamenunua sehemu kubwa ya Tanzania.
nawasilisha