Umeya wa jiji la DSM ni kesho, UKAWA kuweni makini na Wilson Kabwe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,744
239,394
Huyu ni mtu hatari anayefahamika kwa mbinu zake za kizamani , hana aibu linapokuja suala la kuibeba ccm.

Yaliyotokea Mwanza kila mmoja anayakumbuka.

Yuko tayari kuvunja sheria kuhakikisha chama chake kinashinda , si kwa bao la mkono tu bali hata kama mpira uko katikati ya uwanja anaweza kusema ni goli .

Kila la heri UKAWA namba hazijawahi kudanganya .
 
Nafikiri kwa sababu idadi ya Madiwani (Wapiga kura) wanajulikana, nashauri wao (Ukawa) wapige kura ya wazi ili ijulikane kwa kila mtu kwamba wamepata kura ngapi ili waweze kulinganisha na wale wa CCM wataopiga na kuweka karatasi kwenye Sanduku.
Kinyume na hapo ni kwamba, shillingi ukiirusha juu haiwezi kamwe kusimamaa ikishafika chini, Ukawa watumie akili ya ziada.
 
Kwa sababu CCM hawajui hata hesabu wana ndoto za kushinda umeya wa jiji dar?
 
Kila la heri UKAWA namba hazijawahi kudanganya .

UKAWA mna matatizo tena makubwa.Angalia mnataka meya achaguliwe kwa kuangalia vyama badala ya uwezo.Lakini kule bungeni Dodoma mlikuwa mkipiga kelele sana kuwa Spika na naibu spika wanatakiwa wachaguliwe si kwa kuangalia vyama bali uwezo

Hamna msimamo watu wa UKAWA

Lakini ningekuwa mimi hicho cha umeya ningeachia CCM ILI KUGAWANA LAWAMA za kushindwa kutatua kero za jiji.
Sasa hivi umeya wa ILala na Kinondoni kote ni UKAWA.Lakini takataka ziko kila kona,mabarabara yako mahandaki matupu kwa siku mia hakuna kilichofanyika na mbwembwe zao zote za kutaka kugeuza jiji liwe kama Kigali kama walivyokuwa wakibweka UKAWA kwenye kampeni.

Anyway ruksa chagueni mtakavyo ila mwisho wa siku mtalijua jiji la dar es salaam.Na mtajuta kulifahamu na kulivalia majoho ya umeya.
 
MNA hakika wajumbe wote wa Ukawa wapo Dar? Tusije sikia Mara Fulani na Fulani hawapo ni wagonjwa na Fulani hajulikani alipo
 
Any update please!!!! Kitu gani kinaendelea huko? Tujulisheni mlio karibu.
 
Yaani ni kama kumpambanisha Tyson na mada maugo
Ngoja tusubiri "Super Tuesday" tuone nini kitatokea, lakini hoja yangu ni kwamba kura zote za maoni zinaonesha kuwa kama Trump atashinda kwenye "Primaries" basi Demokratik ama akiwa ni Bennie Sanders anayezidi kuwavutia wana demokratik wenzake, au Hilary Clinton anayeungwa mkono na wenye chama chao "Establishment" basi ushindi wa hao wawili utakuwa ni kama kumsukuma mlevi.

Ndiyo maana tangu wiki hii ianze wanachama maarufu wa Republikan wameanza kutangaza "endorsement" kumuunga mkono wa Marc Rubio kama jitihada zao za kumzuia Trump kushinda ingawa wachunguzi wa mambo wanadai wamechelewa kuchukua hatua hiyo ya kuzuia Trump kushinda.

Wamarekani kwa asili ni watu wanaopenda ubabe na wanadai kwa kipindi chote ambacho obama amekuwa Madarakani alifanya mambo yake mengi kwa kutegemea diplomasia!! Kwa sasa wanataka kuwa na Rais mwenye kufanya maamuzi bila ya kumwangalia mtu usoni na wagombea wanaoangukia kwenye "Category" hiyo ni Bennie Sanders na Donald Trump, wote wawili wanapingwa na wao wanawapinga wenye ushawishi kwenye vyama vyao vya Demokratik na Republikan!!
 
Back
Top Bottom