Umiliki wa Ardhi; Rasimu imekaa Kimya

Small Boy

Senior Member
Jul 12, 2007
142
38
Mojawapo ya mambo yanalalamikiwa kwenye katiba ya sasa na sheria zake ni pamoja na swala la umiliki wa ardhi;
1. Swala la Raisi kuwa na mamlaka na ardhi yote
2. Swala la wageni kumiliki ardhi
3. Kiasi cha Ardhi mtu mmoja anachoweza kumiliki
n.k

Rasimu ya katiba mpya nayo imekaa kimya kuhusu Ardhi..Hii ina maana gani?
 
Ni kweli rasimu imeongea umiliki wa mali kwa ujumla lakini haijawa specific kwa suala la ardhi.Ukisoma mambo ya muungano, suala la ardhi halimo hivyo si la muungano na hivyo halishughulikiwi na katiba hii Mambo ya Muungano
________________
1. Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
3. Uraia na Uhamiaji;
4. Sarafu na Benki Kuu;
5. Mambo ya Nje;
6. Usajili wa Vyama vya Siasa; na
7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na
mambo ya Muungano.

Hapana msi panic, ardhi siyo suala la muungano na hivyo halipaswi kuwa katika katiba ya muungano.
Hilo litashughulikiwa na serikali washirika. Kwahiyo Tanganyika itashughulikia ardhi yake kama znz, ndiyo maana hulioni katika rasimu. Rasimu ya Tanganyika ndiyo itakuwa na suala hilo.

Ni kama elimu ya juu na ajira vyote vimeondolewa.
 
Umewajibu vizuri sana mkuu.

Watu wanakurupuka sana kupost thread ili waonekane nao wanajua mambo fulani! #muwe mnasoma na kuelewa kabla ya kuleta shuzi zenu.
 
aisee umenipa macho kuona!!! kwa hiyo katiba hii haitasema lolote kwa masuala ya Tanganyika yetu? basi hayo mapungufu yatatupa mwanya wa kudai turejeshewe Tanganyika yetu na kisha tupe katiba yetu itakayozungumzia masuala ya reslimali zetu!
 
Umewajibu vizuri sana mkuu.

Watu wanakurupuka sana kupost thread ili waonekane nao wanajua mambo fulani! #muwe mnasoma na kuelewa kabla ya kuleta shuzi zenu.
taratibu ndugu hakuna aliyeleta shuzi zake kwenye mada hii. hii mada imewekwa ili kila mmoja aseme hisia na mawazo yake. usiwafunge watu midomo acha waseme! kama katiba hiyo haitogusa na kueleza bayana juu ya raslimali za Tanganyika basi tunaitaka Tanganyika yetu na katiba yake!
 
Umewajibu vizuri sana mkuu.

Watu wanakurupuka sana kupost thread ili waonekane nao wanajua mambo fulani! #muwe mnasoma na kuelewa kabla ya kuleta shuzi zenu.

Tatizo watu hawasomi kama kawaida ya watanzania, mmeambiwa someni rasimu na mmepewa wiki tatu karibu zinaisha hamjasoma mnabaki kulalamika kama kawaida yenu watanzania.aliyewaloga watanzania ni yule aliyechakachua mtaala wa elimu, kamali kabisa. Nawasihi msome mimi nimeanza tangu jtatu nimefikia sura ya tano ,mdogo mdogo hadi nimalize nijenge uelewa.
 
Kweli mkuu. Kawaida ya wabongo kukurupuka! Nahisi alowaloga alishakufa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom