Umeya wazua kizaazaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeya wazua kizaazaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Dec 25, 2010.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Umeya wazua kizaazaa
  • CHADEMA wataka chaguzi ziahirishwe

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa kusitisha chaguzi za mameya katika halmashauri za jiji la Mwanza, Arusha na Kigoma kwa kuhofia kuendelea kuvunjika kwa amani.
  Wakati chama kikitoa msimamo huo, jana msimamizi wa uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi, alimuengua mgombea wa CHADEMA, Grace Shellukindo, kwa kile alichokieleza kuwa hana sifa za kuwania nafasi hiyo, hali iliyoibua mzozo mkubwa.
  Katika uchaguzi huo Didas Masaburi wa CCM, aliibuka kuwa mshindi kwa kura za ndio baada ya diwani wa Chama cha Wananchi CUF, Jumanne Bunjo, kujitoa dakika za mwisho wakati wa uchaguzi huo jana.
  Kadhalika msimamo wa CHADEMA kumtaka Msajili wa kusitisha chaguzi katika majiji hayo ni kutaka fursa ya kufanya mazungumzo kwa ajili ya kusuluhisha mizozo iliyoibuka toka pande zinazovutana.
  Katika mazungumzo hayo, CHADEMA wanataka yamshirikishe Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Hatua yao hiyo imekuja siku chache baada ya kutokea vurugu katika uchaguzi wa mameya katika halmashauri hizo ambao umevurugika kwa sababu ambazo zina utata jambo ambalo limesababisha uvunjifu wa amani na hivyo kulazimika kukutana na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kupata muafaka.
  Katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, alikutana na Tendwa Desemba 22 juu ya kuzungumzia hali hiyo ya uvunjifu wa amani, kabla ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Saidi Mwema ambapo chama hicho kimeamua kusitisha maandamano ya amani kilichopanga kuyafanya Desemba 30, mwaka huu.
  Alisema kimeamua kusitisha maandamano hayo kwa masharti kuwe na mkutano wa ngazi za juu utakaomhusisha Waziri Mkuu na viongozi wa TAMISEMI, utakaoratibiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa siku na mahala atakapopanga.
  Alisema iwapo hadi Januri 4 hakutakuwa na hatua yoyote kuhusu kuwepo kwa majadiliano, CHADEMA italazimika kuitisha maandamano ya amani Januari 5 bila kibali cha polisi.
  Aidha, chama hicho kimetaka kuchukuliwa hatua kali dhidi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, viongozi wa TAMISEMI na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ambao walishiriki kuvuruga uchaguzi huo ikiwemo kumkamata Mbunge wa Jimbo hilo, Godbless Lema, kinyume cha sheria.
  Kwa upande wa uchaguzi wa mameya uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Masaburi aliibuka mshindi kwa kura za ndiyo 103 za madiwani 125, CHADEMA wanadai kuchezewa rafu baada ya msimamizi wa uchaguzi huo Bakari Kingobi kumuengua Grace Shellukindo, dakika za mwisho.
  “Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa umeya, mgombea Grace Shullukindo, hana sifa stahili za kuwania Umeya wa jiji kutokana na kutokuwa mjumbe wa kata na pia ni wa Viti Maalum,” alisema Kingobi.
  Uchaguzi huo ulitaka uingie dosari, baada ya kuibuka mzozo kati ya wajumbe wa CHADEMA na wa CCM kwanza juu ya uhalali wa Mkurugenzi wa Jiji, Kingobi kuwa msimamizi badala ya kuteuliwa mjumbe mwingine kusimamia uchaguzi.
  Pili CHADEMA wanalalamika kutopewa taratibu za uchaguzi pamoja na sifa anazotakiwa kuwa nazo mgombea kabla ya uchaguzi, badala yake walishtukizia suala hilo likitokea dakika za mwisho kwenye uchaguzi jana.
  Mjumbe kutoka CHADEMA, John Mnyika, katika hoja yake alisema: “Kwanza tuweke sawa wajumbe waelewe…., moja hatukupewa kanuni ya uchaguzi huu, pili kwa mujibu wa kanuni hizo tulitakiwa tutaarifiwe siku saba kabla ya uchaguzi huu, hii ni kwa sababu kama kungekuwa lolote la kuhitajika tulifanye,” alisema Mnyika.
  Kwa maelezo ya Mnyika, hatua ya msimamizi wa uchaguzi huo ya kumuengua mgombea wa CHADEMA lilifanywa kwa kukurupuka, kwani chama kilitakiwa kitaarifiwe kabla ya uamuzi kufanyika.


  [​IMG]


  juu[​IMG] [​IMG]
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa staili hii ya kutafuta ushindi kwa hila, huo ustaarabu ambao ccm imekuwa ikijivunia miaka nenda miaka rudi sasa umekwenda wapi!
   
Loading...